Ukweli kuhusu Tanzania yetu na uchaguzi

Sep 12, 2020
2
1
Habarigani! Watanzania,

Tanzania ni nchi nzuri Sana ambayo imejaaliwa kilakitu cha thamani, Amani na upendo kitu ambacho ni dhahabu kuliko vyote duniani lakini siku zote m/mungu mwingi wa rehema na upendo hawezikupa kila kitu. Bali sisi tukanyimwa maarifa likini hii sio sababu japo akili tunazo.

Lakini labda niseme jambo" hakika ewe kiongozi mtiifu usiogopa wala kubabaishwa na wazungu msema kweli ambaye umeletwa na M/Mungu kwetu sisi. Je pia na wewe hauyaoni" walio sema unaongoza kundoo ambao wanaangalia chini wakitafuta riziki ndogo Kwa mateso na shida zillio kithiri wamekupa wewe kura zao.

Viongozi wetu wa Tanzania kwanini mmefikia hatua hii ya kinyama kila mara mkihitaji kura zetu mnajinadi Kwa ahadi nzuri? Tukawaamini mara ya Kwanza na kuwapa dhamana ya kwenda mstari wa mbele kutupambania ikiwa tuliwapigia kura zetu huku jua linatuchoma tumepanga foleni, kiu na njaa tukiamini mtatukomboa leo mnataka tena kura zetu. Tanzania imejaa viongozi wenye umimi na ufisadi wakizuia haki isitendeke ili wabaki juu wakila ubwabwa na toothpick.

Sio wao walitaka democracy wakaona inawabana sasa wanaikata kwakuwapa kesi wapinzani ili waozee jela, sio wao ambo wali ifanya tume huru kuwa kama ndo remote ya kupeana madaraka ili waendelee na Kula mema ya nchi .

Au mmesahau kwamba tume ya uchaguzi sio huru tena. Wapinzani mbona mnakuwa waoga kitu gani kinawashinda bila nyinyi nchi haitoenda japokuwa sidhani kama vurugu na kashfa na kusema Mimi nilifanyiwa hivi na vile kunyooshea kidole serikalini ukisahau vinne vinakiangalia.

Ndugu zangu watanzania!

Watanzania acheni mihemko kwani tuseme mmesahau wajibu wenu wa kumkagua raisi wenu na kumhoji leo wamerudi wanaomba kura tena . Kwanini mnakaa kimya Kwa dhulma mnayotendewa kuhusu gesi imebaki storry watu wachache wakifaidika. Hivi ndugu zangu hamjiulizi gesi yetu wenyewe kwanini tunauziwa?

Unafahamu kwamba ni haki yako ya msingi kupata gesi bure lakini kilichobaki tunauziwa watanzania ikiwa bado wanatafuna kodi zetu huku wakitupangia madaraja jinsi ya ulaji huku wakiishi na familia zao vizuri, huku watoto wao wakiishi vema ulaya au america huku Kwa ujombani na ibabani wakigawana mikoa. Hivi watanzania mnajua kwamba nihaki yako kupata kila kitu bure ewe mtanzania ihurumie kura yako kwani hicho kikura chako kina thamani Sana.

Watanzania tumuombe mungu sana.

Ahsante!
 
Back
Top Bottom