Ukosefu wa Maji Kahama TANESCO mnachangia

Ukosefu wa Maji Kahama TANESCO mnachangia

Zheneba

Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
75
Reaction score
9
Leo ni siku ya nane hakuna maji Kahama kwa sababu TANESCO wamewakatia umeme, sisi wananchi tunalipa bili kwa wakati na usipolipa unakatiwa maji hivi hela zetu zinaenda wapi? Kama wangetenga kila mwezi walipe hata milioni 10 TANESCO sidhani kama wangekatiwa umeme.

Hali ya vyoo hasa mahospitali, mashuleni na majumbani ni mbaya sana, Leo buchani hakuna nyama maana hakuna maji machinjioni muda si mrefu milipuko ya magonjwa itaanza.

Hata hivyo imeonyesha wazi Mkurugenzi wa KASHUWASA ameshindwa kazi aondolewe.
 
Poleni sana, huku shinyanga maji yameanza kutoka kwa baadhi ya maeneo.
 
Ni siku 10 na si nane!Niliuliza ni kwa nini inakuwa hivi ingawa tunalipa bili za maji vizuri tu ikasemekana pesa zote huenda serikalini yaani hazina na waziri wa maji ndiye anawajibika kuziomba na kulipa Tanesco.Sasa kama unavyojua urasimu wa serikali zikishaingia huko kutoka ni mbinde.
Tunaumia sana na utaratibu huu unapaswa kubadilishwa.
Bahati mbaya hakuna hata taarifa yoyote na kama imetolewa basi wengi haijawafikia.
 
Poleni sana wanataka kutuharibia jiji la kahama? nilikuwa nisafiri kuja huko ngoja nisubiri maji yarudi kwani itakuwa kazi sana
 
Ni siku 10 na si nane!Niliuliza ni kwa nini inakuwa hivi ingawa tunalipa bili za maji vizuri tu ikasemekana pesa zote huenda serikalini yaani hazina na waziri wa maji ndiye anawajibika kuziomba na kulipa Tanesco.Sasa kama unavyojua urasimu wa serikali zikishaingia huko kutoka ni mbinde.
Tunaumia sana na utaratibu huu unapaswa kubadilishwa.
Bahati mbaya hakuna hata taarifa yoyote na kama imetolewa basi wengi haijawafikia.
Mm pia nimewaza sana hivi bili zetu zinaenda wap dah asante kwa taarifa
 
Sio utaratibu mzuri kabisa makusanyo kwenda hazina. Urasimu wa kuzitoa hizo pesa kutoka hazina mpka ziwafikie tanesco mwanza tayari watu wameathirika sana. Poleni sana naufaham mji wa khma maji ya visima in hatar sana hasa maeneo ya huduma za jamii kma hospital Polisi magereza kanisani nk
 
Maji ni uhai, sheria ingetungwa ni marufuku kumkatia maji mtu
Thubutu umkatie mtu maji nchi zingine
 
Back
Top Bottom