Lini Kitabu cha Ufnuo kiliandikwa
Wana theology wanasema kwamba kitabu hiki cha ufunuo kiliandikwa mwaka 65AD. Kwamba kiliandikwa kipindi Nero akiwa anatawala.
Kipindi hicho Paul na Peter waliuawa. Na wakristo walikuwa wakisakwa na kuuawa.
Mwandishi wa kitabu hicho hajulikani. Lakini ukikisoma mwanzoni yule aliyeona maono alijiita Yohana alikuwa katika kisiwa cha patimo. Wengine wanasema kwamba aliyeandika kitabu hicho ni Yohana mwanafunzi wa Yesu ambaye alifungwa katika kisiwa cha Patimo baada ya kushindikana kuuawa. Kwamba alitupwa kwenye pipa lililochemka mafuta lakini hakuweza kufa. Lakini Yohana alikuwa ni mtu ambaye hakusoma kwamba isingewezekana kuandika kitabu hicho ambacho ndani yake kuna Nyaraka ambazo zimeandikwa kwa ustadi katika makani saba
(1) Efeso (Ufunuo 2: 1-7) — kanisa lililoacha upendo wake wa kwanza (2: 4).
(2) Smurna (Ufunuo 2: 8-11) — kanisa ambalo litapitia mateso (2:10)
(3) Pergamumu (Ufunuo 2: 12-17) — kanisa ambalo lilihitaji kutubu (2:16).
(4) Thuatira (Ufunuo 2: 18-29) — kanisa lililokuwa na nabii wa uongo (2:20).
(5) Sarde (Ufunuo 3: 1-6) — kanisa lililokuwa limelala (3: 2).
(6) Filadelfia (Ufunuo 3: 7-13) — kanisa ambalo lilikuwa la uvumilivu (3:10).
(7) Laodikea (Ufunuo 3: 14-22) — kanisa lenye imani si baridi wala si moto (3:16).
Kwa mantiki hiyo na mambo mengine mwandishi wa kitabu hicho cha ufunuo sio Yohana mwanafunzi wa Yesu. Na ikumbukwe kuwa Yohana lili kuwa ni jina common wakati ule katika jamii ile
Upande mwingine mwandishi wa Ijili ya Yohana na Mwamdishi wa Ufunuo ni waandishi wawili tofauti. Maana namna ya uandishi ni tofauti. Mwandishi wa Injili ya Yohana alikuwa professional write na alikuwa anaijua lugha, lakini mwandishi wa kitabu cha ufunuo alikuwa haijui lugha, maana kwenye original document ya ufunuo kulikuwa na mistakes nyingi za grammar. Kwa hiyo mwandishi wa kitabu cha ufunuo siyo yule aliyeandika kitabu cha Injili ya Yohana.
Kwa maana hiyo, kutokana na kuchanganya changa kwa taarifa zilizomo kwenye kitabu cha ufunuo kwamba style ya uandishi, kwa sehemu ili copy kitabu cha kutoka, kwa sehemu ili copy kitabu cha Daniel, kwa sehemu ili copy Nyaraka za mitume na sehemu zingine kwenye injili na agano la kale. Kwahiyo sasa hakuwa mwandishi mmoja aliyeandika kitabu hiki cha ufunuo. Ni kwamba waandishi kadha wa kadha zilikusanywa documents zao na kuwekwa pamoja na mtu ambaye alikuwa makini sana.