Niliwahi sikia vampire wapo, ila so mama tuonavyo ktk movie , mama no Bulgaria , sjui Slovakia, kuna popo wanyonya damu, inasemekana wapo ktk mapango hao wakikuuma unabadilika na kuwa na vijitabia flan tofauti, pia kulikuwa na jamii ya mavampire ambao walikuwa wakila majani na damu ya wanyama was porini, Mimi naamini vampire wapo ila si mama tuonavyo ktk movie, kingine mwaka 2010 niliwahi kumuona mtoto Ana memo mama Vampire nchini Burundi, huyu mtoto baba yake ni mkongoman na mama yake ni mwarabu , wakati namuona huyu mtoto alikuwa na miaka minne alikuwa na meno marefu yale manne juu na chini pia yale meno hayakuwa meupe kama mengine, yale manne yalikuwa yana rangi kama ya dhahabu hivi , pia huyu mtoto alikuwa ana hasira muda wote na alikuwa anakula nyama mbichi kama haitawekwa sehemu nzuri, nilijaribu kuongea na mamayake kujua amechukua hatua gani kuhusu mwanaye akasema amejaribu kumpeleka kila mahari ,ila akasema huko Congo ukweni wamemwambia yule mtoto akifikisha miaka saba atakufa, au wakijaribu kuyatoa pia atakufa na ndio sababu wakahama congo kwenda burundi ili kunusuru maisha ya mwanae, wakati anasema hayo alikuwa mwenye huzuni sana, skupenda kuendelea kumuuliza maswali mengine sababu hata mimi sikujua ni jinsi gani ningemsaidia. Nikaishia hapo.. Mpaka leo sijajua hatma ya yule mtoto maana miaka saba ishafika sasa... Mimi naamini wapo ila si kama tuonavyo vituko vya wazungu.