Ukweli kUhusu Mgogoro wa Seif na Hamad Rashid CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kUhusu Mgogoro wa Seif na Hamad Rashid CUF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ASKOFU MSAIDIZI, Nov 27, 2011.

 1. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia makoa mkuu ya CUF nikagundua kuwa hali ni tete kwani kuna makundi Moja ni la Hamadi Rashid na Jingine ni la Maalim Seif Na kwamba makosa aliyofanya Seifu yamewagusa wengi na hapana Shaka kwamba ameanza kuyarekebisha!!!

  Moja ya Mambo ambayo yamekuwa kero kubwa ni suala la pesa ambapo Mgao wa pesa za operations za Makao makuu zilikuwa hazipo Wakati kule Pemba wanatanua kwa kutumia fedha za serikali.

  Julius Mtatilo aliwahi kuongea na gazeti la Sema Usikike akaelezea ukata wa fedha ambapo analazimika kutumia fedha zake Mwenyewe kwa ajili ya shughuri za Chama !!!

  Mtatilo aliwahi kulalamika kwamba Ruzuku imechelewa lakini ukweli ni kwamba hata Ruzuku hiyo ilipotolewa ilikuwa haipelekwi Wilayani kama sheria inavyotaka!!

  Mtu wa karibu na ofisi ya Uhasibu anasema Juzi tu baada ya Hamadi Rashidi kuelezea nia ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu ndipo Maalimu Seif akaamuru pesa zipelekwe kwenye Wilaya 1oo na kila Wilaya imepelekewa 300,000/= katika awamu ya kwanza na Fungu lililotengwa ni Tshs 180m kwa miezi 6.

  Baadhi ya maofisa wa makao Makuu CUF wanalalamika kuwa ni kwa nini fedha zote hizo zilikuwa hazipelekwi mpaka watu walalamike??

  Mjumbe Mmoja wa Baraza kuu kutoka Pemba anasema Maalimu Seif anatafuta njia za kumufukuza Hamad Rashid na jana aliitisha kikao cha siri Pemba na kufanya njama za kuandaa kashifa za Hamad Rashid lakini Watu waliokinyume na sef Pemba wakafichua uovu huo!!!

  Mpaka sasa Cuf kimekuwa chama cha kuwindana!!!
  Maalimu hataki Uchaguzi ufanyike na sasa anataka atoe urithi jambo ambalo halikubaliki!!!
   
 2. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2]Maalim Seif Anaaminika?
  MAALIMU SEIF ANAUA CUF BARA!!!!!
  Thursday, 18 November 2010 19:53 newsroom [/h]  Na Esther Mvungi,Dodoma
  MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, amesema haina maana kwa chama cha siasa kupinga kila jambo. Amesema CUF kwa upande wa Tanzania Bara kinafanya kazi ya upinzani kwa ustaarabu na kuongeza: ├ČTutapinga kwa hoja na si kwa malumbano. Seif alisema hayo jana baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika sherehe zilizofanyika Ikulu Ndogo ya Chamwino. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hoja inayotolewa na baadhi ya wananchi na vyama vya siasa kuwa, CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Haina maana kama Zanzibar kuna maeleweno na upande wa pili wa Muungano iwe tofauti, tutafanya kazi zetu kistaarabu,î alisema Seif.
  Alisema lengo la wote ni kuleta amani, hivyo CUF inataka yaliyotokea Zanzibar yahamie Bara.Seif alisema ni kweli kwa upande wa Zanzibar CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya serikali. CHADEMA imevitenga vyama vingine vya upinzani vya CUF, NCCR-Mageuzi na TLP katika kuunda kambi ya upinzani.Utengano kati ya vyama hivyo umekuwa ukijionyesha wazi bungeni, ambapo katika uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la SADC-PF uliofanyika Jumanne wiki hii, wabunge wa CHADEMA walimdhihaki mgombea wa CUF.

  Baada ya Injinia Mohammed Habib Mnyaa wa CUF kutangazwa mshindi katika kundi la vyama vya upinzani, wabunge wa CHADEMA walipiga kofi wakisema CCM, CCM.
   
 3. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtu mbinafsi kama Seif. Ni hatari kushinda wasaliti. Yeye siku zote ametanguliza maslahi yake. Alimsaliti Mzee Aboud Jumbe mwaka 1984 katika kile kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa ya siasa Zanzibar. Alipokosa kuchaguliwa kugombea uraisi Zanzibar mwaka 1985 alifanya kampeni za chini chini dhidi ya Abdul Wakili. Marehemu Wakili akampa uwaziri kiongozi. Lakini kufikia Januari 1988 kumchimba kwake Wakili kulisababisha afukuzwe nafasi hiyo na CCM. Baada ya hapo akawekwa ndani aliyemtoa ndani ni Lamwai kupitia Mahakama ya Rufaa. Lakini ni Mahakama anayoipinga kwamba inaingilia mambo ya Zanzibar.

  Katika mazungumzo ya muafaka ya kwanza alipigania kurudishiwa mafao yake ya Uwaziri Kiongozi. Je, imewahi kutokea mtu aliyefukuzwa kazi akapewa mafao? Hiyo ni kwa Seifu. Ni lazima watu tumpinge kwa nguvu zote na kuanika unafiki wake bila woga wowote ule.
   
 4. S

  Salimhamad Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Askofu jina limekusibu. Munaweza kumpiga vita huko bara lakini Zanzibar katu hamutafanikiwa. Sisi tuko mbioni kuipa Zanzibar mamlaka yake kamili na kazi hii imekuwa ikisimamiwa na Maalim Seif kwa miaka mingi na insha-Allah kwa hili tutafanikiwa. Ya Jumbe na Seif hamuwezi kuyaelewa nyinyi. Kwa taarifa yako hata watoto na vijukuu wa Jumbe hivi sasa wanamtambua nani Maalim Seif. Kama umeangalia juzi wasanii Zanzibar wa Zanzibar 100% wamemtunikia nishani ya ushujaa na aliyemkabidhi ni Kheri Yussuf Jumbe! Upo hapo? Nyinyi chukuweni Tanganyika yenu na faidini kwa utajiri wenu na sisi tuwacheni na umasikini wetu na mambo yetu tupo tayari kwa hilo. Karume hakuja kuomba kwa Nyerere juu ya Muungano huu, ni Nyerere kwa malengo yake na hakuweza kumchezea Karume mpaka alipo amua kumuuwa.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,448
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Wamechapiana hao awana jipya uji wazanz eeehhhh makosa yote wanasamehe kuchapiana loh
   
 6. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Khaaa ! ?
   
Loading...