Ukweli kuhusu Ndege ya Air Tanzania "kuegeshwa" bila kuruka

Hahaaa kwa ulivyoeleza mkuu inaonekana ni mtu wa serikali nikuulize tu hizi ndege sio salama sana vitu vya kukurupuka havijawahi muacha mtu salama.
 
barafu mkuu upo wapi sasa mbona husemi? halafu zile ndege nyingine 2 hivi zinakuja lini? ngoja niende kwa Mange kwanza nikaangalie hoja yake ikisemaje...maana huyu dada amekuwa mpiaji filimbi mzuri kwani taarifa zake na yeye hutoa hukuhuku kwenye source kabisa...ni sawa na ww upo nje ya bongo na umepata haya majibu I sure kutoka kwenye source za ndani hapahapa...
 
Ok!

Matengenezo hayo au marekebisho(Service) yanachukua muda gani...

Mbona Ndege za Fast Jet na Precision Air hatujawahi ona ziki paki kwaajili ya matengenezo...
Iweje bombadier....??

Ningeona upo sawa atleast kwa kutolea mifano ya Fast Jet na Precion Air..ila umetolea mifano ya Qatar, KLM, .....
 
Mpaka sasa Precision ndege zake tatu zipo chini sbb ya matengenezo
Fastjet wamebakiza ndege moja tu....Na juzi alisitisha safari ya Mbeya na Mwanza sbb ya matengenezo na watu wakalala hotelini!!
Mkuu bruda ni mambo ya kawaida,kama vile mfungo wa kila mara wa mapadre,nyie mnaita "Retreat"
Kwa mkleri si ajabu
 
barafu mkuu upo wapi sasa mbona husemi? halafu zile ndege nyingine 2 hivi zinakuja lini? ngoja niende kwa Mange kwanza nikaangalie hoja yake ikisemaje...maana huyu dada amekuwa mpiaji filimbi mzuri kwani taarifa zake na yeye hutoa hukuhuku kwenye source kabisa...ni sawa na ww upo nje ya bongo na umepata haya majibu I sure kutoka kwenye source za ndani hapahapa...
Nimekuja kupumzika kidogo mkuu injinia
 
Nimekuja kupumzika kidogo mkuu injinia
Sawa kula bata boss barafu Nimepitia hoja ya Mange nadhani inahitaji majibu mazuri Zaidi maana pia kasema hiyo ndege ilishindwa kuchukua abiria na wakafaulishwa kwenye precision..(I'm not sure)...isitoshe kuna abiria wa pale Songwe wamechomeshwa sana mahindi kuisubiria [HASHTAG]#AirTanzania[/HASHTAG] sababu za kuchelewa hazikuwekwa wazi...anyway nasikia kesho itaanza tena safari zake kama kawaida...all the best AirTz
 
Wakuu salamu,sababu ya tofauti ya majira ya huku nilipo na huko nyumbani,basi kuna mambo yamekuwa yakinipita humu jukwaani,ama ninakuwa usingizini au nakuwa busy na kazi iliyonileta.

Nimekuta msgs nyingi na "mentions" nyingi sana za barafu watu wakibishana kuhusu ndege ya ATCL kuharibika.

Kifupi na kwa taarifa rasmi za kiufundi japo nipo mbali na nyumbani ni kuwa,ndege hiyo ya ATCL haijaharibika na sio kweli kuwa eti mainjinia 50 wameshindwa kuitengeneza.Daah!!Jamani huu uongo na masimango kwa shirika letu la ndege inatoka wapi?

Ni kweli hata mimi kuna mambo sikubaliani na JPM,hasa katika masuala ya bunge kuonekana mubashara na uminywaji wa upinzani,lakini simtakii mabaya wala kuizushia serikali yake uwongo.Yoyote unaemuuliza,wewe umepata wapi taarifa hizo?Atakwambia "Mange kasema"....Huyu anayetajwa ni Mhandisi?

Kwa wale waliofuatilia ujio wa ndege hizi wakati zinaletwa Tanzania,watakumbuka kuwa ndege moja ilitangulia kabla ya nyingine,iliyotangulia ni ile iliyokuja na namba za usajili za Canada za C-FHNF ambapo ilipofika Tanzania ikapewa namba ya 5H-TCB.

Hii 5H-TCB ndio ilianza kufanya kazi mbele ya ile ya pili yenye usajili wa 5H-TCD.Kwa hiyo hata kwa masaa ya kukaa hewani,hii iliyotangulia ya 5H-TCB ndiyo yenye masaa mengi hewani kuliko 5H-TCD iliyokuja baadae na kuanza kufanya kazi.

Ndege iliyoegeshwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo madogo ni 5H-TCB,na hii si Tanzania tu,bali dunia nzima.Ndege inapofikisha masaa kadhaa kuwa hewani,let say masaa 12000 hewani,inatakiwa kuwa grounded ili kuweza kubadilishiwa vifaa kadhaa ambavyo masaa yake yanakuwa yamekwisha kwa vyenyewe kutimika.

Hii ni hata kwenye magari,tunashauriwa kutumia matairi ya magari kwa masaa kadhaa,yakipita hayo masaa basi tunapaswa kubadilisha,lakini kiswahili-swahili watu huendesha tu magari mpaka yanawapasukia na kupata ajali.Usafiri wa anga ni tofauti,mambo ya "safety" ni jambo la kwanza na la muhimu.

Kilichotokea kwa ndege moja ya ATCL ni kuwa grounded kwa sababu za kiufundi na kiusalama (safety),ili kufanyiwa "cheki" ya baadhi ya vifaa na kuweza kubadilishwa ili irudi hewani kwa uhakika zaidi.Hii ni kote duniani.

Sisi tunaweza kuona kwa wepesi sababu shirika letu la ATCL lina ndege mbili tu,moja ikienda "hunger" (maintanance area) inakuwa rahisi kujulikana sababu moja tu ndio inabaki ku-operate,lakini jambo hili ni kawaida,leo ukienda Kenya utakuta ndege zilizoegeshwa sbb ya masaa kupita,ukienda KLM,Swiss International,South Africa Airways,Qatar nk.Si jambo la ajabu,kwanini libebwe kama mada?

ATCL ni moja ya kampuni yenye wahandisi wazuri walio wazawa.Na kwa aina ya mkataba wa kampuni ya bombardier,mpaka sasa ATCL imekuwa "attached" na mtaalamu mmoja (Consultant) toka Canada,atakayekuwa kwa muda fulani kama mshauri wa kiufundi moja kwa moja toka kiwandani.

Habari hizo tuzipuuze,si njema kwa mafanikio ya heri ya shirika letu.Tuwatie moyo ATCL,inawasaidia sana watu katika usafiri wa ndani ya nchi.Kwa sasa safari zake za Dodoma,K'njaro,Tabora,Kigoma,Mtwara na Songea zimeokoa muda na kusaidia watu wengi.Safari ya Hahaya-Commoro imekuwa na mafanikio makubwa na yenye faida....Sio kila kitu yule "Binti" akisema kinakuwa na ukweli....

ATCL-The Wings of The Kilimanjaro.......
Imefikisha lini hayo masaa ukiwAhewani hata masaa 20 kwa siku kwa mwezi hayazidi masaa 500 sasa masaa uliyo yataja yanazidi kabisa muda ambao hatakama tangu imenunuliwa ikawa iko hewani unatudanganya ndugu wengine hizo ndio kazi zetu huwezi tudanganya
 
Sijui kama watakuamini kama Mange kasema....
Bora wewe ndio umetoa huo ufafanuzi..........
Mange kasema mimi siwezi kubisha labda Nyani Ngabu

Aaaah Ruta wewe.....

Mange akishasema kuna wa kubisha kweli?

Yaani hapo hakuna wa kubisha....si mimi....si Le Mutuz....si Mwanakijiji....hata Bombardier wenyewe hawawezi kubisha.

Oh halafu nimekumbuka kitu....hivi yule mshikaji 'mtaalamu' wa kupiga picha za ndege aliishia wapi?

:D
 
Mkuu hayo matengenezo kwa wastani huwa yanachukua muda gani?
Kuna uzembe ulifanyika sielewi kwa nini mtoa mada anaficha. Vifaa vikivyomaliza masaa yake vineagizwa ndege ikiwa grounded
Huo ni uzembe wa kiwango cha lami.
Nashangaa mpaka sasa haijatangazwa waliotumbuliwa !
Uzembe ilikuwa sio kugundua muda wa kuisha tu Bali hata kuagiza vifaa husika
Huwezi kuagiza vifaa wakati tayari vinavyotakiwa kubadiriwa Masaa yamekwisha
Vifaa vingi vya ndege ni "plug n play" hivyo uzembe ndio uneifanya ndege moja iwe kwenye loss mode
 
Soma maelezo ya barafu vizuri utapata jibu

Genius
Naomba mwenyewe anijibu maana nimesoma ndiyo maana nikauliza na wewe kama unazo jibu nitashukuru kama unaweza kunijibu kwa niaba yake kwani aulizae ataka kujua
 
Mpaka sasa Precision ndege zake tatu zipo chini sbb ya matengenezo
Fastjet wamebakiza ndege moja tu....Na juzi alisitisha safari ya Mbeya na Mwanza sbb ya matengenezo na watu wakalala hotelini!!
Mkuu bruda ni mambo ya kawaida,kama vile mfungo wa kila mara wa mapadre,nyie mnaita "Retreat"
Kwa mkleri si ajabu
Mkuu barafu uko na taarifa sahihi sana

Genius
 
Wakuu salamu,sababu ya tofauti ya majira ya huku nilipo na huko nyumbani,basi kuna mambo yamekuwa yakinipita humu jukwaani,ama ninakuwa usingizini au nakuwa busy na kazi iliyonileta.

Nimekuta msgs nyingi na "mentions" nyingi sana za barafu watu wakibishana kuhusu ndege ya ATCL kuharibika.

Kifupi na kwa taarifa rasmi za kiufundi japo nipo mbali na nyumbani ni kuwa,ndege hiyo ya ATCL haijaharibika na sio kweli kuwa eti mainjinia 50 wameshindwa kuitengeneza.Daah!!Jamani huu uongo na masimango kwa shirika letu la ndege inatoka wapi?

Ni kweli hata mimi kuna mambo sikubaliani na JPM,hasa katika masuala ya bunge kuonekana mubashara na uminywaji wa upinzani,lakini simtakii mabaya wala kuizushia serikali yake uwongo.Yoyote unaemuuliza,wewe umepata wapi taarifa hizo?Atakwambia "Mange kasema"....Huyu anayetajwa ni Mhandisi?

Kwa wale waliofuatilia ujio wa ndege hizi wakati zinaletwa Tanzania,watakumbuka kuwa ndege moja ilitangulia kabla ya nyingine,iliyotangulia ni ile iliyokuja na namba za usajili za Canada za C-FHNF ambapo ilipofika Tanzania ikapewa namba ya 5H-TCB.

Hii 5H-TCB ndio ilianza kufanya kazi mbele ya ile ya pili yenye usajili wa 5H-TCD.Kwa hiyo hata kwa masaa ya kukaa hewani,hii iliyotangulia ya 5H-TCB ndiyo yenye masaa mengi hewani kuliko 5H-TCD iliyokuja baadae na kuanza kufanya kazi.

Ndege iliyoegeshwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo madogo ni 5H-TCB,na hii si Tanzania tu,bali dunia nzima.Ndege inapofikisha masaa kadhaa kuwa hewani,let say masaa 12000 hewani,inatakiwa kuwa grounded ili kuweza kubadilishiwa vifaa kadhaa ambavyo masaa yake yanakuwa yamekwisha kwa vyenyewe kutimika.

Hii ni hata kwenye magari,tunashauriwa kutumia matairi ya magari kwa masaa kadhaa,yakipita hayo masaa basi tunapaswa kubadilisha,lakini kiswahili-swahili watu huendesha tu magari mpaka yanawapasukia na kupata ajali.Usafiri wa anga ni tofauti,mambo ya "safety" ni jambo la kwanza na la muhimu.

Kilichotokea kwa ndege moja ya ATCL ni kuwa grounded kwa sababu za kiufundi na kiusalama (safety),ili kufanyiwa "cheki" ya baadhi ya vifaa na kuweza kubadilishwa ili irudi hewani kwa uhakika zaidi.Hii ni kote duniani.

Sisi tunaweza kuona kwa wepesi sababu shirika letu la ATCL lina ndege mbili tu,moja ikienda "hunger" (maintanance area) inakuwa rahisi kujulikana sababu moja tu ndio inabaki ku-operate,lakini jambo hili ni kawaida,leo ukienda Kenya utakuta ndege zilizoegeshwa sbb ya masaa kupita,ukienda KLM,Swiss International,South Africa Airways,Qatar nk.Si jambo la ajabu,kwanini libebwe kama mada?

ATCL ni moja ya kampuni yenye wahandisi wazuri walio wazawa.Na kwa aina ya mkataba wa kampuni ya bombardier,mpaka sasa ATCL imekuwa "attached" na mtaalamu mmoja (Consultant) toka Canada,atakayekuwa kwa muda fulani kama mshauri wa kiufundi moja kwa moja toka kiwandani.

Habari hizo tuzipuuze,si njema kwa mafanikio ya heri ya shirika letu.Tuwatie moyo ATCL,inawasaidia sana watu katika usafiri wa ndani ya nchi.Kwa sasa safari zake za Dodoma,K'njaro,Tabora,Kigoma,Mtwara na Songea zimeokoa muda na kusaidia watu wengi.Safari ya Hahaya-Commoro imekuwa na mafanikio makubwa na yenye faida....Sio kila kitu yule "Binti" akisema kinakuwa na ukweli....

ATCL-The Wings of The Kilimanjaro.......
Ahsante sana mkuu Barafu kwa clarification hii nzuri.Wapo watu humu JF ambao uzalendo hawana kabisa. Sana sana wanatanguliza maswala ya vyama.Jamani nchi hii ni yetu sote, kwa hiyo ni vema tukakosoa kwa ajili ya kujenga, sio kubomoa.Uchaguzi umeshakwisha,ni vema sasa tukashirikiana katika ujenzi wa taifa letu.
 
Kuna uzembe ulifanyika sielewi kwa nini mtoa mada anaficha. Vifaa vikivyomaliza masaa yake vineagizwa ndege ikiwa grounded
Huo ni uzembe wa kiwango cha lami.
Nashangaa mpaka sasa haijatangazwa waliotumbuliwa !
Uzembe ilikuwa sio kugundua muda wa kuisha tu Bali hata kuagiza vifaa husika
Huwezi kuagiza vifaa wakati tayari vinavyotakiwa kubadiriwa Masaa yamekwisha
Vifaa vingi vya ndege ni "plug n play" hivyo uzembe ndio uneifanya ndege moja iwe kwenye loss mode
Hata mm nashangaa kwann mtu huyo hajatumbuliwa ,time will tell

Genius
 
!
!
Swali la maana hapa ni je matengemezo kama hayo hucheka muda gani? Na hii panga boi imepaki kwa muda gani? Hii nchi yetu ya vyerehani vitano kuwa [HASHTAG]#kiwanda[/HASHTAG] bwana sio ya kuwa amini sana
 
Back
Top Bottom