Ukosefu wa maji salama kwa baadhi ya mikoa; Wananchi fungueni kesi

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Kwa takribani wiki moja baadhi ya wilaya na mikoa imekosa maji baada ya tanesco kukata umeme kwenye visima/pampu za idara za maji ya maeneo husika. Ni jambo la dharau na dhihaka kwa wananchi sababu wao siyo visababishi vya kadhia hizo. Watumiaji/ wananchi huwa wanalipa bili zao karibu kila mwezi na ikiwa hawajalipa hufungiwa huduma/ mita hutolewa. Iweje leo maji yasipatikane kutokana na shida ya idara za maji?
1. Malipo ya kila mwisho wa mwezi
2. Malipo ya kufungiwa maji
3. Malipo ya wakaguzi

Je fedha zote hizo zinaenda wapi hadi mshindwe kulipia bili za umeme?

Huu ni unyanyasaji ulio wazi. Wizara husika haijui hili? Leo kuna baadhi ya hospital hazina maji.wagonjwa wanahudumiwaje?

Je, hakuna sheria za kushtaki mashirika ya sirikali(serikali)

Tanzania kuna vita vingi muda huu zaidi ya zamani vilivyokuwa vita vitatu
 
NAUNGA MKONO HOJA
 
Back
Top Bottom