Ukweli hauna mwisho (truth is infinity)

Ukweli hauna mwisho (truth is infinity)

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,963
Nawasalimia wote kwa pamoja wana JF.

Mda mrefu tumekuwa na shughuli za uchaguzi, sasa uchaguzi umeisha kwa asilimia kubwa.

Ni mwendelezo wa mada zangu zinazohusu elimu ya kiroho.Kwa utangulizi ni kwamba leo nitaongelea kuhusu "Ukweli". Mambo tunayoishi, kuamini na kufuata utaratibu fulani ni makubaliano yetu sisi wanadamu lakini siyo lazima yawe ndio ukweli. Kuna makubaliano yanayoendana na jamii fulani lakini yanaweza yakawa tofauti na makunaliano ya jamii nyingine.

Kwa mfano katika makubaliano ya jamii tunazoishi ni kwamba kunarangi na kila rangi imepewa jina lake(Nyekundu, Nyeusi nk). Mtu akiona rangi nyekundu atakubali kwenye akili yake ile ni rangi nyekundu. Lakini si kila kila mmoja anajua kuwa kweli hiyo ni rangi nyekundu,

Kwa utangulizi huo nadhani kuna wazo fulani limekuja kichwani kwako. Ngonja niendelee kwa kuongezea kitu hiki hapa. Milango yetu ya fahamu ni njia inayotumika kurekodi matukio mbali mbali kila siku na kuyaweka kwenye akili zetu.

Matukio yanavyozidi kuwa mengi na mengi kwenye akili mtu anajitengenezea ulimwengu ambao unaitwa virtual World ambao upo kwenye akili yake.

Huo ulimwengu wakuwaza yeye ni fulani, anauwezo fulani, anamzidi fulani, ananguvu nk. Mtu akiwa katika ulimwengu huo anakuwa kipofu anakuwa anafuatilia mambo ambayo sio uhalisia.

Tangu binadamu akiwa mtoto amekuwa akiingiza vitu vingi sana katika akili yake. Vitu ambavyo asilimia kubwa vimetungwa na hatimaye anatengeneza ulimwengu ambao sio halisia anaishi katika illusion world.

Watu asilimia nyingi sana duniani tunaishi katika virtual World. Ulimwengu huo unatufanya tuwa na stress, kuuana, kuwa na imani flani flani, Kuogopa nk.

Asili yetu sisi ni emptiness. Vitu vinavyoonekana vyote asili yake ni emptiness. Baadae vyote vitarudi kwenye emptness.

Lakini emptness sio empty ni energy ambayo inatokana na atoms. Kadri siku zinavyo enda mbele na binadamu anapoamua kuanza kutoka kwenye virtual world anaanza safari kuanza kuutafuta ukweli.

Kama nilivyosema kwenye kichwa cha hii thread the truth is infinity. Hautakaa ukaupata ukweli wote tunavyozidi kufanya meditation tuna jua vitu na kuelewa hatua kwa hatua. Lakini haitafika sasa tumeshaujua ukweli wote.

Steve Job ni mmoja ya watu waliokuwa wanafanya meditation na kampuni ya Apple mpaka sasa wafanyakazi wake wapo na sessions the meditation. Sumsung pia na yenyewe ina session hizo.

Ukweli hauna mwisho.

Karibuni tuweze kujadili.
 
Kusema ukweli, sijaelewa. Hili swali likija kwenye mtihani, nitaliruka tu.
 
Je unakumbuka maisha yako ukiwa na miaka 10 hadi 20? je unaweza kuyawaza kichwani na kuona ulivyokuwa unafanya?. Unaweza ukaona kwenye akili zako namna gani ulivyokuwa unafanya shuleni? Hapo ulipo je unaweza ukaona ndani ya chumba chako kila kitu kilivyo?. That is a virtual World people we live.
 
Kuna kitu unamaanisha, kizuri ila ngoja ni refresh akili ili niweze kuelewa vizuri
 
Mkuu haya madini nimeelewa kidogo ...endelea kufafanua mkuu.
 
Nenda staright kwenye point bana ...unataka tufanyaje? Tumuabudu Sakhamuna Budha?
 
Back
Top Bottom