Ukweli kuhusu wafuasi na wanachama wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu wafuasi na wanachama wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KABUKANOGE, Mar 21, 2012.

 1. K

  KABUKANOGE Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina nia yangu ya kuwatukana watanzania wenzangu, ila penye ukweli lazima pawe wazi.
  Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu siasa za Tanzania, na hatimae nikagundua kuwa si wanachama wa upinzani wala wale wa CCM wanaojua vilivyo nini lengo na itikadi ya chama chao,

  Kwa upande wa upinzani wafuasi wao hufuata na kusapoti vyama vyao kwa moyo wa dhati na wakiamini kuwa wakipewa nafasi wanaweza kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kuweza kutumia rasilimali za nchi kuinufaisha nchi yetu.

  Ila kwa upande wa CCM hali ni tofauti kwani wafuasi wao ukweli ni kwamba wako tofauti mno na kwa haraka nimeweza kuwaweka katika makundi kama manne

  1. Wale ambao ni vigogo, hawa ni wale ambao hunufaika na chama mojo kwa moja, na ambao hutumia migongo ya wanyonge kujinufaisha na system, hawa ni viongozi, watoto wa vigogo, kama uvccm,wakuu wawilaya na mikoa,wenyeviti na wengineo ambao hata ukiwauliza wataifanyia nini Tanzania wao kama viongozi hawawezi kukujibu lamaana zaidizaidi watakwambia watanzania wanapenda lawama tu

  2.Kada ya kati, hawa ni kama fisi anaye subiri mkono udondoke naye aokote, hawa ni pamoja na walioko vyuoni, baadhi ya wafanyakazi na baadhi ya watu maarufu, hawa hujipandekeza sana ili angarau wateuliwe katika nafasi mbalimbali hili nikundi ambalo halina nguvu kubwa sana kwani nijepesi kubadilika.

  3.Waoga na wanawake, Hili nikundi kubwa sana ambalo wakati mwingine huwa halilidhishwi na mwenendo wa nchi yao, kwani haliambulii kitu, ila ni waoga wa kutupwa, likiambiwa eti mkichagua mpinzani kutakuwa na vita huogopa hata kufika kwenye kampeni, na wakati mwingine likiona mtu mwenye kitambi kikubwa kama Mkapa, hudhani kuwa ndiye mwenye uwezo wa kuongoza, na hutishiwa sana na kauli za wanasiasa kama ile kauli aliyosema Mkapa kuwa hawatakuwa tayari kuiachia nchi kwa CUF kule Zanzibar kwa njia ya karatasi.

  4.Masikini na wajinga, Hili ni kundi ambalo ukweli halijui linaenda wapi wala kutoka, na hutegemea fadhira ya tisheti na,kanga na kofia na mda mwingine hawana chakula na hufikiria kuwa wanapokuwa wanapewa vyakula, kabga na kofia wataendelea kupewa siku zote na hawajui kuwa ni kwamuda wakampeni tu, na wengine hufikiri kuwa wanasiasa ndo watakao inua maisha yao huku wakitimiwa na wanasiasa hao kujiimarisha asilimia kubwa wako vijijini japokuwa hata mjini kama dar niwengi sana,

  KAZI IPO TUWAOMBEE ILI KILA MTU AJUE ANALO FANYA NA AFANYE UAMUZI KWA UELEWA MPANA
   
 2. K

  KABUKANOGE Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du! kazi ipo
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru nawe umeliona hilo jambo; elimu ya uraia vijijini mbeeeele kama tai kisha CCM kumomonyoka zaidi ya hivi leo kirahisi tu kama mkate mkuuuubwa unapochovya ndani ya chai.
   
 4. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ..........tuendelee kuelimisha tusikate tamaa......Freedom is coming 2moro
   
Loading...