Ukweli kuhusu Forex na IML

Solotov

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
263
295
Hivi karibuni kumekuwa na muamko wa watanzania kutaka kujua kuhusu biashara ya Forex.Aidha kumekua na madarasa kadhaa yakitoa elimu hiyo kwa vijana wa kitanzania na kwa bahati nzuri na mimi sikuwa nyuma sana kutaka kufahamu kuhusu Forex, hivyo nilifanya jitiahada binafsi kung'amua mawili matatu kuhusu biashara hiyo.

Wiki mbili zilizopita nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu akiniambia kuna fursa ya biashara anataka kunishirikisha na kuniomba nifike kwenye presentation inayoelezea namna ya kufanya hiyo biashara.Alinielekeza sehemu ulipo ukumbi ambapo presentation inafanyika, na mimi bila hiyana nikafika kuskiliza

Kwanza tulianza kwa kuelekezwa machache kuhusu forex na namna inavyofanywa ili uweze kunufaika
Mwisho tukaelezwa kuhusu IML[international market live] na muanzilishi wake CHRISTOPHER TERRY.Na kuombwa kujiunga na IML ili tuweze kutrade kwa kufuata mafunzo yanayotolewa na IML na gharama ya kujiunga nao ni USD 195 sawa na TSH 439,256.ambapo utaweza kupata mafunzo yanayotolewa na IML na ukitaka kutrade unaweka USD 200 sawa na TSH 450,519 kisha wanakusaidia kutrade wao mpaka utakapojua vizuri kutrade peke yako.

Kingine ni kwamba kuna kufanya networking ambapo ukishirikisha watu kujiunga na IML utapata commision, mfano umeshirikisha watu watano utalipwa USD 150 na kiwango kitaongezeka kadri ya watu ulionao.

KWA ANAYEFAHAMU UKWELI KUHUSU KINACHOITWA IML NA FOREX ANIFAHAMISHE KAMA KUNA UKWELI NA WANACHOKIFANYA.ASANTENI
 
Nyakati hizi watu wako desparate ndizo nyakati za matapeli kuvuna. Binafsi siamini tajiri anayejidai anamfundisha masikini kuwa tajiri. Huu ni mtego kwako lakini kwao wanavuna mipesa mingi sana.

Ukiona mtu anamlisha ng'ombe ujue yuko karibu kumchinja au kumuuza. Ukiambiwa ukileta wateja tutakupa commission ujue huo ni mradi wa wajanja, hizo pyramid ndiyo mitaji yao. Tajiri ana mfunza masikini njia za kuwa tajiri?!

Hahaha hapo ndio wananipa wasiwasi hao watu, wamekua na roho nzuri ghafla. Kwanini wasigawe huo utajiri mkuubwa kama kweli wanatupenda. Lakini wao wanamnenepesha mbuzi kwa faida yao wamle nyama au wamuuze ghali.

Kumbuka UPATU, wakaja DECI, kuna ponzi scheme nyingi sana, nakushauri achana nazo.

Dunia hii shida, matatizo, na umasikini havitaisha. Usidanganywe kwasababu unashida ukadhani wao ndio muharobaini wa shida zako. Usidanganywe na mafanikio hewa, utaonyeshwa mafanikio kibao lakini tumia akili yako vizuri.

Usije ukawa kama wale wanaonunua kanga kariakoo, break ya kwanza kwa mchungaji akaibariki, mchungaji anapewa pesa kuibariki kanga. Halafu kanga haidumu pia.

Ushauri wangu fanya shughuli zako za halali, ila kama nawe ni mmoja wao basi ongeza bidii kutafuta wateja.
 
Hiyo IML ni uongo mtupu usiingie hapo, kuna jamaa mmoja hvi anajiita PROPHET ni mwizi sana hua anakuja morogoro kutoa semina ya forex ametuingiza mitini na mbali na hapo aka trade akaunti zetu na kuziunguza. PROPHET shame on you
 
Nyakati hizi watu wako desparate ndizo nyakati za matapeli kuvuna. Binafsi siamini tajiri anayejidai anamfundisha masikini kuwa tajiri. Huu ni mtego kwako lakini kwao wanavuna mipesa mingi sana.
Ukiona mtu anamlisha ng'ombe ujue yuko karibu kumchinja au kumuuza. Ukiambiwa ukileta wateja tutakupa commission ujue huo ni mradi wa wajanja, hizo pyramid ndiyo mitaji yao. Tajiri ana mfunza masikini njia za kuwa tajiri?! Hahaha hapo ndio wananipa wasiwasi hao watu, wamekua na roho nzuri ghafla. Kwanini wasigawe huo utajiri mkuubwa kama kweli wanatupenda. Lakini wao wanamnenepesha mbuzi kwa faida yao wamle nyama au wamuuze ghali.

shukrani mkuu, nimekuelewa vizuri
 
Hiyo IML ni uongo mtupu usiingie hapo, kuna jamaa mmoja hvi anajiita PROPHET ni mwizi sana hua anakuja morogoro kutoa semina ya forex ametuingiza mitini na mbali na hapo aka trade akaunti zetu na kuziunguza. PROPHET shame on you
Ndio huyo huyo, pole sana mkuu na asante kwa kunifumbua macho
 
Hiyo IML ni uongo mtupu usiingie hapo, kuna jamaa mmoja hvi anajiita PROPHET ni mwizi sana hua anakuja morogoro kutoa semina ya forex ametuingiza mitini na mbali na hapo aka trade akaunti zetu na kuziunguza. PROPHET shame on you
Hahaha ma Prophet hadi huko kwenye miphorex?! Kweli Yesu karibia afike duniani. Huwa mnapewa pombe, au mnavutishwa bangi?! Mbona hawa watu nyie mnawaelewa vizuri na kwa urahisi sana?! Mi huwa siwaelewi kabisaaaa, na nisipoelewa sotoi hata thumni.
 
Mnatuchosha kurudia hii sentensi kila siku. "Tuache kupenda vitonga, tufanye kazi halali za uzalishaji mali/huduma".
Sikuzote napenda kusema kwamba....
Hakuna mafanikio yenye yanakuja kiulaini, napenda kusisitiza tufanye kazi ndipo tutafanikiwa.
"Na ukiona unaitwa kwenye fursa, basi ujue wewe ndio fursa yenyewe"
 
Nyakati hizi watu wako desparate ndizo nyakati za matapeli kuvuna. Binafsi siamini tajiri anayejidai anamfundisha masikini kuwa tajiri. Huu ni mtego kwako lakini kwao wanavuna mipesa mingi sana.
Ukiona mtu anamlisha ng'ombe ujue yuko karibu kumchinja au kumuuza. Ukiambiwa ukileta wateja tutakupa commission ujue huo ni mradi wa wajanja, hizo pyramid ndiyo mitaji yao. Tajiri ana mfunza masikini njia za kuwa tajiri?! Hahaha hapo ndio wananipa wasiwasi hao watu, wamekua na roho nzuri ghafla. Kwanini wasigawe huo utajiri mkuubwa kama kweli wanatupenda. Lakini wao wanamnenepesha mbuzi kwa faida yao wamle nyama au wamuuze ghali.
Kumbuka UPATU, wakaja DECI, kuna ponzi scheme nyingi sana, nakushauri achana nazo.
Dunia hii shida, matatizo, na umasikini havitaisha. Usidanganywe kwasababu unashida ukadhani wao ndio muharobaini wa shida zako. Usidanganywe na mafanikio hewa, utaonyeshwa mafanikio kibao lakini tumia akili yako vizuri.
Usije ukawa kama wale wanaonunua kanga kariakoo, break ya kwanza kwa mchungaji akaibariki, mchungaji anapewa pesa kuibariki kanga. Halafu kanga haidumu pia.
Ushauri wangu fanya shughuli zako za halali, ila kama nawe ni mmoja wao basi ongeza bidii kutafuta wateja.
Thread closed. Kama mtu atakua bado hajaelewa huyo atakua ni kada wa network marketing na hizo schemes
 
Back
Top Bottom