Ukombozi utaletwa na raia na si chama cha siasa

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam wana JF!

Nimekua nikijiuliza mara nyingi,hivi ni lini TZ yetu itakombolewa kutoka kwenye huu utawala dhalimu? Na mara zote sipati jibu la uhakika! Nimejiuliza tena,hivi kuna chama cha siasa ambacho kinaweza kututoa waTZ kwenye hili janga la shida na umasikini? Hapa pia naona chenga tu!

Lakini mwishowe nimekuja kufahamu kua ukombozi wa kweli utafanikiwa pale sisi raia tutakapoamua kuushikisha adabu utawala huu dhalimu. Pale raia tutakapoifanya serikali ituogope na si sisi tuigope! Na wasaa huu hauletwi na wala hautaletwa na chama chochote cha siasa!

Kwa hiyo waTZ tusitarajie chama chochote ndio kiwe mstari wa mbele katika kuuongoza mapambano ya kutafuta ukombozi wetu! Maana siku za hivi karibuni kumekua na hisia kua chama fulani ndio kiongoze mapambano ya ukombozi;chama fulani ndio kiandae maandamano ya kudai serikali ipunguze ukali wa maisha n.k. Kwa namna hiyo ndugu zangu tutasubiri mpaka Yesu atakaporudi!

Ndugu zangu UKOMBOZI utaletwa na sisi raia! Hivyo ni wakati muafaka wa sisi kuanza kuifanya serikali itimize wajibu wake kwa raia. Na katika nchi za kidemokrasia,maandamano ndio njia kuu ya kuishurutisha serikali.

WaTZ tuwe na mioyo ya uthubutu,tutoe hofu (najua baadhi yetu tunaweza kuuwawa au kujeruhiwa) na tuwe tayari kuikomboa nchi yetu. Wakati ni huu!

Haya ni mawazo yangu,kukosolewa kunaruhusiwa!
 
Sisi wananchi tutapojitambua ndio ukombozi halisi utapatikana.Angalia hata sasa tumewaachia wanasiasa waamue hatma ya katiba mpya.
 
Nakuunga mkono asilimia mia moja.Hakuna chama chochote kitakachotutetea wanyonge wa nchi hii,huu ni ukweli mchungu.Angalia Cdm wamepoteana kabisa hawana uelekeo wowote wa maana.Ukija kwenye posho unawakuta nao wapo mstari wa mbele kutetea posho zinazomnyonga mtanzania masikini, ukija kwenye mgawanyo wao wa madaraka pia nako ni upendeleo mtupu.Ni mashabiki wakereketwa tu ndio ambao hawalioni hili.I hardly find the difference between ccm and Cdm m,they are all both looters of this country.
 
Kudai ukombozi bila kupitia mfumo unaotambuliwa kisheria ni UASI ama neon jingine UHAINI.
 
Kudai ukombozi bila kupitia mfumo unaotambuliwa kisheria ni UASI ama neon jingine UHAINI.

Je, wanachofanya wanasiasa sasa hivi siyo UHAINI? Tena wa kiwango cha juu sana!!
 
Back
Top Bottom