hyassin92
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 582
- 635
TAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA
Biolojia inasema kuwa baada ya tendo la ndoa, mbengu za kiume zinazoingia kwa mwanamke hufikia karibu milioni 300 na zote huanza kuogelea kwenda kukutana na ovum.
Kati ya mbegu hizo milioni 300, ni mbegu 500 tu zinazoweza kufikia sehemu husika (kwenye ovum). Mbegu nyingine huchoka mapema na kufa njiani. Kati ya mbegu 500 zinazofanikiwa kufika kwenye yai basi mbegu moja tuu ndiyo hufanikiwa kushinda na kutengeneza kiumbe. Mbegu hiyo ni wewe unayesoma ujumbe huu. Kama usingeshinda mbio zile, na kuwashinda wenzio milioni 300 usingekuwepo duniani leo.
Umewahi kufikiri juu ya hili? Biolojia inatueleza kwamba ulikimbia mbio na kuwashinda wenzio milioni 300 bila macho, bila miguu, bila mikono.
Ulikimbia mbio bila ya elimu yako na ukashinda. Ulikimbia bila cheti na ukashinda. Ulikimbilia bila msaada wa mtu mwingine yeyote na ukashinda. Je nini kinakufanya ufikiri kushindwa kwenye maisha hadi kukata tamaa?
Kwa sasa una macho, una miguu, una maarifa, una ujuzi wa neno la Mungu kwanini ushindwe? Kwanini ukate tamaa? Muombe Mungu, kuwa na maono, kisha weka mipango thabiti, utafanikiwa. Usikate tamaa hata siku moja kwani tayari ulishakuwa mshindi kwenye mashindano ya watu zaidi ya millioni 300, kwanini ushindwe leo?
Changamoto ni sehemu ya maisha yetu, lakini kamwe zisikukatishe tamaa. Kuwepo kwako duniani ni mpango kamili wa Mungu. Hukuja duniani kwa bahati mbaya, lipo kusudi la uwepo wako. Hakikisha unalitambua kusudi hilo na kulitimiza. Haijalishi unapitia kwenye wakati gani kwa sasa.
Amini kwamba wewe ulizaliwa kwa kuwa ulishinda wenzako weengi mno.!