Ukweli kuhusu kile kinachoitwa Chunusi

Zaidi ya miaka 7 na bado haijachuja😄

Hongera mkuu! Una kipaji cha aina yake.
 
Nguo uliziacha?
 
Chunusi wa baharini ni rip currents..ogopa sana sehemu za ufukweni ambazo zinaonekana zimetulia hazina mawimbi. Chini yake kuna mkondo wa maji ambao unatembea horizontally kurudisha maji ndani ya bahari..Ukinasana humo unaweza kuvutwa zaidi ya mita 100 ndani ya bahari na kama sio mzoefu wa kuogelea basi lazima uzame na kufa.

Sehemu salama kuogelea baharini ni zile zenye mawimbi yaliyoungana ila ukiona sehemu mawimbi yameachana ikimbia kwasababu ndani yake kuna Rip currents na inavuta kwa haraka sana zaidi ya spidi ya bingwa wa kuogelea kwa kasi duniani michael phelps.

Unachotakiwa kufanya ni kutoshindana na Rip currents...relax acha yakuvute ndani kidogo ya bahari...tunza energy yako ukijaribu kukinzana nayo kurudi ufukweli hutaweza, mwisho wa siku utachoka sana na utazama.

So ukisharelax na kuacha mkondo wa maji ukupeleke ndani kidogo mpaka unapoisha nguvu yake...unatakiwa uogelee parallel kuukata mkondo na kuingia sehemu yenye mawimbi ambayo yatakurudisha kwa haraka ufukweni.

Mwaka 2004 nilinusurika kuzama pale Coco beach...sisahau mpk leo...kwasababu niliingia kwenye huu mkondo halafu ghafla nikahisi chini kuna kitu kinanivuta kuzidi kuingia baharini mpk nikashindwa kabisa kugusa chini vidole vyangu...Namshukuru Mungu niliweza kutoka salama...toka siku hiyo ilinifanya niiheshimu bahari.

Ukiwa ndani ya maji usipanic...kitendo cha kupanic jua utapoteza energy yako na mwisho hofu itakupelekea kuzama.

Kuweni waangalifu muwapo Baharini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…