Ukomo wa Toyota Crown Sedan

nimeicheki ni kali, naona waliamua waachane na vile vi body vyao ndio maana imekuwa kali
RAV4 zina tatizo la kuwa na migulubaja... Linachutama, hilo ni tatizo kuu la hizo gari, wheel alignment inahitajika nafikiri kila baada ya KM 3000 duh
 
Basi ngoja ni ahirishe kuliagiza... kumbe mabovu hivyoo.. lisije nitesa bure
 
Maoni ya wanamtandao wengi wamestushwa na habari hizo kwani gari hizo zimeonekana kupendwa sana hasa na vijana kutokana na muundo wake pamoja na perfomance yake, na wameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa gari za juu aina ya SUV zipo nyingi sana kwanini TOYOTA wamekuwa na akili mgando za kuachana na utengenezaji wa gari hizo.


Hao ni wabongo wanaotaka za milion 13
 
Pia tukumbuke kuwa hizi crown ambazo zimejaa hapa Tanzania ni za kitambo kuanzia 2005-2013..
Sasa kama matoleo yanaishia mwakani naona bado kuna muda mwingi wa kuendelea kuagiza haya Magari,nahisi bado crown zitaendelea kutumika mpaka mwaka 2030

2030 ni karbu sana ...izo habari ya kusitishwa wanajua wachache eg ist 2nd generation toka 2016 haipo sokoni ila leo unakaa kijiweni mtu anasema toyota anauza sana ist sababu wanaona old model zilivonyingi wanajua bado zinatoka kiwandan kumbe new model ake ni miaka minne haipo sokoni ...

Kifupi wakimaliza hizo zitatapakaa sana ile ist ya pili hivo bado kuna miaka mingi sana ya kutumia ist sembuse crown ndo bado sana
 
Mnyama nilikiwa namkubali sana kwenye safari ndefu kitu kimetulia puling ya kutosha TOYOTA, shida wanamuwaza sana RANGE ROVER ..... wabaki kwenye mstari tu vinginevyo mambo yatakuwa magumu sana

Mnaonunu used ndo mnaopiga kelele....hao wameona hailipi ...we unaweza nunua vitz mpya ya milion 30 plus🤔 unataka uje nunua baada ya miaka 10

Kama walivoacha production ya IST baada ya mauzo kuwa mabovu ndivo wataacha pia na crown
 
Design ya gari exterior na interior inavutia, yaani ukiambiwa milioni mia unasema kweli. Sasa tizama Toyota, hakuna ata effort ya ku justify milioni mia

Pick up yao single cabin kuna mtu alinununua 145m tsh mpyaa ..simaanishi hilux namaanisha pick up as body style cruizer
 

RR

Range rover

Kwan gari zenye hilo neno zipo ngapi hadi ufikie hatua ya kufananisha na toyota zote🤔
 

Nishawah design kitu kikafanya kazi for several months ila kilizima na mpaka sasa sijui tatizo ni nini😁😁 nimeshindwa repair nawaza badili vitu vyote nianze upya kwa hiyo na LR yamewakuta hayo

Hata kuna kipindi cha window phone nokia ilileta tatizo hata wahusika hawakuwa wakijua
 
Sawa ndugu yangu, lakini unapouza LC milioni 200 ikiwa na tech ya zamani na mwenzako anauza RR kwa milioni 200 ikiwa na tech ya sasa, wewe wa LC utakuwa unatuchezea sasa. Kwanini usiuze tu kwa bei ya zamani kama zilizopita labda uongeze kidogo tu. Nimesema kuna kipindi BBC walikuwa na pick up ambayo imewekwa gorofani sijui jengo ghorofa ngapi lile labda 10, likawa demolished, gari imetolewa inakwenda. RR ingekuwa ishavurugika kitambo. Tuzungumzie price kwa features ili ku justify pricing ya LC na hasa hasa haya wanayotamba nayo viongozi.
 
LC 200 ni mbaya kiasi kwamba vijana wetu wa veta wanaweza kudesign a better looking car.

Unatoa 300Mil kwa Land cruiser ipo poorly designed.
Gari haina ata mvuto aisee. Ndio nasema bei yake, bora ununue RR utafurahi. Yaani haya LC yanashindanishwa na Vogue ila naona ata Velar tu inaifanya LC ionekane mkusanyiko wa vyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…