Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 20, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Ukuta, mabweni ndio vipaumbele vya UDSM? Wednesday, 19 January 2011 21:21

  [​IMG] Profesa Rwekaza Mukandara

  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kinatarajia kujenga ukuta kuzunguka eneo lote la chuo hicho, ili kukabiliana na kile ambacho uongozi wake umekiita tishio la uhalifu na uvamizi wa eneo hilo. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandara alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee itakayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete huko Ikulu leo usiku ya kuhamasisha ujenzi wa kituo cha wanafunzi cha kujisomea kitakachogharimu takribani Sh18 bilioni.

  Profesa Mukandara alisema kuwa ujenzi huo umo katika mpango kabambe wa chuo hicho wa kubadili sura yake na akadokeza kuwa yatajengwa mabweni ya kuhifadhi wanafunzi wapatao 4,500. Alitaja huduma nyingine zitakazotengewa maeneo kuwa ni za Intaneti, ofisi za vyama na makundi tofauti ya wanafunzi, mgahawa, maduka ya vifaa vya kitaaluma, huduma za utoaji nakala, uchapaji na maktaba kwa ajili ya wanachuo wa shahada za juu.

  Tunaupongeza uongozi wa UDSM kwa kufikiria kubadilisha sura ya chuo hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa hakipanui huduma zake wakati idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kwa kiwango cha kutisha kila mwaka.

  Tunaupongeza uongozi huo pia kwa kubuni mbinu za kuchangisha fedha za kuwezesha kufanyika mabadiliko hayo, hasa pale tunapoambiwa kuwa wafanyakazi wa chuo hicho tayari wamechangia zaidi ya Sh1.3 bilioni. Ni kitendo kinachohamasisha kila mmoja wetu kuchangia mradi huo mkubwa na tunadhani Rais Kikwete usiku wa leo atatumia mafanikio yaliyopatikana kuwahamasisha wengine kutoa michango yao kwa chuo hicho kikongwe kuliko vingine hapa nchini.


  Pamoja na kupongeza juhudi hizo ambazo Profesa Mukandara alizitangaza juzi, tungependa kutoa angalizo kwamba UDSM kamwe haihitaji kupoteza mabilioni ya fedha katika kujenga ukuta wa kuzunguka chuo hicho na kwamba isirudie makosa yaliyofanywa na vyuo vingine, kikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kutumia mabilioni ya fedha kujenga mabweni ya kuhudumia maelfu kwa maelfu ya wanafunzi, badala ya kujihusisha na ujenzi au upanuzi wa miundombinu inayoweza kuhimili vilivyo idadi ya wanafunzi waliopo na watakaojiunga na chuo hicho miaka ya usoni.

  UDSM lazima itumie rasilimali zake kwa kuangalia vipaumbele. Kwanza, tatizo la wizi katika chuo hicho halitokani na wavamizi kutoka nje bali tatizo hilo kwa miaka nyingi kitovu chake kimekuwa humohumo, kwa maana ya baadhi ya wafanyakazi na wanafunzi ambao wamekuwa wakiiba mali za chuo.

  Kwa ulinzi uliopo chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na kituo kikubwa cha polisi na kikosi imara cha mgambo wenye silaha, haiwezekani vibaka au mtu mwingine anayejitakia mema kuingia humo na kuiba pasipo ‘ruhusa’ ya wenyeji.

  UDSM iepukane na mbinu zilizopitwa na wakati. Uwapo wa ukuta hautasaidia kitu. Katika ulimwengu wa leo zinahitajika mbinu za kisasa kama kuweka kamera katika sehemu muhimu na kufunga mitambo na vifaa vingine vya kupekua magari, wafanyakazi na wageni wanaoingia na kutoka, bila kusahau kutoa ajira kwa wafanyakazi waaminifu tu.

  Mipaka ya UDSM imekaa vizuri iwapo mfumo wa ulinzi tulioutaja hapo juu utasimamiwa vizuri na ingefaa uongozi wa chuo hicho ujue kwamba vyuo vikuu popote duniani havijifungii ndani ya uzio kwa visingizio vyovyote vile.

  Kwa upande wa ujenzi wa mabweni, uongozi wa UDSM ungefaa pia ufahamu kwamba biashara ya ujenzi wa mabweni katika vyuo popote duniani hufanywa na sekta binafsi au mashirika ya biashara kama ilivyo kwa Hosteli za Mabibo. Kazi ya serikali au vyuo vyenyewe ni kuwapa fursa wawekezaji kufanya kazi hiyo, ingawa mabweni machache yanaweza kuwapo ili kuwasaidia wanafunzi wanaotoka nchi za nje katika mwaka wao wa kwanza.

  Vinginevyo, UDSM na vyuo vingine vijifunze kutumia rasilimali chache zilizopo kwenye miradi yenye vipaumbele kama vile vingine ambavyo Profesa Mukandara alitangaza juzi. Tunakitakia UDSM mafanikio katika harambee yake leo usiku.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,711
  Trophy Points: 280
  Majengo ya zamani ya hali mbaya.yanadai ukrafati sasa sijui kwa nini hayapo kwenye hivyo vipaumbele.............................Tatizo la maji bado ni sugu hivi hata kujichimbia visima na kuongeza matanki ya kutunzia maji hawaoni ni vipaumbele...............
   
 3. K

  KVM JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  I think UDSM on this occassion have got their priorities upside down, especially on the fencing of the main campus. The university is facing many academic and student welfare challenges which should be given priority. For example, I recently visited the University Bookshop. What I found there was heartbreaking. The Bookstore is only selling kindergarten books etc. I have not been inside the University Library in recent years. What I saw years back was also heartbreaking. No new books! The Library was not air-conditioned a situation which makes the stored books lose their colours (white pages become khaki), they become brittle and later break easily. Among the student welfare issues which should be given priority include state of the art sporting facilities such as tennis courts, soccer stadia, etc. Where are the Mlimani professors?
   
Loading...