Ukweli kuhusu hali ya Mabenki Tanzania.

Duh! mambo haya yanawenyewe hiyo hoja ya kwanza nimetoka kapa!! nasubiri hiyo tathmini uliyotabiri hapo mwishoni
 
Too narrow brother...umeelezea Kama mwanasiasa uliyetumwa to clear atmosphere.. Economists huwa tunaelezea kwa data not blah blah... I was expecting unambie kati ya 2016 na miaka ya nyuma ratio ya non performing loans ni kiasi gani? To help for more than five years Crdb imerecord non performing loans kubwa 2016 kubwa kuliko miaka ya nyuma ndio maana bank ikasitisha mikopo... Na bank husitisha utoaji wa mikopo tu inapoona mikopo mingi Inakuwa ngumu to recover (bad debt) and this issue imeenda not only to Crdb but also NMB Postal bank..and to cut the story chanzo cha bad debts huwa ni kuporomoka kwa uchumi kwa wananch au bank kutokuwa makini kwa akina nani wakuwapa mikopo which hili always haliwezi kuwa tatizo. etc
Umezungumzia issue ya twiga bank.. Can you kindly explain ni kiasi gani bank inatakiwa iwe nacho kama minimum mtaji na ni when bank ili fall out of minimum balance as capital? Usiniambie serikali sijui iliacha ijiendeshe bila mtaji kwa sababu wao ndio wamiliki.. Unajua Maana ya required ratio? B. O. T could not allow such thing.. Hili tatizo la twiga ni 2016
Umeandika Bla Bla Bla Kama majibu wanayotoa akina Mwi...mpaka uvivu kukujibu
Mkuu kama wewe unafahamu hayo si utuelezee humu na sio kumponda mwenzio.

Lete hizo takwimu unazozitaka na sio kuzodoa na kuhoroja
 
katika hali yoyote ile ya kutapatatapa either kwa boti kuzama au kuanguka kwa uchumi, kuna makundi matatu huibuka...kundi la kwanza huweka mkazo kuwa uchumi uko sawia (Optimism) na kundi la pili huwa na mtazamo hasi (Pessimism) na kundi la mwsho huwa ni wale wenye mtazamo wa kineutrolali (Neutral). Uchumi ukijakuyumba hawajamaa optimist huwa wanakuwa na hali mbaya sana kisaikologia kutokana na kuonyesha udhaifu wao wa kuchambua masuala makubwa kama haya yanayoligusa taifa (Refer Global Economic Crisis). kwa suala hili la uchumi kwenda mrama si ajabu kumuona mtu kama huyu bwana mdogo akiinuka na kusema hali ya uchumi iko sawa (kwa ufupi ni kuwa huyu jamaa yuko U.S.A na sio Tanzania), pili ni mwanachama mtiifu wa chama kinachoongoza na ni mfanyakazi wa serikali (namwita middle income person). Nenda uendako wanaoanza kuonja joto la mtikisiko wa uchumi ni hawa lower income (unstable income earners) sio wenye kaliba za watu kama martin. Ndg mafuru alieleza wazi kuwa kuna liquidity problem iliyo sababishwa na serikali kuweka hela B.O.T na vile hawajaanza kurelease kwenye projects (NB. PM kalisema hili jana Arusha). wadau wengi mtaani wanakwambia hali ya uchumi haiko OK kutokana na mdororo wa biashara na viwanda kuonyesha nia ya kufungwa/kupunguza wafanyakazi (pessimist class). Kwa ushauri wangu huyu jamaa amalize masomo yake na arudi aendelee na kibarua chake
 
Mkuu The Tomorrow People umeongeza mkangnayiko badala ya kusawazisha mambo. Mimi naomba unisaidie majibu ya maswala machache kutokana na maelezo kwamba banks zinaoperate under prudential limits:

1. Kuna hoja kwamba hakuna tatizo la liquidity kwenye mfumo wa fedha nchini. Hili naomba tutofautiane tatizo la liquidity lipo na halisababishwi na serikali kuondoa pesa pekee zipo na sababu nyingine pia. Mathalani serikali imeondoa pesa na kupiga marufuku ufunguaji wa Fixed Deposit accounts kwa taasisi zake, biashara zimedorora (hii unaweza kuangalia data zako hasa performance ya service industry) na hata watu wenyewe wamekuwa wagumu kusave pesa bank. Kitendo cha kulipa accruing tax in one lumpsum kina maana ya kutoa pesa kwenye mfumo wa kibank na kuzizika BOT. Haya yote kwa pamoja yanapunguza amount ya bank deposit kuboost liquidity.

Kukataa kwamba liquidity ni tatizo ni kukataa kukubali dalili zinazojionesha kwa uwazi. Katika kikao cha taasisi za fedha na BOT, iliripotiwa kuna tatizo la liquidity na BOT wakasema watatoa fedha kunusuru hali hiyo. Kama wangekuwa wako within prudential limits, kwa nini BOT inatoa fedha kuboost liquidity? Na unahisi kwa nini wamesitisha kutoa mikopo au wenzetu hamsomi sababu ambazo wenye mabank wametoa?
 
Wana bodi,

Kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka vyanzo tofauti, nyingi zikipendekeza kuwa hali ya mabenki ni mbaya, ya kutia mashaka, na kuonesha dalili ya mabenki kufilisika. Nimeamua kuandika machache na kwa ufupi, kutokana na uchunguzi na tathmini ya kitaalamu. Sababu za kuandika ni mbili. Moja, kwa kuwa uchumi na hasa sekta ya fedha ni eneo langu la taaluma, na nitakuwa sitawatendei haki watanzania kama sitasema neno. Pili, mabenki na sekta ya fedha ni moyo wa uchumi. Midororo na misukosuko mingi katika historia ya chumi za dunia, mara nyingi huanzia katika sekta ya fedha. Naomba kusema kwa ufupi, kwa hoja tatu.

Hoja ya Kwanza: kumekuwa na tatizo ambalo ni la kawaida katika sekta ya fedha la kutolipa madeni wadaiwa. Benki nyingi, na hasa CRDB imekuwa na tatizo hilo. Kwa utaratibu wa kawaida, mabenki hukisia uwezekano wa kutolipwa na kuweka pembeni uwekezano huo (provision), na wakati mwingine kufanya juhudi za kuweka mikakati ya kuyakusanya (restructuring) kihasibu na kisera. Inaposhindikana, mabenki hutambua kuwa haitalipwa na kuweka kama gharama (expensing loans write offs). Hii hupunguza faida. Kwa CRDB imekuwa na athari kubwa, na pengine hutokea mabenki yakafanya hivi kwa pamoja au kwa namna ya msimu, na hivyo hili limetokea katika robo ya tatu ya mwaka 2016. Takwimu zinaonesha kuwa katika trilioni 16.7 zilizokopeshwa, kuna uwezekana wa trilioni 1.43 kutolipwa (non-performing loans) (asilimia 8.6). Kiwango hiki kwa Tanzania ni cha kawaida, tena cha chini kuliko nchi nyingi za kusini mwa Sahara ambazo viwango vyao hufika hadi asilimia zaidi ya 20.

Hoja ya Pili: Kulikuwa na kutoelewana kati ya mabenki na serikali kuhusu kodi ya mapato yatokanayo na mikopo ya benki. Mabenki mengine yalifungua kesi dhidi ya TRA. Lakini katika mwaka 2016 mfano, CRDB walishindwa kesi na hivyo wakatakiwa kulipa kodi hiyo, ambayo ilijumuisha pia kodi ya vipindi vya nyuma (retrospective). Benki nyingi ziliona matumaini ni machache, itawalazimu kulipa kodi hiyo ya serikali. Kwa hiyo muhula wa tatu wa mwaka 2016, mabenki mengi yakatambua kodi hiyo kama gharama. Na ndio maana faida katika mabenki mengi na sekta ilishuka kwa kasi sana, ukizingatia hoja ya kwanza na hoja hii ya pili.

Hoja ya Tatu: Wengi wamehusianisha hasara hii na tatizo la mtaji katika benki ya Twiga. Ukweli ni kuwa, uhusiano ni mdogo sana. Kilichotokea benki ya Twiga, ni kuwa wamekuwa na tatizo la mtaji kwa muda mrefu, wa karibu miaka kumi. Wakaomba serikali aliye mmiliki aongeze mtaji, hilo halikufanyika. Kwa sababu serikali ni mmiliki, benki ikaendelea kuendeshwa bila mtaji wa kutosha. Pamoja na tatizo la mikopo kwa kiasi fulani, hali ikawa mbaya hadi hapo Benki Kuu walipoamua kuchukua dhamana ya benki. Jambo jema linalokuja, ni kuwa wawekezaji binafsi wamekaribishwa kuingiza mtaji, na hadi ninapoandika, Mohammed Dewji na Exim Bank ya China wana nafasi kubwa ya kushinda tenda hiyo.

Nimesikitishwa na upotoshaji unaofanywa, tena na wataalamu. Wakizungumzia kuwa kuna ukasi wa mtitiriko wa fedha (liquidity) katika sekta ya fedha kutokana na serikali kutoa fedha zake na kuziweka benki kuu. Ukweli ni kuwa serikali ilitoa shilingi bilioni 515, wakati liquidity ya mabenki yote kwa takwimu za Disemba 2015, ni bilioni 9,004. Kiasi kilichotolewa ni asilimia 5.7 pekee ya ujazo wa fedha. Na fedha hizi mabenki yanaweza kuzikopa kutoka benki kuu. Kwa tathmini yangu, viashiria vyote ya msingi (fundamentals) vya sekta ya fedha kama mtaji, ujazo wa fedha, ubora wa dhamana, faida na ubora wa uongozi wa mabenki (CAMEL) vipo katika viwango vinavyokubalika (prudential limits). Na mwisho, tathmini yangu inaonesha kuwa mwisho wa mwaka 2016, robo ya nne, mabenki mengi na kwa ujumla wake, yatarekodi faida.

Genuine Martin (Economics PhD Candidate, Northern Illinois University, USA)
ww umeatoa hoja kitaalamu kabisa lakini kuna wapotoshaji hawatataka kuelewa.
 
mdau mpya

...Huyo jamaa, haongelei uchumi kuyumba. Ukisoma sentensi ya kwanza, utaona anazungumzia hoja ya mabenki kufilisika. Na hilo amelitolea hoja hizo tatu.

king kan

...Unaposema, "biashara zimedorora (hii unaweza kuangalia data zako hasa performance ya service industry) na hata watu wenyewe wamekuwa wagumu kusave pesa bank." na kuhusisha hii na Serikali kuondoa kiasi cha fedha kwenye mabenki, huoni unaleta mkanganyiko?

...Hawana hela, wata save nini?

...Well, mi ntasema kwamba, mdororo uliopo kwenye biashara, unatokana na upungufu wa kipato (cha halali, and otherwise) cha wananchi. Hili limesababishwa kwa kiasi kikubwa na Serikali kupunguza au kuondoa matumizi, mazingira ya kibiashara kubadilika, n.k.

...Je, hali hii itapelekea mdororo wa uchumi? The jury is still out!
 
Wana bodi,

Kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka vyanzo tofauti, nyingi zikipendekeza kuwa hali ya mabenki ni mbaya, ya kutia mashaka, na kuonesha dalili ya mabenki kufilisika. Nimeamua kuandika machache na kwa ufupi, kutokana na uchunguzi na tathmini ya kitaalamu. Sababu za kuandika ni mbili. Moja, kwa kuwa uchumi na hasa sekta ya fedha ni eneo langu la taaluma, na nitakuwa sitawatendei haki watanzania kama sitasema neno. Pili, mabenki na sekta ya fedha ni moyo wa uchumi. Midororo na misukosuko mingi katika historia ya chumi za dunia, mara nyingi huanzia katika sekta ya fedha. Naomba kusema kwa ufupi, kwa hoja tatu.

Hoja ya Kwanza: kumekuwa na tatizo ambalo ni la kawaida katika sekta ya fedha la kutolipa madeni wadaiwa. Benki nyingi, na hasa CRDB imekuwa na tatizo hilo. Kwa utaratibu wa kawaida, mabenki hukisia uwezekano wa kutolipwa na kuweka pembeni uwekezano huo (provision), na wakati mwingine kufanya juhudi za kuweka mikakati ya kuyakusanya (restructuring) kihasibu na kisera. Inaposhindikana, mabenki hutambua kuwa haitalipwa na kuweka kama gharama (expensing loans write offs). Hii hupunguza faida. Kwa CRDB imekuwa na athari kubwa, na pengine hutokea mabenki yakafanya hivi kwa pamoja au kwa namna ya msimu, na hivyo hili limetokea katika robo ya tatu ya mwaka 2016. Takwimu zinaonesha kuwa katika trilioni 16.7 zilizokopeshwa, kuna uwezekana wa trilioni 1.43 kutolipwa (non-performing loans) (asilimia 8.6). Kiwango hiki kwa Tanzania ni cha kawaida, tena cha chini kuliko nchi nyingi za kusini mwa Sahara ambazo viwango vyao hufika hadi asilimia zaidi ya 20.

Hoja ya Pili: Kulikuwa na kutoelewana kati ya mabenki na serikali kuhusu kodi ya mapato yatokanayo na mikopo ya benki. Mabenki mengine yalifungua kesi dhidi ya TRA. Lakini katika mwaka 2016 mfano, CRDB walishindwa kesi na hivyo wakatakiwa kulipa kodi hiyo, ambayo ilijumuisha pia kodi ya vipindi vya nyuma (retrospective). Benki nyingi ziliona matumaini ni machache, itawalazimu kulipa kodi hiyo ya serikali. Kwa hiyo muhula wa tatu wa mwaka 2016, mabenki mengi yakatambua kodi hiyo kama gharama. Na ndio maana faida katika mabenki mengi na sekta ilishuka kwa kasi sana, ukizingatia hoja ya kwanza na hoja hii ya pili.

Hoja ya Tatu: Wengi wamehusianisha hasara hii na tatizo la mtaji katika benki ya Twiga. Ukweli ni kuwa, uhusiano ni mdogo sana. Kilichotokea benki ya Twiga, ni kuwa wamekuwa na tatizo la mtaji kwa muda mrefu, wa karibu miaka kumi. Wakaomba serikali aliye mmiliki aongeze mtaji, hilo halikufanyika. Kwa sababu serikali ni mmiliki, benki ikaendelea kuendeshwa bila mtaji wa kutosha. Pamoja na tatizo la mikopo kwa kiasi fulani, hali ikawa mbaya hadi hapo Benki Kuu walipoamua kuchukua dhamana ya benki. Jambo jema linalokuja, ni kuwa wawekezaji binafsi wamekaribishwa kuingiza mtaji, na hadi ninapoandika, Mohammed Dewji na Exim Bank ya China wana nafasi kubwa ya kushinda tenda hiyo.

Nimesikitishwa na upotoshaji unaofanywa, tena na wataalamu. Wakizungumzia kuwa kuna ukasi wa mtitiriko wa fedha (liquidity) katika sekta ya fedha kutokana na serikali kutoa fedha zake na kuziweka benki kuu. Ukweli ni kuwa serikali ilitoa shilingi bilioni 515, wakati liquidity ya mabenki yote kwa takwimu za Disemba 2015, ni bilioni 9,004. Kiasi kilichotolewa ni asilimia 5.7 pekee ya ujazo wa fedha. Na fedha hizi mabenki yanaweza kuzikopa kutoka benki kuu. Kwa tathmini yangu, viashiria vyote ya msingi (fundamentals) vya sekta ya fedha kama mtaji, ujazo wa fedha, ubora wa dhamana, faida na ubora wa uongozi wa mabenki (CAMEL) vipo katika viwango vinavyokubalika (prudential limits). Na mwisho, tathmini yangu inaonesha kuwa mwisho wa mwaka 2016, robo ya nne, mabenki mengi na kwa ujumla wake, yatarekodi faida.

Genuine Martin (Economics PhD Candidate, Northern Illinois University, USA)
Kumbe na huyu ticha wangu chuoni yuko humu. Tumekusoma mkuu maelezo mazuri, ila watu kama nyie kwa serikali ya sasa hamna maana maana mnaweza kutoka mapendekezo mazuri ila yakatupwa kapuni.
 
Brother you were the best at the university 2005/2008 tunakukubali sana kipindi kile unasoma Finance Udsm,umetoa nondo nzuri
 
Tumekuelewa sana mkuu na hata hiyo digirii yako ukiipata ni haki. Ila, ukirudi home, angalia sana usiajiriwe na sirikali hii unayotakiwa uiweke digiriii yako pembeni ujibu ka mlevi wa gongo.
Watu wanasema kiwanda flan kinafungwa kwa sababu hii, unasimama na kubisha kuwa sio kweli bali kinatengenezwa tu. Mwingine anaenda kuinua walevi huko na kuwavalisha makofia ya mainjinia na kuwauliza tu; Mmeona mali ghafi yetu. Wanajibu, ndiyoooo.
Kesho yake mnakubali kiwanda kile kimeshafungwa. Hata mtoe sababu gani, nani tena atakuamini kwani watu weshakuona kuwa mpiga dili??
Haya uliyo yasema, yangelielezwa tu kirahisi hivi ka ulivyo eleza, si watu wangelielewa?? Lakini mnasikia tu, Fedha ya serekali haina ruksa kuwekwa benki binafsi. No explanation, no what!! Ndo maana watu wanawaita wengine, madikteta. Kwa sababu, si wewe wa kuyatamka hayo. Waache uliowapa madaraka wayaseme. Jamani, msinielewe vibaya wakuu
 
Mtoa post umeandika mengi kwa utaalam kabisa. Nakubaliana na wewe kwamba sekta ya fedha nchini haina hali mbaya ya kutisha ila pia ni ukweli usiopingika kwamba kwa mwaka huu sekta ya fedha itapata matokeo mabaya kulinganishwa na mwaka uliopita. Na pia kumbuka kama umetumia interim results za mabenki ni kwamba hazipo audited, inabidi kusubiri final results ambazo zipo audited, kila benki inatakiwa kuzikamilisha by 31 March 2017.
 
Wana bodi,

Kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka vyanzo tofauti, nyingi zikipendekeza kuwa hali ya mabenki ni mbaya, ya kutia mashaka, na kuonesha dalili ya mabenki kufilisika. Nimeamua kuandika machache na kwa ufupi, kutokana na uchunguzi na tathmini ya kitaalamu. Sababu za kuandika ni mbili. Moja, kwa kuwa uchumi na hasa sekta ya fedha ni eneo langu la taaluma, na nitakuwa sitawatendei haki watanzania kama sitasema neno. Pili, mabenki na sekta ya fedha ni moyo wa uchumi. Midororo na misukosuko mingi katika historia ya chumi za dunia, mara nyingi huanzia katika sekta ya fedha. Naomba kusema kwa ufupi, kwa hoja tatu.

Hoja ya Kwanza: kumekuwa na tatizo ambalo ni la kawaida katika sekta ya fedha la kutolipa madeni wadaiwa. Benki nyingi, na hasa CRDB imekuwa na tatizo hilo. Kwa utaratibu wa kawaida, mabenki hukisia uwezekano wa kutolipwa na kuweka pembeni uwekezano huo (provision), na wakati mwingine kufanya juhudi za kuweka mikakati ya kuyakusanya (restructuring) kihasibu na kisera. Inaposhindikana, mabenki hutambua kuwa haitalipwa na kuweka kama gharama (expensing loans write offs). Hii hupunguza faida. Kwa CRDB imekuwa na athari kubwa, na pengine hutokea mabenki yakafanya hivi kwa pamoja au kwa namna ya msimu, na hivyo hili limetokea katika robo ya tatu ya mwaka 2016. Takwimu zinaonesha kuwa katika trilioni 16.7 zilizokopeshwa, kuna uwezekana wa trilioni 1.43 kutolipwa (non-performing loans) (asilimia 8.6). Kiwango hiki kwa Tanzania ni cha kawaida, tena cha chini kuliko nchi nyingi za kusini mwa Sahara ambazo viwango vyao hufika hadi asilimia zaidi ya 20.

Hoja ya Pili: Kulikuwa na kutoelewana kati ya mabenki na serikali kuhusu kodi ya mapato yatokanayo na mikopo ya benki. Mabenki mengine yalifungua kesi dhidi ya TRA. Lakini katika mwaka 2016 mfano, CRDB walishindwa kesi na hivyo wakatakiwa kulipa kodi hiyo, ambayo ilijumuisha pia kodi ya vipindi vya nyuma (retrospective). Benki nyingi ziliona matumaini ni machache, itawalazimu kulipa kodi hiyo ya serikali. Kwa hiyo muhula wa tatu wa mwaka 2016, mabenki mengi yakatambua kodi hiyo kama gharama. Na ndio maana faida katika mabenki mengi na sekta ilishuka kwa kasi sana, ukizingatia hoja ya kwanza na hoja hii ya pili.

Hoja ya Tatu: Wengi wamehusianisha hasara hii na tatizo la mtaji katika benki ya Twiga. Ukweli ni kuwa, uhusiano ni mdogo sana. Kilichotokea benki ya Twiga, ni kuwa wamekuwa na tatizo la mtaji kwa muda mrefu, wa karibu miaka kumi. Wakaomba serikali aliye mmiliki aongeze mtaji, hilo halikufanyika. Kwa sababu serikali ni mmiliki, benki ikaendelea kuendeshwa bila mtaji wa kutosha. Pamoja na tatizo la mikopo kwa kiasi fulani, hali ikawa mbaya hadi hapo Benki Kuu walipoamua kuchukua dhamana ya benki. Jambo jema linalokuja, ni kuwa wawekezaji binafsi wamekaribishwa kuingiza mtaji, na hadi ninapoandika, Mohammed Dewji na Exim Bank ya China wana nafasi kubwa ya kushinda tenda hiyo.

Nimesikitishwa na upotoshaji unaofanywa, tena na wataalamu. Wakizungumzia kuwa kuna ukasi wa mtitiriko wa fedha (liquidity) katika sekta ya fedha kutokana na serikali kutoa fedha zake na kuziweka benki kuu. Ukweli ni kuwa serikali ilitoa shilingi bilioni 515, wakati liquidity ya mabenki yote kwa takwimu za Disemba 2015, ni bilioni 9,004. Kiasi kilichotolewa ni asilimia 5.7 pekee ya ujazo wa fedha. Na fedha hizi mabenki yanaweza kuzikopa kutoka benki kuu. Kwa tathmini yangu, viashiria vyote ya msingi (fundamentals) vya sekta ya fedha kama mtaji, ujazo wa fedha, ubora wa dhamana, faida na ubora wa uongozi wa mabenki (CAMEL) vipo katika viwango vinavyokubalika (prudential limits). Na mwisho, tathmini yangu inaonesha kuwa mwisho wa mwaka 2016, robo ya nne, mabenki mengi na kwa ujumla wake, yatarekodi faida.

Genuine Martin (Economics PhD Candidate, Northern Illinois University, USA)
This is yet another theory...maelezo ya kwenye karatas mengi tu kama ya mafuru na wasomi wengine "wa kukariri"...tufanye nini?...tusaidie...mohamed wa bangladesh came up with brac idea...he won nobel prize..uplifted lives of not only banglas..but of many other african and asian countries..hiyo ndio faida ya mchumi na financier...kama huna msaada unaandika andika tu..hata hapa mliman we have a bunch of ur like..hiding under the "thin" forest of "academicians"...go do ur assignment and come with smthn nobler..
 
Too narrow brother...umeelezea Kama mwanasiasa uliyetumwa to clear atmosphere.. Economists huwa tunaelezea kwa data not blah blah... I was expecting unambie kati ya 2016 na miaka ya nyuma ratio ya non performing loans ni kiasi gani? To help for more than five years Crdb imerecord non performing loans kubwa 2016 kubwa kuliko miaka ya nyuma ndio maana bank ikasitisha mikopo... Na bank husitisha utoaji wa mikopo tu inapoona mikopo mingi Inakuwa ngumu to recover (bad debt) and this issue imeenda not only to Crdb but also NMB Postal bank..and to cut the story chanzo cha bad debts huwa ni kuporomoka kwa uchumi kwa wananch au bank kutokuwa makini kwa akina nani wakuwapa mikopo which hili always haliwezi kuwa tatizo. etc
Umezungumzia issue ya twiga bank.. Can you kindly explain ni kiasi gani bank inatakiwa iwe nacho kama minimum mtaji na ni when bank ili fall out of minimum balance as capital? Usiniambie serikali sijui iliacha ijiendeshe bila mtaji kwa sababu wao ndio wamiliki.. Unajua Maana ya required ratio? B. O. T could not allow such thing.. Hili tatizo la twiga ni 2016
Umeandika Bla Bla Bla Kama majibu wanayotoa akina Mwi...mpaka uvivu kukujibu
ka mkubwa we wa moto...
 
Mkuu nina wasiwasi na phd yako
Kwenye hoja ya kwanza unakiri kabisa ni watu kushindwa kulipa madeni yao ktk mabenki-hv phd candidate unayesomea mamb ya fedha unashindwa relate uhusiano huu wa kushinwa kwa wateja wengi kurejesha mikopo na uchumi wa nchi????? Kama miaka ya fedha 2 iliyopita watu waliweza kurejesha why jn this financial year??
Kwenye hoja ya pili-kama mabenki yalishindwa kesi na yakalazimika kilipa kodi hiyo inayotokana na mikopo-na kutokana ulivyooandika unamanisha walitoa kodi hiyo kwa mkupuo-sasa serikali kupitia wizara ya fedha na benk kuu walikuwa wapi kujua kawa hatua hiyo inaweza kusababisha hali mbaya ya kiuchumi na badala yake wangefanya au kuweka utaratibu mzuri ili mabenki yalipe kodi hiyo kwa awamu ili kuepusha mdororo wa uchumi????
Hoja ya tatu ndio umechochora kabisa unasema kuanguka kwa twiga benk ni kutokana na serikali kutoongeza mtaji katika benk hiyo-naomba nikuulize kwani twiga walikuwa wanapanua biashara mpaka waongezewe mtaji???? Kama benk ingekuwa inafanya vizuri maana yake mtaji ungeongezeka automatically.watejwa kushindwa kurejesha mikopo ndani ya benk hiyo na twiga kuomba mtaji tena ni dalili mbaya kiuchumi
Naomba nijibu paragraph yako ya kwanza, haya mabenki kwa miaka kadhaa wamekuwa na hiyo mikopo isiyo lipika ika walikuwa wakifumbia macho kwa sababu hamna mtu alikuwa akifuatilia, nakumbuka humu jf palikuwa na thread kuhusu mikopo mibovu ya crdb na nbc hata kabla Kikwete hajamaliza muda wake, kwa mfuatiliaji mzuri wa hoja atakuwa alisoma, lakini pia siku ike JPM aliposhtukiza BOT aliliongelea hilo la usimamizi wa mabank kwa sababu ni kazi ya BOT na hawakuwa wakifanya kwa uadilifu unaotakiwa.
Sasa JPM alichofanya ni kuwataka BOT watekeleze majukumu yao na ndio maana huo udhaifu ukaonekana sasa.
 
Back
Top Bottom