Ukweli kuhusu ajali ya Majinja express iliyoua watu 43 mafinga huu hapa

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
456
[h=3]Soma kwa umakini halafu useme chanzo cha ajali ni nini. Mimi binafsi naona hata kama barabara ilikuwa mbaya lakini dereva wa basi alichangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuendesha gari mwendo kasi na kuwajibu abiria vibaya pale walipomuonya kuhusu mwendo kasi.[/h]Habari kamili inapatikana kwenye website MAPYA AJALI ILIYOUA 42 IRINGA LEO ,DC MUFINDI AANZA KWA MKOSI - Mzee wa matukio daima (matukiodaima.co.tz)




Hili ndilo eneo la ajali

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas (kulia ) akimtazama mmoja kati ya majeruhi 22 waliolazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambao walipata ajali mbaya baada ya basi la majinja lenye namba za usajili T348 CDE kugongana na lori na kufunikwa na kontena lake jana eneo la Changalawe nje kidogo ya mji wa Mafinga ,katika ajali hiyo watu 42 walifariki dunia
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili kulia akiwa na viongozi mbali mbali wa tatu ni kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi , akifuatiwa na mwenyekiti wakamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas na mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita jana walipofika eneo la ajali iliyoua 42 na kujeruhi 22

basi likiwa limefunikwa na kontena la Lori

Hili ndilo shimo chanzo cha ajali
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo
Miili zaidi ikiondolewa eneo la tukio

* Mtoto wa miaka 3 akutwa hai wazazi wake wafa



* DC mpya Mufindi ndio ilikuwa siku yake ya kwanza kuanza kazi


*Madereva walikuwa wakigombea kupita eneo katikati kukwepa mashimo
* Basi lilijaza abiria 64


* Wajeshi wavunja simu shuhuda wa ajali
* RC na kamati ya ulinzi na usalama yazingirwa na wananchi




Na Francis Godwin BLOG Iringa


MAAJABU na kweli moto wa miaka 3 asalimika kwa kutokuwa na mchubuko wowote baada ya ajali basi la kampuni ya majinja lenye namba za usajili T 438 CDE aina ya Scania lililoua watu 42 na kujeruhi 22 kufuatia basi hilo kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam ugongana uso kwa Uso na Lori na kufunikwa na kontena la lori hilo.


Katika ajali hiyo imeelezwa kuwa mtoto huyo ambae jina lake halijafahamika alikuwa akisafiri na wazazi wake wote wawili kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam na baada ya ajali hiyo mtoto huyo alichomoka katika mikono ya mzazi wake na kukutwa chini ya siti nyuma na basi hilo ambako hakukuharibika kabisa.


Mmoja kati ya abiria wa ajali hiyo Lucy Mtanga ameueleza mtandao huu wa Mzee wa matukio daima kuwa mtoto huyo alikuwa amekaa siti za mbele kama siti ya tatu kutoka kwa Dereva pamoja na wazazi wake na cha ajabu baada ya ajali hiyo mtoto huyo alikutwa chini ya siti ya mwisho kabisa mwa basi hilo akiwa ametulia.

Katika ajali hiyo iliyotokea leo Majira ya saa 4 asubuhi eneo la Changalawe nje kidogo ya Mjini wa mafinga wilaya ya Mufindi mkoani hapa katika barabara kuu ya Iringa - Mbeya abiria wake waliopoteza maisha walisagika vibaya kichwani na wengi wao miguu kuvunjika vunjika huku sura zao zikishindwa kutambulika .



Imeelezwa pia katika basi hilo kulikuwa na baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari Sangu mkoani Mbeya akiwemo ndugu wa Mwanahabari na meneja wa gazeti la Mtanzania mkoani Iringa Marcy Mwalusamba kijana Omega Mwakasege aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Sangu ambae alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi ..

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa jumla ya watu 41 walikufa eneo la tukio na mmoja alifia hospitali ya wilaya ya Mufindi na mmoja kufariki akiwa anapatiwa matibabu hospitalini hapo.

Pia alisema watu 22 akiwemo Mtoto wa miaka mitatu wamejeruhiwa vibaya huku zaidi ya 10 hali zao ni mbaya zaidi.

Mkuu huyo wa Mkoa pia aliagiza maiti 32 kupelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Baada ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya wilaya ya Mufindi kutokuwa na uwezo wa kuhifadhi miili zaidi ya 8.



Wakati mkuu wa mkoa wa Iringa akitaka chanzo cha ajali hiyo kuchungwa zaidi baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wameibuka na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na mashimo makubwa yaliyokuwepo Eneo hilo.

JOsamu Obedi alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo mkali toka anatoka Eneo la Uyole Mbeya na kufanikiwa kuyapita mabasi zaidi matano yaliyokuwa yameondoka stendi ya Mbeya mjini saa 12: 00 asubuhi .

Hata hivyo Kabla ya kufika Eneo la ajali zaidi ya mara tatu abiria walimuonya kupunguza mwendo japo hakusikiliza zaidi ya kuwakejeli kuwa yeye ni zaidi ya dereva hivyo wasimfundishe kazi.

Pia alisema kuwa basi hilo hilijaza abiria na baadhi yao kukaa nyuma ya dereva kwa kutandikiwa godoro na kuwa mwendo kweli ulikuwa mkali zaidi na ndio maana uwezekano wa kukwepa mashimo ulikuwa mdogo hivyo kusababisha ajali hiyo .

Alisema Baada ya kufika eneo hilo lenye mashimo makubwa barabarani kushoto na kulia lori lilitaka kupita katikati na basi pia lilitaka kupita ebeo hilo ndipo yalipokutana uso kwa uso.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Iringa Salim Asas akizungumza Eneo la tukio mbali ya kuwapa pole ndugu wote waliopoteza Maisha ,alisema kuwa ajali hiyo ni kubwa kwa Mkoa wa Iringa na haijapata kutokea ajali Kama hiyo toka ameingia mwaka 2008 hajapata kushuhudia ajali mbaya Kama hiyo.

Alisema kuwa Mkoa wa Iringa umekuwa ukisifika kwa kutokuwa na ajali mbaya na kuwa mwaka Jana umepewa tuzo ya kitaifa ya kuongoza bila ajali kubwa.

Hivyo alisema kwa tukio hili kuna haja ya kujitathimini na kuangalia sababu ya ajali hiyo ambayo wapo wanaosema ni mashimo barabarani na wapo wanaosema mwendokasi wa madereva.

Alisema eneo hili lina mteremko mkali na mlima na kuwa lori lilikuwa likishuka na basi lilikuwa linajiandaa kupanda mlima baada ya kushuka mteremko kwa kasi .

Hivyo alisema iwapo sababu kubwa ni mashimo basi wahusika kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo huku akiwataka madereva pia kuwa makini zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mbaya na kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.

Kuhusu hali za madereva kamanda Mungi alisema hana uhakika Kama wamepona ama wamekufa kutokana na miili yao kuharibika zaidi na wapo ambao ni mahututi .



Wakati ajali hiyo ya kihistoria ikitokea mkoani Iringa katika wilaya ya Mufindi taarifa kutoka katika wilaya hiyo zinadai kuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita ndio ilikuwa ni siku yake ya kwanza ya kuanza kazi rasmi katika wilaya hiyo baada ya kuapishwa na kurudi kwao kuchukua mizigo yake.


Mkuu huyo wa wilaya ambae hakutaka kuzungumza chochote na wanahabari alionekana ni mwenye mawazo na asiyejua nini cha kufanya kufuatia tukio hilo pamoja na kuvaa gropsi mikononi kwa ajili ya kusaidia kupakia majeruhi na maiti ila hakuweza kufanya hivyo


Wakati huo huo wananchi wenye hasira kali walishindwa kujizuia kumtolea lugha kali na kumzonga mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na .kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wakilalamikia mashimo hayo kuwa ajali hiyo ni uzembe wa serikali kupitia TANROADS kutokana na mara kwa mara madereva kulalamikia mashimo hayo kwa zaidi ya mwaka sasa bila kutengenezwa .


Mbali ya tukio hilo kijana mmoja ambae jina lake halikufahamika mara moja alinusurika kichapo na kuishia kuvunjiwa simu yake aina ya Nokia kutoka kwa wanajeshi wa JKT Mafinga ambao walifika kusaidia ulinzi na uokoaji eneo hilo kwa kile walichoeleza ni kumpiga picha mmoja kati ya wanajeshi hao wakati akimthibiti kibaka aliyekuwa akitaka kupora mali za marehemu bila ridhaa yake.



































 
Back
Top Bottom