Ukomo wa CCM madarakani: Je, wakati wake umetimia?

Ukomo wa CCM madarakani: Je, wakati wake umetimia?

ArchAngel

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
4,513
Reaction score
3,764
Ni ndefu, but tafadhali isome...

Dr Makira:
"Hakuna chama duniani kinacho weza kutawala mfululizo zaidi ya miaka 40. CCM inaondoka madarakani rasmi baada ya Uchaguzi wa tarehe 25 October 2015, Hakutakuwa na Fujo yoyote wala Msuguano wa aina yoyote kama baadhi ya watu wanavyotaka iwe.

Kuondoka kwa CCM madarakani sio kosa la Rais aliyeko madarakani, Sio kosa la Kiongozi yeyote wa utawala huu bali ni kutimia kwa nyakati zake. Kuna watu wanahemka sana na kutamani kutupiana lawama na ghadhabu. Naamini raisi mwenyewe anajitahidi kufanya liwezekanalo ili akinusuru Chama na kila mbinu na bidii inakuwa kama kutwanga maji kwenye kinu.

Kila kitu kinacho shikwa kimepasuka na hii inaumiza vichwa watu wengi kwenye madaraka wakipambana usiku kucha Chama kisidondoke. Lakini watamaliza mabilioni yao yote na hela zao lakini CCM imefikia hatma yake kwa mujibu wa majira na nyakati zake.

Hitimisho la Chama hiki halitokani na matakwa ya kisiasa bali NYAKATI na MAJIRA yake kutimia. Watu hawapambani na Majira bali binaadamu huyafuata majira. Majira yakifika yamefika huwezi kuyazuia.

HAKUNA, NARUDIA TENA, HAKUNA MAJIRA YA DOLA YANAYO WEZA KUTAWALA ZAIDI YA MIAKA 40 MFULULIZO. Miaka 40 ni mchoro wa mstari mwekundu hakuna mamlaka za kidunia zinazo weza kuacha utawala ukavuka mstari huo. CCM from
1977-2015 ina miaka 38 , hapo ndio kikomo.

Kama CCM itashinda kwenye uchaguzi basi itakuwa madarakani kwa miaka mitano zaidi 2020 hapo itakuwa na miaka 43, itakuwa imeshavuka mstari mwekundu wa utawala kitu ambacho HAKIWEZEKANI wala hakuna mtawala wala Chama hapa duniani kilicho tawala zaidi ya miaka 40 wala kinacho weza kuvuka mstari wa utawala wa Mwenyezi Mungu.

NITOE MIFANO MICHACHE YA VYAMA VYA KISIASA VILIVYO TAWALA MUDA MREFU BARANI AFRIKA:

Algeria (NLF …1962-1992 ) miaka 30
Angola (PMLA …1975-2015) miaka 23
Cameroon (CPDM…1985-2015) miaka 30
Congo (PMR ..1971-1997) miaka 26
Ivory Cost (PDCI-RDA..1960-1999) ..miaka 39
Kenya (KANU …1963-2002)…… Miaka 39
Mozambique /msumbiji (FRELIMO 1992-2015 [after 17 years of civil war]..miaka 23
Rwanda (NRM..1973-1994)…miaka 20
Uganda (NRA.. 1986-2015)…miaka 29
Zambia (Unip..1964-1991) miaka 27
Zimbabwe (ZANU-PF 1980-2015) miaka 35
TANZANIA (CCM ..1977-2015) miaka 38

Vyama vingine vya kiafrika vimekuwa na utawala wa muda mfupi mfupi. Ukiangalia jedwali hilo utaona chama cha
Parti Démocratique de la Côte d'Ivoire - Rassemblement Démocratique Africain,(PDCI-RDA) Kilivuta utawala wake kuanzia mwaka wa uhuru wa ivory cost wake 1960 hadi 1999 kwa miaka 39, kilipo karibia kunusa miaka 40 kikatupwa nje na Robert aliye pindua kijeshi.

Chama kikijikakamua kujaribu kupenya miaka 40 ama kitaondolewa kwa demokrasia au hata kijeshi kama ilivyokuwa kwa Ivory cost ambapo kwa mwaka mmoja jeshi lilichukua nchi kabla ya kuachia utawala wa raia.

Mfano mwingine wa chama ng'ang'anizi kilikuwa KANU. Chama hiko cha Kenya kilijikongoja kwa bidii tokea uhuru wa Kenya 1963 lakini ilipofika 2002 kikagota. Untold story kuhusu Kenya ni kwamba Kanu Kilitupwa nje mgombea wake akiwa Uhuru Kenyatta wakampa Mwai Kibaki wa NRC, lakini wakenya hao hao wamekuja tena kumchagua Uhuru kenyatta akiwa Jubileee Alliance hiyo juzi 2013.

Ina maana gani, kwamba 2002 Uhuru alikuwa mbaya na 2013 kapakwa mafuta gani kawa mzuri tena!!, NO.. Fact za Hekima ni kwamba Majira ya TANU yalikuwa yametimia. Tanu isingeweza kupenya 40 years more. Uhuru hakuwa na ubaya wowote lakini majira ya Chama Chake yalitimia. Ni kama Watu wanavyo mwona Magufuli na CCM, Majira ya CCM Yametimia no way Magufuli anaweza kupenya. Ila Baadae akijiweka vizuri au kutumia CCM hii hii au chama kingine May be Magufuli can go but not NOW.

CCM wangetaka kuendelea kuwa madarakani WANGEKIVUNJA CHAMA NA KUZAA CHAMA KINGINE KWA JINA JINGINE, hapo wangefanikiwa kuendelea na utawala kama walivyofanya 1977 kuvunja TANU na kuzaa CCM. Ila ila kwa sasa too late. Kupambana CCM iendeleee kuwa madarakani ni Kupambana na Mwenyezi Mungu ndio maana wengi wanaishia Kufa au kupatwa na matatizo makubwa.

Nataka Nifafanue kweli hii kwenye maandiko ya biblia pia.

Katika Utawala wa wafalme wa Israel.. Mfalme wa kwanza alikuwa Sauli, Huyu alitawala kwa miaka 27, Mfalme wa pili alikuwa Daudi naye alitawala kwa miaka 40 hakuzidi hapo. mfalme wa tatu alikuwa Solomoni aliyetawala kwa miaka 40. Wa nne walikuwa wawili Yeroboamu ma Rehoboamu ambao wote walitawala kwa miaka 22 kila mmoja. Baadae ukisoma habari za wafalme utagundua wote hakuna aliye zidi miaka 40.

Ukiangalia utawala wa Musa. Alilelewa kwenye Nyumba ya Kifalme –Misri baada ya kufanya vitu vyake akatimuliwa akiwa na miaka arobaini, akaenda midiani huko jangwani alikokaa miaka mingine arobaini. Akiwa na miaka 80 akarudi sasa kuanza harakati za kuwaongoza wana wa Israel kuwatoa misri kwenda kanaani. Akawaongoza miaka arobaini tu akafa akiwa na miaka 120 ingawa biblia inasema Musa alikuwa bado ana nguvu za kutembea na kuona sawasawa ila Mstari wa uongozi wake ulifikia kikomo cha miaka 40.

Ukivipeleleza vitabu vyote vya dini hakuna mtawala aliye zidi miaka 40, Mtume Mohammad Alikuwa mfanya biashara na mwanaharakati kwa miaka 26 kuanzia 583–609 CE na kisha akawa Kiongozi wa Dini kwa miaka 23 kuanzia mwaka 609–632 CE. Katika Historia zote za kitawala hakuna Chama au mtawala ambaye anaweza kuvuka miaka 40 kwa sababu hiyo ni kanuni ya Kimungu na haivunjwi na binadamu.

Ukiangalia Taifa la Marekani, tokea Uhuru wake1732 Chama kilicho ongoza kwa muda mrefu ni Democratic Republican, kipindi hicho mahasimu hawa wawili waliform chama kimoja, kiliongoza kwa miaka 28 mfululizo from 1801-1829. Hakuna chama kingine kilicho ongoza mfululizo zaidi ya hicho. Huko Uingereza kipindi kile ikiitwa Great Britain Chama cha WHIG 1721-1761 kwa miaka 40 mfululizo kabla ya kung'olewa."
��������
Summary ya haya yoote tuyaonayo!!

Imenipa na majibu ya kwa nn Edo alikatwa na CCM kumbe ni ili maandiko yatimie. Aliyeandika ana akili sana kwa kweli!!
 
Chukua Weka Lowassa, Piga hatua 200M, Endelea na Mambo Mengine na Baadae Ukasikilize Utangazwajwi wa Mtokeo.
 
MTU wa maamuzi Magumu kashindwa kujibu maswali Magumu juu ya UFIDADI na WIZI, anasema ni Swali gumu linahitaji mchakato hafai kua Kiongozi CCM inaenda kuongoza tena miaka 5 mingine.
 
MTU wa maamuzi Magumu kashindwa kujibu maswali Magumu juu ya UFIDADI na WIZI, anasema ni Swali gumu linahitaji mchakato hafai kua Kiongozi CCM inaenda kuongoza tena miaka 5 mingine.

kweli wewe na avatar yako mnalandana sana. Ulijuaje ukaichagua kama upeo wa uelewa wako ni mfupi hivi? Kikwete akiwa ziarani Marekani aliulizwa ni kwanini wananchi wake ni maskini akajibu hata yeye hajui ni kwanini. Swali, aliendelea kuwa rais? Mkapa akiwa UK aliulizwa swali hilihilo akamtukana mwandishi na mwisho akajibu hajui ni kwanini. Na aliendelea kuwa rais. Siyo kila swali lina majibu ya papo kwa papo kama nauli ya daladala mengine unatakiwa upewe muda na ujiandae kwani majibu mengine yanahitaji vielelezo na ushahidi. Jifunze kuanzia leo na uache tabia za digidigi.
 
Ndio maana wanahangaika wameajiri vijana na wamewaweka hostel za chuo cha afya muhimbili iliyopo masaki ndio wanapiga simu kumchafua Lowasa
 
Lakini kuna chama kule Mexico ambacho nadhani ndicho kinachotawala sasa kwamba kipo madarakani kwa miaka 70 sasa!!

Sijui historia ya nchi ya Mexico lakini kwa yeyote anayefahamu hasa mleta mada, naomba nifahamu kwanza kama hii ni kweli.

Pili, Je, ni mazingira yepi yamepelekea chama hicho kuwepo madarakani (kwa kuchaguliwa) kwa miaka 70 hata "fact" na asili ya mambo haya ya "kutovuka mstari mwekundu" chenyewe kisihusike?
 
Back
Top Bottom