Ukuta utazuia raia kujenga holela kwenye eneo la machimbo ila si kuzuia wezi wa madini maana hawatokei porini

Kwenye mikataba mambo yashakuwa sawa sasa. Hili la ukututa ndio ulikuwa mwanya wa mwisho
Airport na bandarini hakuna ukuta?? Je waliwezaje kutorosh Tanzanite miaka yote kma ukuta upo na kuna mashine za kukagua na mapolisi kibao??
 
Kwa kweli watz wengi sana mnauwezo mdogo wa kufikiri...ukuta hauna faida zenye tija kwani mtu anaweza kusimika nyenzo za uchimbaji hata kilomita moja kutoka kwenye huo ukuta na bado madini akayafaidi vizuri. Ni swala la kuchimba chini kwa chini kufwata madini yalipo nyie mtabakia kulinda juu wenzenu chini wanajichimbia madini wapendavyo. Madini sio maembe kusema unajenga ukuta watu wasije kuyachuma....
Asanteee kula gwala

Ova
 
Tunaanza
Mwizi wa madini ya Tanzania ni nani na huputia wapi?

Mwizi wa madini ya Tanzania ni yule ambaye anasaini mikataba ofisini kinyume na maadili na taratibu zilizowekwa juu ya uchimbaji na uuzwaji wa madini.

Mwizi wa madini ni yule anayesafiri mpaka nchi wanazonunua au kwenye masoko ya madini na kufanya udalali wa madini yetu ama kuyauza kwa bei ya chini na kupata ten percent au kuyauza yote bila kuleta hata mia kwenye nchi yake.

Mwizi wa madini ni yule anayekaa katika baraza au kikao cha kutunga sheria lege lege ili zimlinde wakati wa kuyatorosha.

Nani hasa amewahi kuwa mwizi wa madini?

Yeyote yule aliyepitisha mkataba wa kuuza madini au kuleta wawekezaji bila kufuata utaratibu hata kama amekuwa waziri hata ikitokea akashika wadhifa wa juu kabisa wa nchi bado ni mwizi.

JE WEZI HAO HUPITIA KULIKO JENGWA UKUTA?

Tujue madini siyo kokoto, madini siyo mahindi, madini siyo, mchanga, madini siyo maharagwe, madini siyo maji, kusema wanaoiba wanatembea kwa mguu wananyatia hapana , wezi wa madini ni Mawaziri , wanasheria, makatibu wa wizara nyeti za madini, wawekezaji wanaoshirikiana na madalali.

Swali dogo tu;

Hivi waliokuwa wanatuibia dhahabu zinapita porini? Yaani Accacia, Liganga, Meremeta wote hao wamepita porini?

Leo hii tunashangulia tu kwamba ukuta umejengwa tena na kusema utapunguza wizi wa madini? Aisee Tanzania ni nchi ya ajabu ulimwenguni, ni ajabu la Tisa.

CHAIN YA WIZI WA.MADINI IKO HIVI;

1.Dalali
Anatokea dalali anatumwa na mabwenyenye kwamba nataka madini Tanzania na nakulipa kiasi fulani na anatoa masharti, yaani bepari anatoa masharti kabisa ya bei, kiwango na uchenjuaji.

2. Dalali anawasaka viongozi wa Serikali na wakuu wa sekta husika kwamba kuna dili hili alafu wanajadili wanagawana vipi.

3. Wanafuatwa viongozi wenye ushawishi ndani ya bunge la wengi CCM wanakubaliana kwamba tupitishe mswada fulani h sheria fulani, inapita wanapata ten percent.

4. Anaitwa mkuu wa kitengo cha ulinzi kuwapa ulinzi katika operation hizo zote na idara nyeti.

5. Wakuu wa sehemu za uchimbaji nao wanahusishwa.

6. Maafisa wa usalama wa barababrani wakemia mpaka maafisa wa uwanja wa ndege wa ukaguzi.

Alafu madini yanatoroka.

Nauliza hapo kuna atakayezuiwa na ukuta?

Sibezi juhudi za Rais ila suala la UKUTA litasaidia wananchi wasijenge holela kwenye machimbo ila si kuzuia wezi wa madini.

Pia hela iliyotumika ingefanya mengine.
Mkuu umesema ukweli mtupu.

Nukuu haya maneno yangu..

"1. Ukuta utazuia utoroshaji wa madini lakini wizi wa Tanzanite utabaki pale pale."
"2. Unaweza ukazuia utoroshaji wa madini lakini thamani kwa jamii ndiyo haitaonekana"
 
Mkuu umesema ukweli mtupu.

Nukuu haya maneno yangu..

"1. Ukuta utazuia utoroshaji wa madini lakini wizi wa Tanzanite utabaki pale pale."
"2. Unaweza ukazuia utoroshaji wa madini lakini thamani kwa jamii ndiyo haitaonekana"
Hakika
 
Je airport wanavyopitisha kimagendo nako hakuna ukuta?? Makinikia bandarini kulikuwa hakuna ukuta wala wakaguzi?? Tuacheni siasa mngeongeza wataalam wa ukaguzi basi ingetosha kuliko kujenga ukuta as if walinzi wakihongwa hawawezi toroshea hata kutumia magari yao ya patrol!!!
Neno langu sio sheria
 
Airport na bandarini hakuna ukuta?? Je waliwezaje kutorosh Tanzanite miaka yote kma ukuta upo na kuna mashine za kukagua na mapolisi kibao??
Mkuu kwa mimi niliyeishi kule Arusha. Huu ukuta utapunguza tu vipato kwa wana apollo wale ambao huwa wanapata vi mia mia vya mboga za familia.
Kiufupi Magu kawaongezea umaskini watanzania walio walalahoi.
Bahati mbaya kuna watu wanafikiri kuna faida ya li ukuta hilo..
Yani nchi imepata kiongozi wa ajabu na amejipa washangiliaji ambao hata tukishauri vizuri hatusikiki na tunaishia kuhojiwa uraia..

Tutachelewa sana...
 
Tunapigwa kwenye mikataba na sheria za madini na siyo kwenye ukuta

Hadi Leo hii mikataba ya rasilimali ya nchi hii ni siri wanaojua ni viongozi wakuu wa nchi na hata bunge halina mikataba hiyo

Siku tukijitambua kama taifa ndipo tutaacha kushangilia vitu vidogo vidogo kama ukuta na kujikita kwenye msingi wa tatizo
Hakika
 
Una takwimu kiasi gani cha madini yaliyoibwa kwenye karatasi vs yaliyoibiwa kupitia njia za panya?

Unadhani Dalali anatoa wapi mzigo?

"Kama hatuogopi wezi kwa nini hata nyumba za udongo zina milango yenye kufuli"???
Jingalao
 
Nyumba isiyo na madini inalindwa na electric fence sembuse pori la mererani lenye Tanzanite?
Njoo utetee huu upuuzi wako uliokuwa unautetea wakati ule wa utawala wa nguvu kuliko akili. Mama amesema huko Mererani madini yanaibiwa na ukuta upo.
 
Njoo utetee huu upuuzi wako uliokuwa unautetea wakati ule wa utawala wa nguvu kuliko akili. Mama amesema huko Mererani madini yanaibiwa na ukuta upo.
Kabla ya ukuta tulikuwa tunaibiwa juu ya ardhi na chini ya ardhi.Ukuta umetupa fursa ya kujua mengi
 
Ukuta ulikuwa suluhisho la watu wanaotumia mabavu kuliko akili. Naona mama kaamua kujitenga na matumizi ya nguvu kuliko akili.
Hawa jamaa walishangaza sana eti ukuta uzuie wizi? Utadhani wanalinda shamba la mahindi.

Wenzetu huko wanatumia teknolojia kma RfID eti hku tunakimbizana na majeshi na Maukuta kulinda madini!!

Utashangaa watasifia hii kauli pia
 
Je airport wanavyopitisha kimagendo nako hakuna ukuta?? Makinikia bandarini kulikuwa hakuna ukuta wala wakaguzi?? Tuacheni siasa mngeongeza wataalam wa ukaguzi basi ingetosha kuliko kujenga ukuta as if walinzi wakihongwa hawawezi toroshea hata kutumia magari yao ya patrol!!!
I said this back then watu wakanipinga na mapovu juu
 
Back
Top Bottom