Ukweli kuhusu maisha ya sanaa na wasanii

Likwanda

Likwanda

JF-Expert Member
3,888
1,250
Mtoa Mada umeongea point sana, Tumuangalie Michael Jackson ndiye mwanamuziki aliyrefanya matamasha makubwa zaidi ya kimuziki tena sold out za mapema kabisa ikiwa anatumia nyimbo zake za zamani tu. Ikumbukwe kua nyimbo mpya aliyotoa Kama bonus track ni rock the world tu. Pia Kuna Marehemu Milium Makeba yeye ulikua anaalikwa kwenye majukwaa makubwa bila kua na nyimbo mpya ila ulikua anakonga nyoyo za mashabiki kwa nyimbo zake za ujana kama Patapata, Hapo zamani na Maraika, sijajua Hawa wakwetu wanapigania vikumbo vya nini wakati ilikua wako wasubiri kupewa collaboration na wasanii wasasa ili kuonesha ukubwa wao.

Hivi hawajui kua hata Boby Brown bado anapiga shows je yeye ametoa nyimbo Gani mpya!?
 
Mirhea

Mirhea

JF-Expert Member
810
1,000
Big up. Hizi ndio sredi za kiume sasa. Sio zile za kina nani mtanashati na the Co, hata Wema akijamba anakuja mbio mbio Jf kumuanzishia uzi.
 
mzaramo

mzaramo

JF-Expert Member
6,348
2,000
Hii kitu ya maana sana wakongwe waache uoga bado wana mashabiki wengi sana tena sana.

Mwaka ule Sugu alipiga show kijitonyama na Vinega ilikuwa bonge ya show wakina Soggy,babu,Nature,Mkoloni walipanda jukwaani na kila shabiki aliimba nao nyimbo za zamani.

Wasifikilie kutoa ngoma mpya wajikusanye wafanye matamasha wapige hata tour nchi nzima.

Watu kama Majani na Master Jay wanaweza kusimamia hii kitu na kikawa kitu kikubwa tu
 
olele

olele

JF-Expert Member
1,004
2,000
Umeandika vizuri mkuu,uchambuzi murua kabisa.

Ila kingine kinachowafanya hawa wakongwe wasisikike tena kama zamani ni sasa hivi soko lipo updated,watoto wengi sana mtaani kila unapopita utasikia pua tu zikibanwa huku wakicheza kwa kuzunguka zunguka chini trousers zikitaka kuwashuka sasa hawa ukiwaambia habari za Hili Game,Ana miaka chini ya 18 by Sugu hata hawakuelewi maana wakati zinapigwa wengine walikuwa bado hawajazaliwa.

Enzi hizo ilikuwa ikitangazwa Nature anatoa ngoma mpya basi siku hiyo vijana tupo pembeni ya radio kama ni chakula au maji haviliki mpaka umeisikiliza kwanza,Sasa hivi wengi wetu umri umesogea majukumu mengi muziki huwa nasikiliza siku moja moja sana so ktk mazingira kama haya inakuwa ngumu sana hawa jamaa kurudi tena,pia nilichokigundua kadiri mileage zinavyosoma ndo mtu unavyozidi kuhama kutoka kupenda hiki hadi kupenda kile.miaka 18 nyuma haikuwa rahisi unikute nasikiliza taarifa ya habari au malumbano ya hoja mara nyingi ilikuwa mziki so naamini wengi kama nilivyo mimi akili zimekua ndo maana wakongwe tunawauwa njaa.

Pia hata wakirudi hiki kizazi cha sasa hakitaki kusikiliza harakati chenyewe kinataka mahaba tu sasa imagine mkongwe kama Nature aingie studio akabane pua anaona ujinga bora akafanya mambo mengine tu.

Sent using Redmi Note 5
Mi nakumbuka nilisikia kwa jirani mtangazaji wa radio one anasema "ifuatayi ni nyimbo mpya ya Prof J Bongo Dar es salaam" tukasogea na kutega sikio kwenye fensi mi na Dada yangu kwa ajili ya kusikiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
4,970
2,000
ulichokisema ni sahihi sana huwa najiuliza mfano anatokea MB dog kwa stage aisee sipati picha zile nyimbo (ratifa, naona raha, e.t.c) kwa kweli zinanikumbusha mambo mengi ya miaka hiyo(2007+ nilivyokuwa natoroka manyanyaso ya ndugu niliekuwa naishi nae, arafu ndani ya basi nyimbo hizo zilivyokuwa zinani burudisha) kiukweli huwa nakumbuka mbali sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukhuty

ukhuty

JF-Expert Member
16,880
2,000
Daima dumu huwa naamini maisha ya sanaa ya muziki hayana tofauti na kukidunda kitenesi kwenye sakafu automatically kitaenda juu na kisha kugonga ceiling board na kurudi chini huku kikipungua kasi yake ya kwenda juu na hatimae hutulia tuli sakafuni. Ndio yalivyo hata maisha ya muziki kuna kipindi unafika kwenye peak yako unaenjoy na kutawala then wakati wako unaisha afu muda unakuengua bila wewe kutaka ili upishe wasanii wengine watawale game.

Maana kila binadamu anakuwaga katika ubora wake mara moja tu maishani mwake. Mrema kuna time kidogo tu atinge ikulu, alikuwa kwenye prime yake. Ila kesho Mrema hata agombee na mimi ujumbe wa Nyumba 10 namnyoosha mapema tu. Sababu ni simple tu hayuko kwenye ubora wake tena. Mrema tayari kaishafubaa kisiasa.

Kwenye kilele chake Ferooz aliuza album yake kwa Mhindi kwa zaidi ya million 30, wakati huo daladala za Dar nauli 100 hadi 150. Hivyo million 30 ya miaka ile kwa inflation ya sasa ferooz angekuwa kadhibiti zaidi ya million 100 kwa ngoma zake tu kutoka kwenye album yake... Ferooz alikuwa kwenye prime yake. Lakini leo hii nyimbo mpya ya ferooz haifikishi views hata 30k huko YouTube. Amefubaa kimziki Ferooz.

Ni sawa na kifo tu, kifo hakina ubaya na mtu yeyote yule, chenyewe kinafanya Kazi ya kuondoa kizazi kilichozeeka na kuchoka ili kupisha kizazi kingine kipya cha watoto watawale na kuendesha Dunia. Its human nature to clear the old and welcome new one.

Siku hizi ninawaona wasanii wakongwe wa zamani wa bongo fleva kibao wakitaka kurudi kwenye game kwa kutambulisha ngoma zao mpya kibao redioni, ni jambo zuri... Lakini hawajui ukweli huu mchungu kwamba muziki huwa hautoi hiyo nafasi ya kuvuma mara mbili maana binadamu anakuwaga katika ubora wake mara moja tu maishani mwake yaani unataka kuniambia kuna siku TID atatoa ngoma kali kuliko Zeze? Au Fid Q anaweza kuna kutoa ngoma Kali zaidi ya Mwanza Mwanza? Ngoma aliyoitoa ikahit kwa mwaka mzima bila kutoa nyingine ambapo mwaka pekee huu katoa ngoma nne ila zote haipo hata moja iliyofikia robo ya mafanikio ya Mwanza Mwanza...!

Kuvuma mara mbili huwa haitokei na ikitokea inatokea kwa watu wachache sana, ambao ni very special na wenye extraordinary talent, lucky and potential. Mfano wa watu hawa ni kama huyu hapa chini;

Bwana Carlos Santana, mchawi wa gitaa Duniani huyu, ambae Dunia nzima inakiri jamaa anao uwezo wa kuliimbisha gitaa yaani anaweza kucharaza gitaa tu bila kuimba na ngoma yake hiyo ikafanya vizuri sokoni. Na kwa talent yake alikimbiza soko la muziki la Dunia kwa miaka zaidi ya 22 ya mafanikio mengi ambapo mwishoni kwa miaka hiyo 22.. Mwaka 1970, alitoa ngoma ya "black magic woman" ngoma hii ilihit sana Duniani hadi kuingia top 3 ya chart kubwa za muziki Duniani ikiwemo billboard. Akitumia lugha ya picha ya sanaa kuficha yaliyokuwa yanamsibu katika maisha yake halisi kwenye hiyo ngoma Santana alilalamika kwa hisia sana kwamba amenasa kwenye penzi la kigoli mweusi, mwenye utamu wa kustaajabisha na hawezi kuchomoka maana anampenda sana hadi amemfanya ageuze moyo wake uwe mgumu kama jiwe, wengi waliamini nguli huyu amependa kigoli cheusi dawa kutoka huko Cartagenà tamka (katagenya). kutokana na title yake ya "black magic woman" watu walibaki wanaielewa hii nyimbo kama ni ya mapenzi hadi pale waliposhuhudia muda mfupi baada ya hii nyimbo kuwa released, Santana alitoswa na lebo yake, kundi lake linavurugika, mke wake anamkimbia, na Santana anaokotwa mitaloni kalewa chakari!

Hapo ndipo santana akaweka wazi ukweli wa ile nyimbo kwamba mwaka ule 1970 ile nyimbo ya 'black magic woman' haikuwa kwa ajili ya mwanamke yeyote bali ilikuwa ni ajali ya yeye kuingia kwenye mapenzi mapya na madawa ya kulevya ambayo hakuweza kuwa na nguvu ya kufikiri hata kuyaacha tu yaliyomharibia maisha yake na career yake ya mziki. Na akakiri kwamba hataki tena maisha ya madawa na atafanya kila linalowezekana kuyashinda madawa na anawahidi Siku moja atarudi tena na kulishika soko la muziki Duniani kama awali. Alikaa kimya akifanyiwa rehab na akafanikiwa kwa kiasi flani kubadilisha lifestyle yake. Toka mwaka 1971 hadi mwaka 1999 yaani ilipita miaka 28 hajatoa ngoma yeyote.

Lakini ilipofika mwaka 1999 akiwa amerocover kutoka kwenye drugs abuse akaachia ngoma yake ya "smooth" na album ikijulikana kama "supernatural" album iliyotikisa Dunia kwa kuuza copy million 30, album yake ikipitia tuzo kubwa 9 za Grammy ikiwemo album of the year. Ilikuwa ni maajabu ya mvuta unga alierudi kwenye game na kuwakimbiza hadi wale waliokuwa mental and physically fit. Hii ni bahati ya mtende! Haitokei kwa watu wote! Ni kwa watu wachache tu special, talented, lucky enough with extraordinary talent.

Baada ya Carlos Santana Dunia haina rekodi za haraka haraka za watu walioukacha muziki kwa miaka kuanzia 5 na kurudi tena na kuliteka game. Hawapo! Na kama wapo ni wachache sana.

Hapa nataka niongee na wasanii wetu wa zamani kwamba wasitegemee kurudi na ngoma mpya na kuteka soko tena kwani huwa haitokei mara kwa mara... Nimeona hadi mkali Sir nature alitaka kutembelea nyota ya harmorapa kwa kufanya nae ngoma baada ya harmorapa kutrend... But haikutosha kumrudisha nature kwenye spotlight ya peak? Karudi na ngoma ya natoa lock but mapokezi yake yamekuwa hafifu sana, huko YouTube viewers walioangalia ngoma yake nature ni wachache sana.

Vivyo hivyo kwa maprodyuza, P funk aka Majani leo hii hata atengeneze biti ya mchiriku bado haiwezi kuhit kama zamani alipokuwa kwenye peak yake ambapo salama jabir host wa planet bongo alikuwa kila asubuhi ya jumamosi anaenda kwa Majani anapewa ngoma 20 ambazo zote ni hit na zinaingia top 10 ya ngoma Kali kila wiki. Hivi karibuni Majani katengeneza biti ya harmorapa feat juma nature. Biti nyepesi na unorganized kama ya amateur vile.

Ninachotaka kuwaambia wasanii malegendary ni waachane na kung'ang'ana kutoa ngoma mpya na watambue kwamba kama kuna ngoma zenye roho na zinaishi basi ni ngoma zao zile zamani kidogo, maana ni ngoma zao pekee ndio zenye uwezo wa kuibua hisia za matukio flani kila zikipigwa..mfano mimi nikisikia machozi ya lady jaydee nakumbuka nilikuwa na demu mkali sana huko mwanza tuliekuwa tunapigia show zetu ngoma hii ya jide then naamsha hisia nzuri za good old days kila ninapoisikia hii ngoma. Kila inapopigwa ngoma ya mgambo ya nature popote hisia za maisha yangu ya uhardcore na usela mavi wangu wa zamani inaguswa. And it feels good to feel it. Nikisikia Zeze nakumbuka ndio ilikuwa dedication kwa demu wangu those days. Sasa inakuwaje hawa wawe na concert afu nisiibuke? Kuchokoza hisia zangu? Mwaka mpya nature kakonga nyoyo za watu huko Mombasa kwa ngoma zake zile za long time ila hakuna alieomba kusikia natoa lock.

Sijui wanakosea wapi hawa wasanii wa zamani.. Maana kama ni fans wenye pesa na wanaopenda kuenjoy mziki mzuri, wenye Kazi na vipato vya uhakika ni basi ni fans wale wa zamani wanaozielewa na kuzikubali ngoma zao? Lakini inakuwaje wasanii wa zamani hawana mechanism ya kuchukua hela zao?

Ni msanii mmoja tu hapa bongo alifahamu kwa uzuri art(sanaa) ya jinsi ya kuishi na ngoma yake kwa miaka mingi na namna ya kupiga nayo hela na muda ukafika akafanana nayo.. Huyu ni Bi kidude! Yaani muhogo wa jang'ombe ilimpa platform ya Ku perform hadi majukwaa makubwa ya mbele huko Germany, USA na heshima kubwa tu akapata ikiwemo kuperfom jukwaa Moja na mega artist wa Dunia.

Ila shangwe alilolipata Dudubaya kule mtwara kwenye Wasafi festival limenifanya nikaamini kabisa Kwamba ngoma za zamani zinaishi na zina nguvu yake ambayo sio rahisi kuiona. Supernatural power flani hivi. Ambayo sipati maneno sahihi kuielezea.

Sababu dudubaya hakuimba alikuwa anapunga tu mikono kulia na kushoto huku halaiki ikiimba kwa munkari na morali ya hali ya juu. Old is gold.

Nawashauri malendary wa bongo fleva wawe na tamasha lao binafsi la wasanii magangwe, manguli wa zamani... Afande Sele, Daz nundaz, ferooz, Sir nature, soggydoggy, Mr Paul, e.t.c liitwe aidha "BB Legendary Flavour" humo watu watapata kila kitu cha zamani kuanzia music, comedy, acrobatic e.t.c malegendary mna kila kitu kizuri kuanzia genuine talent, experience, good music, potential e.t.c mnashindwaje wazee? mimi nahisi hawa njemba hawajui Lakini nataka niwambie kung'oa nywele moja kichwani kwa mkono ni Kazi rahisi sana ila kung'oa nywele nyingi kwa mkono ni kitu haiwezekani! Hii inamaanisha umoja wao hawa wasanii wa zamani ndio nguvu yao. Waungane watengeneze chao, hii itawanufaisha zaidi wao kiuchumi na kijamii. Their unity is their power.

Wasipobadilika watatumiwa kwa malipo kiduchu kutoka kwenye hizi summit kubwa za Fiesta, Wasafi festival, mziki mnene e.t.c Muhimu wazichunie hizi ili watu wawe na hamu ya kuwaona. Can you imagine mimi sijawahi kumuona nature akiperfom kwa miaka 12 mfululizo? Kwa hiyo nina kirarurau cha kumshuudia kibra matata, sir nature akikiwasha stejini live but sio under wasafi or fiesta sababu nikiingia nitawanufaisha wengine na sio nature . Sijawahi kumuona Afande Sele for so many years too. Nataka nimuone akiperfom kama kwenye jukwaa lao wenyewe wasanii wa zamani na sio under supervision ya hawa mabepari wawili fiesta na Wasafi festival.

Ninatoaga mfano wa hela... Hela ina thamani sababu haipatikani kiwepesi, kwa hiyo ili hawa wasanii wakubwa ili wazidi kuwa na thamani lazma wajifunze kutopatikana kirahisi kwenye majukwaa mengine isipokuwa jukwaa lao pekee. Wasafi wamemaster hii sanaa hawajaperform kwenye matamasha ya kibwege for years wametutengenezea kiu ya kutaka kuwaona jukwaani sasa hivi unaona tunavyoshonana kwenye festival yao kuwapelekea hela zao? Haya mambo ni sayansi na sio uchawi wala nini.

Ninajua kuna wasanii wa zamani kwa sasa wana maisha magumu hadi wanafikiria kwamba hela zao za mazishi wangepewa leo hii ili siku wakifa watajua nini cha kufanya.

Anyways, happy new year maana naona nazidi kutiririka tu sijui balimi zimenikolea?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha hapo mwisho nimecheka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pandagichiza

pandagichiza

JF-Expert Member
3,401
2,000
Mada nzuri tatizo ni ndefu sana sijaisoma yote
 

Forum statistics


Threads
1,424,934

Messages
35,076,363

Members
538,167
Top Bottom