shungurui
JF-Expert Member
- Sep 1, 2008
- 3,765
- 5,153
Kuna mambo mengi yamekuwa yakitajwa kuwa ndio yamepelekea kuvunjika kwa AZIMIO LA ARUSHA.Lakini haya hapa ndio ukweli wenyewe.
1.HAKUKUWA NA UKWELI KATIKA BAADHI YA MISINGI YAKE
Mfano Binadamu wote ni sawa kama ni kweli yalitoka wapi maneno zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM na kwanini basi Raisi wa nchi yetu hawezi kushitakiwa hata kama kafanya makosa yaliyo wazi kabisa.
Kumbuka Raisi ni Mwenyekiti wa CCM! Hata chama hakiwezi kumwajibisha
Kama kweli Nyerere alikuwa anamaanisha hivyo, yeye kipindi hicho kama Mwenyekiti na Raisi mbona hakutoa mwanya kwa wenye nafasi hizo (yaani Mwenyekiti na Raisi)wawajibishwe wanapokwenda kinyume na misingi hiyo ya kiazimio la Arusha, au yeye hakuwa Banadamu kipindi kile na amekuwa Binadamu baada ya kuuacha uraisi na uenyekiti.
Ndio maana wengine wanasema hili Azimio la Arusha lilikufa kabla halijaanza.(nimenukuu).
2.LILIKUWA NI AZIMIO LA NYERERE
Hivi ni nani alishilikishwa kuunda hili Azimio ? ni wanachama wa CCM au mwananchi?
MIMI naamini hakuna ambaye aliyeshilikishwa kati ya mwananchi au mwanachama wa CCM. kama alidiliki kuunda katiba ya nchi yeye mwenywe
Why ashindwe Azimio la Arusha?(Yaliyofanyika ni kiinimacho tu, si unajua zidumu fikra za Mwenyekiti ).yaani bora kama lingekuwa limeundwa na wananchi wa Arusha kidogo kungekuwa na uafadhari.Yaani halikuwa hata ni azimio la chama cha mapinduzi
Pia ndio maana hakulifanya Azimio liwe na nguvu ya kisheria,that's why likafa kilahisi (natural death)
Huo ndio ukweli wenyewe,ndio maana hata siasa ya ujamaa na kujitegemea nayo ikafa, Hivyi ni lini sisi wenye nchi tulikaa tukaamua kuwa tuwe na siasa ya ujamaa na kujitegemea au sera ya vijiji ya kuwatoa wananchi na kuwarundika sehemu moja hivi hakuna hata mmoja aliyekuwa na vision kuwa vijiji vitakuja na kuwa miji?inawezakana walikuwepo ila waliogopa kumwambia si unajua tena zidumu fikra za mwenyekiti.
Bila shaka kuna wale ambao hawaamini kama dar es salaam ilianza kama kijiji.
Ndugu zangu nawaomba tupoteze muda wetu mwingi katika kujadili na hatimaye kuunda katiba yetu sisi wananchi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA