Ukombozi wa fikra; tatizo linalowatesa wanawake wengi

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam wakuu,

Kwanza nitoe angalizo kuwa mada yangu hailengi kuwaondolea heshima wanawake kwani umuhimu wao kwenye jamii zetu umetukuka.

Nimeona niwashirikishe kisa kufupi Cha mwanamke huyu aliyekataa kuolewa na rafiki yangu kwa kuhofia kukosa misaada kwa mchepuko wake.

Unaweza kushangaa lakini ndo ukweli.

Dada mmoja msomi wa kiwango Cha Kati ambaye ameajiriwa chini ya wizara ya afya amegoma kabisa kuolewa na rafiki yangu ambaye nae kwa kipato chake anaweza kuendesha maisha Kama wanandoa wengine.Rafiki yangu alikua serious kweli kutaka kumuoa kutokan naumri kusogea.

Dada huyo amemweleza jamaa kuwa kweli anampenda lakini anashindwa kumwacha huyo mchepuko wake kwani kamfanyia Mambo mengi sana ikiwemo connection ya ajira.

Kilichonishangaza zaidi nikwamba huyo mchepuko wa mdada ni mume wa mtu na alishamwambia yule dada akipata mume aolewe tu kwani hawezi kuoa wake wawili.

Kingine cha ajabu nikwamba walau kwa mshahara namarupurupu yake,dada huyu inakuaje amtegemee mume wamtu hadi asitake kuwa na ndoa yake.

Kwa kuwa huyu rafiki yangu nae alimpenda yule dada na ukizingatia yupo kwenye uhitaji mkubwa wakuoa, amempa yule dada muda wakufikiria ili aone namna yakumwacha huyo mchepuko. Alimwahidi yule dada Kuwa atajitahidi wakioana wafanye maendeleo ambayo hayatatoa nafasi yakujutia maamuzi yake yakumwacha mchepuko.

Mwezi Sasa umekata dada hajarudisha majibu.

Mwisho: huyu dada yupo sahihi kukataa ndoa kisa kuogopa kukatika kwa misaada toka kwa mume wa mtu?

Naamini huyu bado kafungwa kweny fikra za utegemezi, anahitaji ukombozi.
 
Kwa upande wa maamuzi huyu mwanadada hayupo sahihi. Ila pia naamini mwanadada hana uhitaji wa ndoa kwa wakati huo ama jamaa yako hayuko sawasawa kifedha mpaka mwanadada amepata kigugumizi kufanya maamuzi.

Lakini pia huyo jamaa yako nae anafanya makosa kwani attitude ya mwanadada imeshaonesha kua ananufaika na huyo mtu aliemtengenezea connection kwa namna nyingi hivyo hata kama mwanadada angeridhia kuolewa na jamaa yako bado naona wangesumbuana kwani mwanadada anaonesha wazi kua huenda angeendelea kua wa uhusiano wa karibu na mtu yule.

So kwa upande wangu naona mwanadada kamuokoa jamaa katika majanga ya hapo baadae kwa kuamua kile ambacho ameona yeye kinafaa kuliko ange pretend tu.
 
Huyo dada Bado anakula ujana, na kwa Sasa Hana utayari wa kuolewa, Bado anatembeza mbusus kwa kuonj radhaa ya rungu mbalimbali za watu mbaya zaidi ana pesa na kipato cha kutosha.

Huyo hawezi kuwa wife matarial, huyo jamaaa yako pabaya panamkataa pema panamwita, lakin Bado analili pabaya.

Mwambie amchape rungu tu, then atafute mwanamke mzuri asiye na malingo wala kipato kikubwa ambaye atamtii, aachane na hao slay queen 🔥🔥
 
Fainali uzeeni, visa vya aina hio mwisho wake huwa majuto kwa binti kwa kuwa maringo yao huwa ni ya muda mfupi kabla ya kuwa phased out sokoni.

Ipo siku atatamani ndoa kisha akirudi kwa mwana atakuta alishapata mke na watoto watatu. Atabaki na ningejua tu sahio ubao unasoma 33 yrs. Old
 
Usipende kupangia watu maisha kila mtu mzima anafanya maamuzi vile serikali yake inavyomuendesha. Kila mtu na staili yake ya maisha na sio kila mwanamke hitaji lake ni ndoa, the world is changing so fast.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mdada anakwambia kabisa kwamba ana enjoy life na mchepuko, wewe unamshawishi aolewe! Nadhani hapo kaka unatafuta balaa huko mbeleni.. huyo dada thinking yake sio kuolewa bali ku enjoy life na mchepuko, hyo ndo life style aliyo chagua
 
Back
Top Bottom