Ukweli kuhusu biashara ya Forex

Malcom_X

Member
Mar 23, 2017
20
49
Habari ya wakati huu wanajamvi!
Leo nimeona vema niwaletee mezani mada hii.

Katika harakati za kupambana na Maisha kama kijana pia mwenye kiu ya kufanikiwa nilikutana na jamaa mmoja mwenye USHAWISHI wa hali ya juu hapa JF

baada ya kusoma Nyuzi zake kali zilizoteka hisia za vijana wengi, Nilivutiwa sana na Moja ya UZI wake maridadi uliokua umezungumzia vizuri kuhusu biashara ya kubadili fedha za kigeni (FOREX).

Jamaa alifanikiwa kunishawishi kuhudhuria mafunzo ya Forex aliokua akiyatoa yeye na wenzake kutoka Nchi fulani ambao walidai kua Biashara hii ndio imewafanikisha wao na wanaimudu kwa kiwango cha juu yani kimombo tunaita Professional Traders.

Nilihudhuria Training yao baada ya kulipa kiasi fulani cha pesa na kulikua na bra bra nyingi za mafanikio ambazo zilipelekea wadau wengi kuhisi Maisha si ndo haya binafsi niliona kama nimeshatusua niliona kama ndo naelekea kuachana na kimbute changu Starlet Glanza nachukua mzigo wa BMW X6 Mapema bila msoto wa kupambana na Mr Employer.

Basi nikapata mafunzo vizuri na kupractise vizuri nikaona naweza mudu business nkaendelea na kazi, Lakini nilichokuja kukifahamu zaidi ni kwamba FOREX ni kama biashara zingine HAKUNA PESA ZA BURE FOREX, ni lazima uwekeze vizuri akili na pesa zako na kufanya analysis nzuri ya soko ndipo utasonga mbele, kiasi kikubwa cha walimu wengi wa Forex sio Traders ni wababaishaji waoga wa Kutrade Mafanikio yao ni Pesa yako wewe unafundishwa sio Kutrade Forex . Kua Makini Forex ni Rahisi kujifunza tafuta vitabu invest muda wako katika kujifunza Mambo yataenda achana na Walimu Feki Utapigwa pesa na usije irudisha.
 
Hakuna cha burebure mkuu...
Hata kama ulichangia pesa kwa kwa hayo mafunzo lakini faida si umepata na unaendelea kupata.

Vitabu vinapatikana wapi mkuu
 
Vitabu vinapatikana wapi mkuu
#1. Kuna mamia ya vitabu vya forex hapa: Traders Library
- Kwanza download telegram na weka kwenye simu yako / pc, Jisajiri
- Ndipo rejea kwenye hiyo link na telegram itafunguka

#2. {a} Inatakiwa uwe na trading stratergy uliyo ichagua, then soma vitabu vyake kuhusu hiyo stratergy, Sio kila kitabu cha forex kitakufaa.
{b} Soma zaidi vitabu vya trading psychology
 
Back
Top Bottom