Ukuaji wa viwanda vya kuzalisha mbumbumbu Nchini Tanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukuaji wa viwanda vya kuzalisha mbumbumbu Nchini Tanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tembeleh2, Jan 27, 2011.

 1. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila mtanzania anakubali kwamba nchi hii ilitengenezwa na watu waliojaribu kushughulisha bongo zao kufikiri. Kufikiri huku ni katika kujaribu kuitengeneza Tanzania ya wakati huo (wakati wa uhuru), na wakati huu/ujao. Waliweka misingi mizuri sana ambayo hata mtu ambaye hajaenda shule akisomewa tu anajenga matumaini juu ya maisha yake ya wakati huo na baadae.

  Kitu kibaya zaidi na kinachotisha zaidi ni namna uzalishaji wa watu watakaotoa majibu mepesi ya maswali magumu unavyoongezeka kwa kasi ya ajabu. Wazazi wamekuwa wakiwashawishi na inapobidi kuwalazimisha watoto wao wasome UHASIBU au IT (Information Technology) na sio ualimu kwa sababu wanazozijua wao. Sasa fani ya ualimu imebakia kwa ajili ya watu waliofeli, kufoji vyeti, na mbaya zaidi kutokana na mazingira ya waalimu huko kwenye vituo vyao hupoteza kabisa ari ya kufanya kazi. JE MWALIMU WA AINA HII ATAZALISHA WANAFUNZI WA NAMNA GANI????
   
Loading...