Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,962
Chagulaga ni neno la kisukuma lenye maana ya chagua.
Hatuwengi sana wamekuwa hawaelewi nini hasa maana ya hii tamaduni. Naomba japo kidogo niwaeleze ukweli wa jambo hili.
Kwa wale ambao hamjawahi kusikia kuhusu kitu hiki basi mnaweza kujifunza japo kidogo kuhusu tamaduni zilizo kuwa zikifanyika.
Kwanza kabisa chagulaga ni kitendo cha mwanaume au wanaume kufuata binti mmoja na kumwambia chagulaga. Basi kama huyo dada atakuwa amempenda kijana atamshika mkono na kuondoka nae. Basi kama kuna vijana wengine watamwacha huyo binti na ataambatana na yule aliye mchagua.
Baada ya hapo kijana wa kiume ataanza kutupa point zake kwa huyo binti. Ikiwa huyo binti atakubali basi watakuwa wamekubaliana lakini akikataa basi huyo mwanaume atakuwa hana jinsi.
Kumbuka huyo binti huenda anawazazi au ndugu zake huwezi ukafanya kitu chochote bila ya ridhaa ya huyo dada. Na ukifanya hivyo basi utakuwa umemuaibisha huyo dada na unaweza kuchukuliwa hatua.
Kunawatu wengi wametokea wakilaumu kuhusu chagulaga na kusema ni ukatiri dhidi ya wanawake lakini mimi hapa ninasema la hasha si hivyo hawajui maana halisi ya chagulaga. Na wale wanaofanya tofauti walikuwa wanachukuliwa hatua kama wabakaji.
Kumbuka mwanamke akiwa bikira ilikuwa ni heshima kubwa sana kwake na kwa wazazi wake. kwahiyo wasichana wa kisukuma walijichunga sana na kutunza bikira zao. Na kama chagulaga ingekuwa holela holela kwahiyo mabinti wengi wangekuwa sio bikira.
Vilevile wazazi walipenda sana kama binti yao anafuatwa na wanaume wengi kumwambia chagulaga. Msichana akitoka kwenye ngoma mzazi wa kike alidiliki kumuuliza kuwa alifuatwa na wanaume wangapi.
Na kama binti anakuwa hafuatwi na mwanaume yeyote walijua binti yao nyota yake imechafuka, iliwabidi wazazi au ndugu waioshe nyota yake.
Na baada ya kuiosha nyota yake huwaka na kung`aa na ndipo vijana wengi wa kiume humfuata na kumwambia chagulaga.
Kama kuna mtu mwingine hapa JF anajua zaidi au anacomment karibu.