Ukweli kuhusu laana (Curse)

Ukweli kuhusu laana (Curse)

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,752
Reaction score
21,974
wakuu habari zenu
kama tujuavyo sote ya kwamba kuna uzoefu uliozoeleka na kukaa mawazoni na katika fahamu za watu yumkini hata mimi na wewe, hii ni LAANA ambayo inaweza kutokana ati na wazazi, mizimu, au Mwenyezi Mungu, katika kufikiria hili nikapata maswali yafuatayo:-
*Je laana ni imani tu au ni uhalisia umpatao mhusika na kumuathiri bila yeye kuwa na njia ya kuepuka?

* Je, sayansi inaweza kutoa ushahidi wowote juu ya hili suala au itathibitisha tu matokeo ya laana mfano maradhi, njaa, ukame, umasikini au vita?

*Je, ni namna gani laana husafiri kutoka kwenye chanzo (mtoa laana) hadi kwa mhanga (anaye laaniwa)?

Karibuni tujuzane wakuu
 
kwa hiyo mkuu laana ni imani tu na sio suala halisi?
Ndiyo hivyo. Hiyo ni dini kama zilivyo imani za dini. Ni METAPHYSICAL. Na halina logic yoyote. Ingekuwa ipo kweli ni kwa nini itoke kwa wazazi ama watu wa karibu tu wakati maovu umewatendea watu mbali mbali?! Kwa nini ukikosa adabu kwa wengine usilaaniwe?! Hata hilo neno "baraka" ni upuuzi mtupu! Hakuna kitu kama hicho.! Na ndiyo maana hata ukisali kabla ya kula, yaani kukibaliki chakula, kama kina sumu itakuathiri tu na kama kina kipindupindu utaugua tu.
 
Ndiyo hivyo. Hiyo ni dini kama zilivyo imani za dini. Ni METAPHYSICAL. Na halina logic yoyote. Ingekuwa ipo kweli ni kwa nini itoke kwa wazazi ama watu wa karibu tu wakati maovu umewatendea watu mbali mbali?! Kwa nini ukikosa adabu kwa wengine usilaaniwe?! Hata hilo neno "baraka" ni upuuzi mtupu! Hakuna kitu kama hicho.! Na ndiyo maana hata ukisali kabla ya kula, yaani kukibaliki chakula, kama kina sumu itakuathiri tu na kama kina kipindupindu utaugua tu.
hahahaaa mkuu huamini katika laana wala baraka, hii ipo kwenye philosophy kama ulivyosema metaphysics, ina deal na mambo ya imani hasa tawi lake la theology
 
Kwa mfano mtu anaposema anavunja chungu (analaani)familia nzima iteketee na inakuwa kweli.
Naomba kuelewesha mahusiano ya laana na watu kufa.
 
Hapo ndipo utakapojua sayansi haina jibu la kila kitu. Sayansi sio ukweli wote. ukweli mwingine tunahitaji njia zingine (REVELATION).
revelation= ufunuo ni sahihi lakini naomba majibu ya hayo maswali japo umejibu hilo la sayansi vs laana,thanks but i need more
 
aisee watu wanachelewa kuja mana topic nzito sana hii, ila mi nadhan laana huitwa laana baada ya mapokeo ya mhusika, ukiiamini hapo ndipo huitwa laana na akili yako kuanza kujitesa yenyewe and not otherwise.
sawa mkuu unamaanisha unaweza kujiondoa kwenye laana kwa uamuzi wako?
 
subir ulaaniwe ndio utajua laana ipo.na uzr ukipata laana ww km ww huwezi kujijua ila wengine.hii ipo kiimani na nikwl ipo
i dont want to be a victim of this!! ila mimi nimeuliza ili tujadili wote kwa mapana mkuu, maana hii kitu ina tatanisha sana
 
Kwa mfano mtu anaposema anavunja chungu (analaani)familia nzima iteketee na inakuwa kweli.
Naomba kuelewesha mahusiano ya laana na watu kufa.
you've the same dilemma!!! haya mambo sijui ni nini tu na nguvu yake inatoka kwa nani(wapi)
 
Katika hali ya kawaida watu wa kale waliaminishwa vitu hivi yaani baraka na neema kuwa vipo alihali kiuhalisia ni kitu ambacho hakipo.. hii ni kwa upande wangu.
Umewahi kujiuliza kwann wanaotoa laana na baraka weng wao husemekana ni wazazi au wazee/walezi kuliko mtoto kutoa laana kwa mzazi?
Je hii laana ilipangwa kwa wakubwa tu wao ndo watoaji wa laana na baraka?

Jibu ni kwamba enzi za mababu zetu maneno haya laana na baraka yalitumika kujenga watoto kukaa katika malezi mazur yaan wasifanye vitu vibaya vya kuweza kuikwaza jamiii lasivyo walitishia watapata laana and vice vesa kwa baraka maneno haya yalitumika kama silaha tu na sikweli.
Na kama kuna ukweli uliwahi kumuona mtu kapata laana papo kwa papo? Hii imejengwa akilini mwa watu kuwa laana huja baadae...hakuna ukweli wowote na ili jambo ni imani tu tumejengewa kama ilivyo imani zingne.
 
Kwanza tujiulize neno laana latoka kwenye lugha gani? halafu ndio ulete huo ushahidi wako wa uongo latoka kwenye lugha ya kiarabu maana yake nikuwa mbali na kukubalika na Allah (Mwenyezimuungu) Hilo neno sisi wa swahili sio letu halafu hakuna dini itwayo sayansi kama hujui maana ya sayansi maana yake ni jitaahidi za uvumbuzi upo mkuu sio dini alio Kuja nayo Muhammad na Yesu isibitishe na sayansi hapana sayansi isibitishwe na vitabu vikatifu upo mzee cc waislamu na wakiristo hatuna dini itwayo sayansi upo
 
Back
Top Bottom