A3M
Member
- Jul 23, 2019
- 84
- 178
Habari za humu wa wadau wa JF,
Nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa neema na baraka nyingi ambazo ametupa na kikubwa zaidi ni afya njema na maarifa mazuri aliyoturuzuku. Lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Great thinkers wote wa JF ambao walitoa mawazo yao juu ya Mpango wangu wa kuzamia Nchini Marekani mara baada ya kupata Visa ya nchi hiyo.
Nafahamu wapo watu ambao walitamani sana kujua nini kilichojiri baada ya mimi kufika USA na kilichoendelea baada ya kuzamia huku Ughaibuni. Niwakumbushe tu kidogo kuwa nilisafiri tarehe 15 August mwaka huu 2019 kwaajili ya kuhudhuria mkutano ambao ulifanyika na nilihudhuria Nchini Marekani katika mji wa Washington DC ambapo ilinichukua siku 3 kukamilisha kile nilichotumwa na ofisi yangu kukikamilisha.
Nakumbuka watu wengi wa JF walinipa ushauri baada ya kumaliza mkutano nirudi Bongo kwa sababu sina pa kuanzia Marekani ila kwangu mimi hiyo haikuwa sababu ya kunizuia nisizamie Marekani.Kiukweli Marekani ni kuzuri mno japokuwa sijawahi kwenda nchi yeyote hiyo ndio Mara yangu ya kwanza tangu nizaliwe ila sidhani kama kuna nchi nzuri kuliko Marekani hapa duniani,Ni kuzuri nashindwa hata kuelezea kwa kweli.
Mara baada ya kutuma ile Post hapa jukwaani kuna jamaa alinitafuta Private kabla ya kuruka akanipa mchongo akaniambia hapo Marekani hapafai akasema atanipa njia niende Canada ila nikifika nijiripue kama mkimbizi wa Kisomali ndivyo Wazanzibari wengi hufanya hivyo na alinitumia Makaratasi ya Somalia niyasome ili niijue vizuri Somalia kuna maeneo Somalia wanaongea kiswahili.
Nilipomtumia picha yangu akasema nafanana sana na Msomali hivyo nikifika Marekani nimtafute ataniunganisha na mtu nitakayemlipa anivushe upande wa pili yaani Nchini CANADA. Kwa kweli nilikuwa naogopa sana na niliogopa isije ikawa anataka kunipoteza ila nilikuwa na moyo wa ujasiri na nilishachunguza kuwa watu wengi wanatoka Marekani na kuingia Canada kupitia Illegal borders.hivyo nilijipa moyo na kusema ntaweza.
Hivyo nilipomaliza mkutano nikawasiliana na jamaa mvushaji akasema niende New York atakuja kunipokea Airport,kwasababu nilikuwa na Pocket money ya kutosha nilijiamini sana.Baada ya kufika akanipeleka hoteli fulani akasema atakuja kesho asubuhi, Ilipofika majira ya saa 4 asubuhi akafika akiwa yeye na mwenzake ambae alikuwa ni Mmexico na huyo alienipokea alikuwa ni Mzanzibari.
Kwa hiyo tukapanda bus mpaka sehemu ambapo tulishuka na tukachukua Taxi tukawa tunaenda nikaona msitu tu nilipouliza akaniambia kuwa huku sasa ndio tunaelekea CANADA nikashangaa sana tuliposimama sehemu tukashuka na kukutana na watu watano na wale wawili wakawa saba wakaniambia niwape hela tuliyokubaliana yaani Dollar 3000 ikabidi niwape then tukaendelea na safari nikiwa nahofia kuwa nisije nikawa naenda kuchinjwa na kutolewa viungo vya mwili wangu maana hakuna ninaemjua pale na hata huyo Connector wangu nilikuwa simjui ila ilikuwa balaa la hofu limetanda naona sifiki.
Hatimaye nilifika sehemu nikaoneshwa bendera ya Canada na kuambiwa nenda pale na waeleze kuwa wewe ni mkimbizi kutoka Somalia utasaidiwa.Nikaenda na nikavuka mpaka nilipofika nikapigwa pingu palepale kwa kosa la kuvuka kinyume na utaratibu.
Itaendelea...
Nitawaeleza siku nyingine baada ya Pale ila kwasasa nipo Canada.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pia, soma:
www.jamiiforums.com

Habari za leo Wana JF,Natumai mko poa sana na wale ambao hawako vizuri kwa namna moja au nyingine namuomba mwenyezimungu awaondoe katika hali hiyo na awapeleke katika hali nzuri zaidi ili waweze kuendelea na mapambano ya maisha ya kila siku.Nichukue nafasi hii kipekee kabisa kuweza kumshukuru mwenyezimungu,Mwenyezimungu ambae anatupenda sana sisi Wanaadamu na ametuumba umbile zuri kuliko kiumbe mwingine yeyote yule na ametufanya kuwa na akili ya kufikiria na kuamua na kuchagua kile ambacho tunakitaka hivyo hatuna budi kumshukuru.Ntakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawashukuru wana JF ambao wamesoma na kucoment hadithi yangu ya ukweli na sio ya kutunga hivyo nawashukuru sana.
Inaendelea...........
Baada ya kuvuka ile border ya USA na Canada nilikutana na polisi na bila ya kunihoji walinipiga Pingu jambo ambalo lilinishitua sana na moyo wangu ukaanza kwenda mbio nikaona sasa nimejiingiza kwenye matatizo maana sikuambiwa kuwa ntapigwa Pingu niliambiwa ntasaidiwa tu.Nikasachiwa mwili mzima then nikapelekwa kwenye kituo cha polisi,Nilipofika mule ndani nikafunguliwa pingu kisha kikafunguliwa chumba kidogo sana ambacho kilikuwa na Choo chake nikaingizwa ndani kisha nikaambiwa na Polisi wawili wa CANADA nivue nguo zangu zote hivyo kubaki uchi kama nilivyozaliwa kisha wakanifungia mlango wakaondoka.Walipoondoka nikaanza kukiangalia kile chumba huku nikiwa na wasiwasi mkubwa na mawazo nikaona heater na Camera nne nikawasha heater maana kulikuwa na baridi kiukweli nilikuwa katika wakati mgumu sana nilikumbuka nyumbani hasa mama yangu,Watoto wangu,mke wangu na ndugu zangu nikaanza kutokwa na machozi nikikumbuka nilivyosoma kwa shida na kupata kazi na nikawa namudu maisha yangu na kusaidia ndugu zangu nikajiona katika watu wapumbavu mimi ni mpumbavu kwelikweli.Chumba hakikuwa hata na kigodoro hivyo sikuweza kulala Usiku mzima.
Ilipofika asubuhi majira ya saa tatu mlango ukafunguliwa na Polisi wawili wakafungua mlango kisha wakaingia ndani ya chumba changu wakanipa nguo zangu na kisha wakaniambia niwafuate.Tukaingia chumba kingine mulemule ndani nikakutana na Afisa mwengine wa Polisi akaniuliza kwa ukali "Why did you cross the border Illegally?" Nikamwambia kuwa mimi ni mkimbizi kutoka Somalia nimeletwa na Agent Marekani na amenipokea mtu ambae amenileta mpaka hapa akaniambia nivuke ntasaidiwa hivyo wakaniuliza tangu naianza hii Safari nimetokea wapi na nimepita wapi mpaka nimefika hapa,Waliniuliza maswali mengi sana ambayo sitaweza kuyaandika yote humu Pia waliniuliza kwanini nisiombe Asylum USA nikawaambia kuwa nimeambiwa USA hawapokei wakimbizi na uzuri nilishapangwa cha kusema hivyo nilikuwa naigiza vilevile nilivyofundishwa kujibu na wakati wananiuliza walikuwa wanaandika kwenye computer walipomaliza tu wakatoa Karatasi ambayo ilikuwa inaonesha maswali niliyoulizwa na nilichojibu kisha nikaambiwa nitie Signature yangu.
Baada ya hapo nikaambiwa niwafuate Polisi wale wawili walionitoa mule chumbani kisha tukatoka nje nikaambiwa nipande gari hivyo nikaingia kwenye gari ikiwa na Polisi wengine wapya watatu .Gari ikaanza mwendo ambapo nakumbuka ilituchukua masaa matatu mpaka Kufika mji mkubwa kidogo nakumbuka unaitwa Québec ambapo mji huo wanazungumza Sana Lugha ya Kifaransa.Nilipofika Quebec nikapelekwa sehemu kwenye mjengo mkubwa Sana ulivyo kama Hotel nikakabidhiwa kwa Ofisa mmoja mwanamke na akapewa karatasi zangu huku akiaambiwa kwa Kifaransa kisha wakaniaga wale walionileta wakaniambia wananitakia kila la kheri
Mwanamke huyo akaniuliza Je nkilichoandikwa kwenye zile karatasi ni kweli au uongo nikajibu ni kweli,Akatoka akaniletea kitambulisho kinachoonesha kuwa mimi Mkimbizi kutoka Somalia kisha ikapigwa simu kwa Security wakanipeleka sehemu humohumo ndani nikapewa Lotions,Sabuni za kuogea,Shuka na Blanket kisha nikapelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa na watu wawili tu ila kilikuwa ni chumba kidogo ambacho kilikuwa na vitanda vya Double decker viwili yaani kitanda kimoja mmoja analala juu na mwingine chini kwahiyo chumba kimoja hulala watu wanne japo nilikuta watu wawili tu ila ikiwa mtu na mkewe wanapewa chumba kimoja peke yao na kitanda kikubwa.Nilikaa pale mwezi mmoja huku nikapata breakfast na lunch na dinner kwenye Kantini kubwa iliyokuwa na watu wengi Sana ikiwa wengi wao ni Waarabu wa Syria,Yemen na Afghanistan pia kulikuwa na Wasomali wengi na Watanzania ambao wengi walikuwa Wazanzibari na Kutoka Dar ilikuwa nipo peke yangu ila hawakunibagua.
Niliiishi pale kwa miezi miwili huku nikiutembea mji maana tulipewa ticket za bure kwa mwezi mzima na ikiisha muda unapewa nyingine na tulikuwa tunalipwa kwa mwezi pesa kidogo bila ya kufanya kazi.Kwa kweli nilipata marafiki wengi wa Kizanzibar pale kambini na kupeana hope kuwa tutashinda kesi na kupata Papers za kuishi na kukubalika kisheria.Na tulipeana Technic nyingi za kushinda case maana kuna Wazanzibari walijiripua kuwa ni Wasomali na walipoulizwa kwenye Interview ya kesi zao walisema kuwa Walitoa rushwa ili wapate Passport za Tanzania na wengine walisema wao ni mashoga kwahiyo jamii zao zimewatenga na wanataka kuuliwa maana jambo hilo halikubaliki kisheria kwetu na wengine walisema wao ni Wanasiasa hivyo Serikali inawaua na kuwapoteza na wengine walisema kuwa ni Waandishi wa habari na vyeti feki wametengeneza vya Uandishi wa habari kwa kweli Wazanzibari uzamiaji upo kwenye Damu.
Baada ya mwezi mmoja niliitwa kwenye Interview yangu ya kwanza ya kuhojiwa kilichonikimbiza Somalia na nikienda nikahojiwa kwa muda wa masaa 6 na maswali niliyoulizwa ni mengi sana..........
ITAENDELEA................
Ntataja maswali yote niliyoulizwa kwasababu dhamira yangu sio kuwafundisha watu kuzamia ila wayajue maisha halisi ya kuzamia ili mtu akiamua kuja ajue nini kitakachotokea hivyo Kujiandaa kisaikolojia mapema
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari za humu wadau,
Natumai kuwa mko poa na wenye matatizo nawaombea kwa Mungu awaondolee matatizo yao ili waweze kuendelea na mapambano ya kila siku ya kuboresha maisha yao.
Nichukue nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza wale wote waliotumia muda wao kusoma au kufuatilia na kucomment kile nilichokiandika kuhusu story yangu ya kweli ya kuzamia nchini Canada.
Wadau sina haja ya kuwadanganya watu, lengo langu ni kuwaambia watu wanaofikiria kuzamia nchi zilizoendelea (ughaibuni) kwa ajili ya kujipatia maendeleo, na niwaahidi leo kuwa ntawaeleza kila kitu kuhusu maisha ya huku Canada, yaani changamoto zake na Faida zake.
Inaendelea...
Nilifanikiwa kwenda kwenye Interview ni mwendo wa saa 2 kutoka hapa ninapoishi mpaka kwenye Immigration Department Office. Hivyo niliamka alfajiri na mapema nikajiandaa kwenda kwenye hiyo Interview kwakuwa baridi ni kali nilivaa jacket zito na pullover ndani na gloves za baridi na buti za baridi na kofia ya baridi, hivyo niliweza kuihimili baridi.
Nilienda kituo cha basi nikapanda basi then nikashuka nikapanda treni then nikabadilisha treni mpaka nilipofika ilikuwa ni saa moja na nusu na uzuri wa nchi za wenzetu kabla ya kutoka unaangalia katika simu yako unaandika ulipo na unapokwenda inakueleza basi litapita muda fulani mpaka muda fulani utafika mahala fulani na utasubiri muda fulani hapo treni itapita.
Cha ajabu unakuta muda ni uleule, ukichelewa tu imekula kwako kiukweli. Huku muda unathaminiwa kuliko kitu chochote.
Nilipofika kwenye hilo jengo nilikuta Security wa kawaida tu ambao hawakuwa wazungu hivyo walinisachi kisha wakaniruhusu niingie na wakanambia niende kwenye counter nikadaiwa kitambulisho nikawapa kisha wakaichukua wakanipa namba then wakaniambia niende ninyooshe mbele kidogo nikaenda na nikakutana na kama hall kubwa hivi ambapo nilikuta watu wengi sana, Waafrika na Waarabu wengi sana.
Nikawa nasubiri kusikiliza namba yangu ikiitwa na nilisubiri masaa matatu mpaka kuitwa, hivyo niliingia ndani nikakutana na Mcanada mmoja mwanaume akiwa na computer yake na Mwafrica mmoja mwanamke. Yule Mwafrica akajitambulisha Kiswahili akasema yeye ni Mkenya na atakuwa Mkalimani kwaajili ya kesi yangu hivyo nikaulizwa swali "Je, unataka kuwa interviewed kwa lugha gani?" Nikajibu KISWAHILI kwasababu tayari Mkalimani yupo pale kwanini nijifanye mjuaji sana.
Tukaanza Interview ambapo waliniuliza maswali yafuatayo:
1. Je, huyu ni wewe? (Walinipa karatasi inayoonesha Visa yangu ya Marekani). Nilistuka sana kwasababu sikuambiwa kabla. Hivyo nilisema ndiyo.
2. Je, wewe ni raia wa Tanzania? (Nikajibu siyo)
3. Ulipataje Passport ya Tanzania (Nikajibu kuwa nilitengenezewa safari na agent hivyo sijui yeye aliipataje). Kumbukeni wadau Mzungu anaandika kwenye computer yake kila ninachokujibu.
4. Je, ulimlipa nini agent? (Nilimpa dhahabu)
5. Ulipata wapi hizo dhahabu (Nilijibu ni urithi kutoka kwa wazazi wangu)
6. Wazazi wako wako wapi (Nilijibu baba alishakufa ila mama yupo)
7. Mama yako yuko wapi? Nikasema Tanzania.
8. Una mke na watoto? (Nikasema Nina mke na watoto watatu)
9.Mkeo ni Mtanzania? (Nikajibu ndiyo).
Kwa kweli maswali ni mengi mno maana kikubwa walitaka kuthibitisha kuwa mi ni Msomali kweli au nadanganya. Hivyo maswali ni mengi mno.
Uzuri nilikuwa nishapangwa vizuri eneo la Somalia nililotoka na tamaduni za huko. Maswali mengine hata sikufundishwa katika zile karatasi alizonitumia jamaa kwahiyo nilitumia akili yangu ya ziada.
Mwisho waliniuliza, je tukikurudisha Somalia itakuwaje nikawaambia nitaenda kuuawa kwasababu Al Shabab waliwahi kunitaka nijiunge nao nikakataa wakanipiga sana.
Waliniuliza pia, je tukikurudisha Tanzania? Nikajibu "Ntafungwa kwa kosa la kumiliki nyaraka nisiyostahili kumiliki"
Interview ilikuwa ngumu sana yaani mpaka sasa siamini kuwa nitabakishwa au nitarudishwa.
Mbaya zaidi nimejipiga under age kuwa nina miaka 18 na wameamini. Hivyo elimu yangu sijui itakuaje yaani niko shaghala bagala sielewi matokeo yatakuaje?
Baada ya kumaliza Interview karatasi mbili zikatoka kwenye printer nikatia saini zote kisha nakala moja nikachukua mimi moja ikabakiwa. Nikitoka nikiwa na mawazo sana.
Siku ya pili nikawa nimekaa na rafiki zangu tunabadilisha na mawazo nikawaelezea balaa lililonikuta na maswali mazito sana wakaniambia kesi si lolote si chochote ni kutimiza wajibu tu ila hawawezi kukurudisha Bongo maana hawa nchi yao ni nchi ya pili kwa ukubwa duniani na haina nguvu kazi hivyo wanahitaji nguvu kazi. Kwahiyo tulipeana moyo sana.
Baada ya week 1 nililetewa post inayoeleza kuwa ninaruhusiwa kutafuta kazi nikipata kazi ntapewa kibali cha kazi. Kazi ni nyingi mno Canada zinahitaji watu hivyo niliingia kwenye mtandao nikaangalia kazi ninayoitaka kisha nikaomba kazi ya Hoteli KFC. Baada ya siku 2 nikaitwa kwenye Interview nikaenda nikafaulu interview hivyo nikapewa mkataba nikajaza vizuri kisha nikaambiwa nizipeleke Government zikapigwe muhuri.
Hivi tunavyoongea muda huu mimi nafanya kazi huku nikisubiri majibu ya Interview yangu ambapo sijui yatatoka lini? Ila najua ntapewa Negative tu.
Mshahara wangu ni mara 5 ya mshahara niliyokuwa naupata nyumbani. Na bado nipo kambini hivyo sina mzigo wa kodi ila wenzangu washaletewa barua walipe bili ya maji na umeme na malazi, hivyo wamesema bora kutafuta nyumba ya kupanga na ku-share.
Kikubwa ambacho nataka niwaambie ndugu zangu maisha ya nyumbani hayana guarantee wala warranty ila kwa mtu aliyesoma na akafanikiwa kupata kazi ni bora akatulia nyumbani maana kuwa karibu na familia ni bora zaidi.
Tazama leo napata pesa ila nipo mbali na mke wangu na wanangu, sasa haya ni maisha gani?
Na huku sio lele mama na ukifika utakuwa tajiri, hapana! Sivyo hivyo wanavyofikiria wengi. huku ni kazi kazi tu ila malipo mazuri sana. Na utofauti wa nyumbani na huku. Huku elimu bure tena elimu bora na matibabu bora. Usafiri wa umma ni mzuri sana hakuna foleni. Kwa kweli jamaa wamejipanga.
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu Njoo huku ikiwa unaona huna elimu na huna mtaji na maisha yako mabovu mno. Yaani hata chakula huna na huoni mwanga nyumbani.
Nimeifupisha stori kwasababu niko busy sana na kazi.
Nawatakia jioni njema.
Nakaribisha maswali kwa anayetaka kujua kuhusu maisha ya kuzamia huku.
Asanteni sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pia, soma:
Nimefatilia post za A3M nimegundua jamaa ni muongo na ana kitu anakilenga humu
Jm