Ukweli kuhusu kuzorota kwa huduma ya M-PESA

Status
Not open for further replies.

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
22,491
19,434
Na Mwandishi wetu.

Siku mbili tu baada ya mtandao wa Vodacom M-pesa kurejea hewani, kuna taarifa zimeenea kwamba baada ya serikali kuishiwa fedha za kujazia kwenye bajeti yake ya 2014/2015, walienda kuomba mkopo Vodacom. Zoezi hilo lilisimaniwa kwa ukaribu kabisa na makada wawili wa CCM ambao walipewa jukumu la kusaka hizo fedha na kuhakikisha zinapatikana. Mmoja wa makada hao wa CCM ni mwanahisa katika kampuni ya Vodacom na ni mbunge kutoka mkoa mmoja wa kaskazini mwa Tanzania anayepigiwa chapuo kuwania urais kwa tiketi ya chama chake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Mwingine ni kada maarufu wa CCM, aliwahi kuwa mweka hazina wa chama, alijiudhuru ubunge baada ya kutuhumiwa kwa ufisadi na pia ana hisa Vodacom.

Serikali imetumia kete ya kuwatumia makada hawa kwa kuzingatia kwamba wana hisa kubwa kwenye kampuni husika, hivyo ni rahisi kukubaliwa na kampuni kwa kuwa wanahusika moja kwa moja katika umiliki wa kampuni hiyo. Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kumshawishi mmoja wa hao kada wawili akubali kuisaidia serikali kupata fedha hizo kutokana na kuwa na kinyongo na chama tangu alijiudhuru kwa tuhuma za ufisadi. Lakini, kufuatia kikao cha siri kilichoketi katika hoteli moja maarufu mkoani Dodoma, hatimaye kada huyo alifanikiwa kushawishiwa na kukubali kushiriki mpango huo.

Inasemakana kwamba serikali ilifanya juhudi kubwa kumshawishi kada huyu akubali kuisaidia kwa sababu hakukuwa na namna nyingine ya kuinusuru serikali na aibu ya kukosa fedha za bajeti. Kumbuka kwamba serikali imekwishakopa fedha nyingi sana katika mabenki ya ndani kiasi kwamba mabenki hawakubali tena kutoa fedha zao hadi serikali itakapoanza kuwalipa fedha zao. Pia serikali imeishakopa fedha nyingi sana kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hadi kupelekea baadhi ya mifuko hiyo, hasa mfuko wa PSPF, kufilisika. Hivyo isingekuwa rahisi kuendelea kukopa kwenye mifuko hii wakati imeishashindwa kulipa fedha hizo kufuatia ukweli kwamba mifuko hiyo imefilisika.

Ndipo sasa serikali ikaona kwamba njia pekee iliyobaki ni kuwatumia makada wake kuishawishi Vodacom iwape fedha za kuendeshea serikali. Kikao cha siri kati ya makada hao na mkurugenzi wa uendeshaji wa Vodacom, raia wa Afrika Kusini, kilifanyika katika hoteli moja katikati ya jiji inayopakana na bahari ya Hindi. Majadiliano yalikuwa makali sana. Meneja wa Vodacom alikubali kuwakopesha fedha serikali lakini alisema kwamba hawakuwa na fedha taslimu za kuwapa serikali kwani fedha nyingi walizokuwa nazo zimeelekezwa kwenye miradi ya kampuni kama vile ujenzi minara, uanzishaji wa huduma ya M-pawa na ukarabati wa njia za mawasiliano. Hata hivyo, makada hao wa CCM waliokuwa kwenye majadiliano walishauri Vodacom iwakopeshe fedha za wateja zilizopo kwenye akaunti zao za M-PESA amabzo serikali iliahidi kuzirejesha pindi ikizipata.

Suluhisho likawa limepatikana. Ila tatizo moja na lililokuwa linawaumiza kichwa ilikuwa ni namna ya kuchukua fedha hizo bila wateja kufahamu. Mmoja wa maofisa wa Vodacom, mwenye asili ya India alisika akisema: "The only way we can grab the customers' money from their accounts behind their knowledge is to disable the M-pesa system so that they can't be able to do any transaction." Maana yake ni kwamba: "Njia pekee tunayoweza kutumia kuchota fedha za wateja ni kuvuruga mfumo mzima wa M-pesa ili kwamba wasiweze kufanya muamala wowote". Baada ya kusema maneno hayo, wale makada wa chama walikuwa kimya huku wakimtazama kwa umakini na mmoja wao, aliyekuwa mevaa miwani, alionekana akitikisa kichwa kuashiria kwamba amekubaliana na mpango huo (haramu).

Kwa ufupi, hiki ndicho kilichotokea na kupelekea huduma ya M-pesa kutopatikana tangu siku ya Ijumaa mpaka Jumanne na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja waliokuwa wameweka fedha zao kwenye akaunti za M-pesa. Ilikuwa hakuna jinsi kwani kuchukua fedha za wateja bila kuvuruga huduma ya M-pesa isingewezekana. Lazima wateja wangekuwa wakali na wangefikia hatua ya kuipeleka kampuni mahakamani kwa kuwafanyia utapeli kama ule wa DECI.

Wananchi wamesikika wakilalamika kupata hasara kufuatia kuzorota kwa huduma ya M-pesa kwa takribani siku 6. Mpaka tunaenda mitamboni, kiasi halisi cha hasara iliyosababishwa na kuvurugwa kwa huduma ya M-pesa bado kilikuwa hakijapatikana.
Mwandishi wa makala haya aliwahoji watumiaji wa huduma za M-pesa katika maeneo mbalimbali jijini la Dar es Salaam ambapo wengi wao walidai pesa zimepungua kwenye akaunti zao, huku baadhi wakitishia kwenda mahakamani kuishitaki kampuni ya Vodacom. Hasara kadhaa zimeripotiwa kufuatia kukosekana kwa huduma hii ikiwemo, watu kufukuzwa kutoka kwenye nyumba za kupanga, watoto kufukuzwa shule kwa kutolipa karo na baadhi ya watu kufa hospitalini kwa kukosa fedha za kununulia dawa.

Mkazi wa Mwananyamala, Bw Juma John, alidai kufiwa na ndugu yake aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya mwananyamala kwa sababu ya kukosa fedha kumnunulia damu. "Naumia sana kwa kufiwa na ndugu yangu…ameferariki mbele yangu nikiwa sina la kufanya kwa sababu tu ya kushindwa kutoa shilingi elfu 30 za kunulia damu. Niliwaomba madaktari wamuongeze damu ndugu yangu na kuwaahidi kwamba nitalipa fedha zao pindi huduma ya M-pesa ikirudi, lakini walinikatalia". Mwananchi huyo alisikika akilalamika kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi.

Source: TANURU LA FIKRA

MOANI YANGU
Ndugu zangu watanzania, tunapaswa kuamka kutoka kusingizini na kuidai fidia Vodacom kwa kukubali kula njama na serikali ili kuiba fedha za wateja kwa madhumuni ya kifisadi. Suala hili halina tofauti na ufisadi wowote ule unaofanywa na mafisadi hapa nchini. Mimi ni mmoja wa watu walioathirika na huduma hii na ninajipanga kumtafuta wakili anayejua masuala ya fedha anisimamie nifungue kesi mahakamani nikaidai kampuni hiyo fidia kwa ajili ya usmumbufu na utapeli. Pamoja na kwamba serikali imekopa fedha Vodacom kwa ajili ya kufanyia mambo ya msingi ya kuendeshea serikali, haikubaliki hata kidogo Vodacom kuharibu mtandao wa M-pesa kwa makusudi na kusababisha usumbufu kwa mamilioni ya watanzania wanaotunza fedha zao kwenye akaunti za M-pesa.

:yield:
 
Hivi hizi mambo za kijiweni bado zinashadadiwaga tu maana hakuna proof yeyote juu ya hili.. Thanks for the copy n paste..
 
Kuna kitu hakiko sawa hapa:
  • Hizo fedha zilitakiwa kwa ajili ya kujazia bajeti 2014/2015 kivipi? Mbona MPESA ilipotea hewani jioni siku ya jumamosi tarehe 14.06.2014 na kurejea hewani Jumanne tarehe 17.06.2014? Inamaana zilihitajika kwa siku moja tu?
  • Bajeti ya serikali ilisomwa bungeni tarehe 12.06.2014, iweje M-PESA ikatike 14.06.2014?

Mkuu tpaul hebu tufafanulie vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Uongo mwingine unaudhi hata kuusikia..kwahiyo serikali imeshailipa vodacom kabla budget kupita?nani kakuambia benk zmeishiwa pesa za kuikopesha serikali?mawazo ya maiti haya
 
Ukiwa na Raisi kama Kikwete unategemea nini kitokee nchi kuuzwa tu hatari kubwa sana na sisi wananchi hatufani kitu nchi nyingine kungezuuka maanadamano yasiyoyakawaida watu kudai fedha zao na huduma chini ya masaa mawili tu
 
Acha porojo mkuu...unachokisema ni kitu ambacho hakipo...hivi mtu unawezaje kukaa muda mrefu kutunga riwaya kama hizi zisizo na kichwa wala mkia?

By the way,hela ya bajeti huwa ni estimation ya mapato na matumizi...hakuna real money kwa sasa..hela iko kwenye makaratasi......
 
eti chanzo tanuru la fikra kunawatu wajinga nchi hii acha tu.
 
Acha porojo mkuu...unachokisema ni kitu ambacho hakipo...hivi mtu unawezaje kukaa muda mrefu kutunga riwaya kama hizi zisizo na kichwa wala mkia?

By the way,hela ya bajeti huwa ni estimation ya mapato na matumizi...hakuna real money kwa sasa..hela iko kwenye makaratasi......

mkuu wala usipate tabu na huyu mburula ambaye kila kitu ni uongo na uzushi kwa faida ya ujinga wake.
 
Ingawa siipendi CCM ya serikali yake HABARI HII NI ya UWONGO, UDAKU, UMBEYA NA UZABIZABINA.

tpaul sisi ni watu wazima na tunaelewa taratibu za uandaaji wa bajeti ya serikali vizuri sana. Kama bajeti inayojadiliwa ni ya mwakani hizo pesa za kuchukuliwa voda sasa serikali inazipeleka wapi kwa sasa???

Anyways kuendelea kujadili huu uzi ni kudhihirisha upumbavu na kuficha hekima. Potelea kuleeeee
 
Na Mwandishi wetu.

Siku mbili tu baada ya mtandao wa Vodacom M-pesa kurejea hewani, kuna taarifa zimeenea kwamba baada ya serikali kuishiwa fedha za kujazia kwenye bajeti yake ya 2014/2015, walienda kuomba mkopo Vodacom. Zoezi hilo lilisimaniwa kwa ukaribu kabisa na makada wawili wa CCM ambao walipewa jukumu la kusaka hizo fedha na kuhakikisha zinapatikana. Mmoja wa makada hao wa CCM ni mwanahisa katika kampuni ya Vodacom na ni mbunge kutoka mkoa mmoja wa kaskazini mwa Tanzania anayepigiwa chapuo kuwania urais kwa tiketi ya chama chake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Mwingine ni kada maarufu wa CCM, aliwahi kuwa mweka hazina wa chama, alijiudhuru ubunge baada ya kutuhumiwa kwa ufisadi na pia ana hisa Vodacom.

Serikali imetumia kete ya kuwatumia makada hawa kwa kuzingatia kwamba wana hisa kubwa kwenye kampuni husika, hivyo ni rahisi kukubaliwa na kampuni kwa kuwa wanahusika moja kwa moja katika umiliki wa kampuni hiyo. Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kumshawishi mmoja wa hao kada wawili akubali kuisaidia serikali kupata fedha hizo kutokana na kuwa na kinyongo na chama tangu alijiudhuru kwa tuhuma za ufisadi. Lakini, kufuatia kikao cha siri kilichoketi katika hoteli moja maarufu mkoani Dodoma, hatimaye kada huyo alifanikiwa kushawishiwa na kukubali kushiriki mpango huo.

Inasemakana kwamba serikali ilifanya juhudi kubwa kumshawishi kada huyu akubali kuisaidia kwa sababu hakukuwa na namna nyingine ya kuinusuru serikali na aibu ya kukosa fedha za bajeti. Kumbuka kwamba serikali imekwishakopa fedha nyingi sana katika mabenki ya ndani kiasi kwamba mabenki hawakubali tena kutoa fedha zao hadi serikali itakapoanza kuwalipa fedha zao. Pia serikali imeishakopa fedha nyingi sana kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hadi kupelekea baadhi ya mifuko hiyo, hasa mfuko wa PSPF, kufilisika. Hivyo isingekuwa rahisi kuendelea kukopa kwenye mifuko hii wakati imeishashindwa kulipa fedha hizo kufuatia ukweli kwamba mifuko hiyo imefilisika.

Ndipo sasa serikali ikaona kwamba njia pekee iliyobaki ni kuwatumia makada wake kuishawishi Vodacom iwape fedha za kuendeshea serikali. Kikao cha siri kati ya makada hao na mkurugenzi wa uendeshaji wa Vodacom, raia wa Afrika Kusini, kilifanyika katika hoteli moja katikati ya jiji inayopakana na bahari ya Hindi. Majadiliano yalikuwa makali sana. Meneja wa Vodacom alikubali kuwakopesha fedha serikali lakini alisema kwamba hawakuwa na fedha taslimu za kuwapa serikali kwani fedha nyingi walizokuwa nazo zimeelekezwa kwenye miradi ya kampuni kama vile ujenzi minara, uanzishaji wa huduma ya M-pawa na ukarabati wa njia za mawasiliano. Hata hivyo, makada hao wa CCM waliokuwa kwenye majadiliano walishauri Vodacom iwakopeshe fedha za wateja zilizopo kwenye akaunti zao za M-PESA amabzo serikali iliahidi kuzirejesha pindi ikizipata.

Suluhisho likawa limepatikana. Ila tatizo moja na lililokuwa linawaumiza kichwa ilikuwa ni namna ya kuchukua fedha hizo bila wateja kufahamu. Mmoja wa maofisa wa Vodacom, mwenye asili ya India alisika akisema: “The only way we can grab the customers’ money from their accounts behind their knowledge is to disable the M-pesa system so that they can’t be able to do any transaction.” Maana yake ni kwamba: “Njia pekee tunayoweza kutumia kuchota fedha za wateja ni kuvuruga mfumo mzima wa M-pesa ili kwamba wasiweze kufanya muamala wowote”. Baada ya kusema maneno hayo, wale makada wa chama walikuwa kimya huku wakimtazama kwa umakini na mmoja wao, aliyekuwa mevaa miwani, alionekana akitikisa kichwa kuashiria kwamba amekubaliana na mpango huo (haramu).

Kwa ufupi, hiki ndicho kilichotokea na kupelekea huduma ya M-pesa kutopatikana tangu siku ya Ijumaa mpaka Jumanne na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja waliokuwa wameweka fedha zao kwenye akaunti za M-pesa. Ilikuwa hakuna jinsi kwani kuchukua fedha za wateja bila kuvuruga huduma ya M-pesa isingewezekana. Lazima wateja wangekuwa wakali na wangefikia hatua ya kuipeleka kampuni mahakamani kwa kuwafanyia utapeli kama ule wa DECI.

Wananchi wamesikika wakilalamika kupata hasara kufuatia kuzorota kwa huduma ya M-pesa kwa takribani siku 6. Mpaka tunaenda mitamboni, kiasi halisi cha hasara iliyosababishwa na kuvurugwa kwa huduma ya M-pesa bado kilikuwa hakijapatikana.
Mwandishi wa makala haya aliwahoji watumiaji wa huduma za M-pesa katika maeneo mbalimbali jijini la Dar es Salaam ambapo wengi wao walidai pesa zimepungua kwenye akaunti zao, huku baadhi wakitishia kwenda mahakamani kuishitaki kampuni ya Vodacom. Hasara kadhaa zimeripotiwa kufuatia kukosekana kwa huduma hii ikiwemo, watu kufukuzwa kutoka kwenye nyumba za kupanga, watoto kufukuzwa shule kwa kutolipa karo na baadhi ya watu kufa hospitalini kwa kukosa fedha za kununulia dawa.

Mkazi wa Mwananyamala, Bw Juma John, alidai kufiwa na ndugu yake aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya mwananyamala kwa sababu ya kukosa fedha kumnunulia damu. “Naumia sana kwa kufiwa na ndugu yangu…ameferariki mbele yangu nikiwa sina la kufanya kwa sababu tu ya kushindwa kutoa shilingi elfu 30 za kunulia damu. Niliwaomba madaktari wamuongeze damu ndugu yangu na kuwaahidi kwamba nitalipa fedha zao pindi huduma ya M-pesa ikirudi, lakini walinikatalia”. Mwananchi huyo alisikika akilalamika kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi.

Source: TANURU LA FIKRA

MOANI YANGU
Ndugu zangu watanzania, tunapaswa kuamka kutoka kusingizini na kuidai fidia Vodacom kwa kukubali kula njama na serikali ili kuiba fedha za wateja kwa madhumuni ya kifisadi. Suala hili halina tofauti na ufisadi wowote ule unaofanywa na mafisadi hapa nchini. Mimi ni mmoja wa watu walioathirika na huduma hii na ninajipanga kumtafuta wakili anayejua masuala ya fedha anisimamie nifungue kesi mahakamani nikaidai kampuni hiyo fidia kwa ajili ya usmumbufu na utapeli. Pamoja na kwamba serikali imekopa fedha Vodacom kwa ajili ya kufanyia mambo ya msingi ya kuendeshea serikali, haikubaliki hata kidogo Vodacom kuharibu mtandao wa M-pesa kwa makusudi na kusababisha usumbufu kwa mamilioni ya watanzania wanaotunza fedha zao kwenye akaunti za M-pesa.

:yield:

Inaelekea shule hujaenda.yaani mpaka leo ujui maana ya budget.kiufupi bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi.kinachoitajika bungeni ni makaratasi tu sio pesa taslim
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom