Ukweli kuhusu laana (Curse)

Laana ipo.

Ukitaka kujua kuwa laana ipo, mkorofishe au mchukize kwa kiwango cha juu mzazi wako, shangazi yako au ndugu zako wa karibu kidamu afu akupe laana ndo utajua kuwa kweli ipo

Kwa ufupi ni kwamba, si rahisi sana kwa mzazi wako aliyekuzaa kukupa laana, ila wengine ndo hukimbilia kutoa laana.
 
Members naona sasa mnajadili hoja ya "kumjua ama kutomjua aliyepigwa laana". Msimamo wangu ni kuwa laana ipo.

Kimsingi laana ni tamko, ili laana ifanye kazi ni lazima iwe ni tamko la Mungu (ambalo tayari lipo ktk maandiko yake) au mtu ambaye anàtamka hayo kwa niaba ya Mungu.

Ili laana ikupate lazima uwe umevunja agizo la Mungu.

Kuonekana kuwa una laana ni ngumu sana maana matokeo yàke yana utata mwingi ni Mungu tu ndiye anajua.

Unaweza kufikiri mtu ana laana kwa mwonekano wa nje kumbe kuna nguvu nyingine ina mnynyasa.

Kwa hiyo kuhukumu flani ana laana kwa viashiria fulani ni tatizo.
 
Haijashindwa bado? Mpaka sasa wamezuia kifo sio?
Muwe mnajipanga kabla hamjauliza... Acheni kukurupuka... Ndio maana Sayansi hamuielewi na Dini hamzielewi... Kaa chini utulie kisha uliza swali moja subiri jibu kisha kulia lingine utapata jibu na utaelewa..

Soma thread inauliza nini? Hiyo kifo haihuaiani humu... Ila Sayansi inayo mijibu ya kila kitu... Just fuata hatua tu utaelewa...

Ukitaka kuishi kwa mashindano utapata taabu kwani Sayansi imechukua nafasi baada ya uumbaji unaouamini ikaunda hadi unachotumia kuandikia humu... Ukiumwa ni Sayansi inakitibu n.k.
 
Tulia sasa unaruka ruka nini kwa maneno meng?

Mimi nawew tumeanza ivi. Mi nimesema Sayansi haina majibu yote. We ukasema ina majibu yote. Mi nikakujibu mbona tatizo la kifo haijaondoa?

Unakuja na ngojera kwamba kifo hakipo ktk mjadala. Si nimeleta kwa hoja yako ya kuwa sayansi ni kila ktu?

Ukitaka kuwa mwongo uwe na kumbukumbu nzuri.
 
Ngoja nijaribubkueleza hivi. Kwanza nakubaliana na dhana kwamba LAANA ipo na ni jambo la kisaikolojia. Laana ni tukio ambalo humpata mtu ambaye ametenda jambo ovu kwa nia ovu huku akijua kuwa kufanya hivi ni makosa. Baada ya kulitenda kosa hilo la makusudi kwa undani wake moyo wake humsuta na ndio mwanzo wa sonona anbayo hugeuka kuwa mateso moyoni mwake. Hali hii ikiendelea kwa muda mrefu au mfupi kulingana na jinsi mateso yalivyo moyoni hugeuka kuwa majanga kwa mhusika na hapo ndipo tunasema Laana sasa imeanza kumpata mtenda. Kwa upande mwingine mtoa LAANA ni kitendo cha mtu mwema (Mzazi, Mlezi, nk) kwa nia ya kutoa karipio la kisaikolojia kwa mtenda maovu ambaye njia zingine zote za suluhu zimeshindikana basi humgeukia muumba wake na kunena kuwa na limpate...
 
laana siyo lazima itoke kwa wazazi tu, inatoka kwa jamii, na kwa viumbe wengine inategemea vipi umevunja mipaka ya ubinaadamu na kuwadharau, kudhuru au kudhulumu haki za watu au viumbe wengine. Kuna watu walifanya dhuluma kubwa na wakawa OK lakini mwisho wao ulikuwa mbaya sana na walijuta sana kabla mwisho wao haujafika . Kuwadharau wazazi na kuacha kuwasaidia wakati wewe una uwezo wa kuwasaidia huleta laana mbaya sana na mwisho huwa sio mzuri

Hakuna sayansi hapa - ni kuwa unaingia duniani kuna majukumu ya kibinaadamu yanakusubiri - ukikiuka kuna malipo yake hapa hapa
 
safi sana mkuu Mwenyezi wetu Muumba wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana akupe nguvu na maarifa zaidi uendeleze huduma ya neno lake kupitia karama aliyokupa.
 
Kumkasirisha mzazi kunaweza kuwa na sababu nyingi ila zipo ambazo hazina msingi kabisa mfano kuna baadhi ya wazazi kama ikitokea ukaoa mwanamke nje ya kabila au dini yao watakasirika na kutishia kukupa laana pia wapo baadhi ya wazazi wanaoweza kutumia udhaifu wa watu kuamini sana laana kutumiza matakwa yao mfano mzazi anaweza kulazimisha kufanya mapenzi na mtoto ikitokea mtoto anagoma atatishia kutoa laana na kama huyo mtoto anaamini sana laana ataishia kubakwa kila siku...
CONCLUSION,
Siamini kama kuna binadamu anayeweza kutoa laana hata kama ikiwa ni mzazi wako hana uwezo wa kukupa laana bila ya kuwepo mkono wa Mungu,Mungu ndo mtoaji laana wa kwanza na wa mwisho hakuna binadamu anayeweza kujifanya Mungu na kuanza kutoa laana hata mama yako na baba yako hawana uwezo huo.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…