Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,399
- 829,717
Kwanza Niombe radhi kwa kuahidi mara nyingi kuweka hii post lakini bila kufanya hivyo!
Tunazungumzia chunusi mnyama, shetani, jini au kizuka. Sio chunusi zile za usoni zinazotokana kwa sehemu kubwa kuibana au kuwa domozege! Hapa ni chunusi mtoa roho, majini.
Tumekulia kwenye hizo habari, tumepoteza ndugu jamaa na hata marafiki huko kwenye mito maziwa na hata baharini sababu ikitajwa kuwa ni chunusi.
Ukweli huu hapa
1. Chunusi wa kishirikina - Hapa ni kiumbe jini ndio kinaua kimazingara na binadamu kutafsiri kuwa ni chunusi (nimeshindwa kwa hakika kupata uhalisia na chanzo cha chunusi kuhusishwa na maji)
2. Wanyama wa majini(kwenye maji). Wapo wanyama wasiojulikana sana waishio kina kirefu cha maji ambao nao kwa namna moja au nyingine wamesababisha mauaji na kudhaniwa kuwa ni chunusi - hapa hakuna chembe ya ushirikina.
3. Chunusi kutokana na mkondo wa maji (strong current) Haya ndio yanaweza kuwa maelezo sahihi zaidi kuhusu chunusi.
Mara nyingi chini ya uso wa maji hupita mikondo ya maji inayoenda kasi sana na inayopita kina kirefu cha maji. Mikondo hii iko ya aina mbili;
- Mikondo ya maji inayoonekana juu ya uso wa maji
- Mikondo ya maji isiyoonekana juu ya uso wa maji.
Hii sasa ndio hatari sana kwa kuwa ukiangalia utaona maji yametulia kabisa lakini kumbe huko chini yake ni habari nyingine
Wenzetu ambao sio wavivu wa kufikiri waliamua kufanya utafiti wa kwanini kuna baadhi ya maeneo yanaua sana (dhana ya chunusi) na hiki ndicho walichogundua na kuweka tahadhari kwa wasiojua.
Sisi tumekuzwa na hulka moja mbaya sana ya kupuuzia mambo hata kama kuna chunusi wa kichawi lakini ufafanuzi wa jinsi hii ungehitajika!
Kumbuka bado tuko kwenye msiba wa ndugu zetu watatu waliopoteza maisha kwa kudhaniwa ni mumiani wanyonya damu. Tungekuwa na matangazo kwenye vyombo vya habari yanayotoa elimu na ufafanuzi kuhusu mambo kama haya wale ndugu pengine wangesalimika.
Kwenye dhana nzima ya chunusi inasemekana kuna chunusi wa aina mbili;
A. Chunusi anayeua na kuondoka na maiti (uhalisia ni mkondo mkali wa maji)
B. Chunusi anayeua na kuacha maiti akinyonya damu tuu (uhalisia ni kifo kinachotokana na viumbe wa majini)
Hizi za mwisho ni picha zinazodhaniwa ni za chunusi ambao wamewindwa na kuuawa na sasa nyama yao iko sokoni (sio Tanzania).