jean paul marie
Member
- Aug 17, 2015
- 47
- 20
Ukomavu mkubwa sana
Kura si kigezo pekee cha uhalali wa kuongoza watu zaidi ya million 40, ndio maana wako wasiopiga kura na bado katiba inawapa haki na wajibu wa kuheshimu mamlaka ya Urais, ukiacha kura mgombea ajipime kwa namna anavyoungwa mkono na anaowaongoza.
Unaweza kuanza kutoa tathmini ni mgombea gani mpaka sasa anayeungwa mkono mijini, kabla hata ya kampeni, rejea jk alipoingia madarakani 2005, muelekeo wa ushindi wa kishindo ulianza pale tu alipoonyesha nia na kupitishwa na chama chake. Watu tulijitokeza kila alipopita kuonyesha namna tulivyokuwa na imani naye, na matokeo yaliakisi uungwaji mkono wa wazi, hakuhitaji mkapa ampigie kampeni kuweza kushinda, alisimama kwa miguu yake mwenyewe kwa kushirikiana na washirika wake, ikamuwezesha kushinda kwa kishindo bila ubishi.
Vivyo hivyo hivi sasa tuanze kufanya tathmini namna wagombea wanavyo hitaji backup ya hali ya juu kuweza kusimama, hii inatukumbusha mwalimu nyerere aliposema "mjue mtu mnaye mchagua ni lazima akubalike, kwa kuwa hatakuwa kiongozi wa ccm peke yake ila Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni lazima akubalike na umma".
Nguvu kubwa inatumika kuwachafua wagombea walioruhusiwa kuchukua fomu kwenye vyama vyao hapo kabla, ikidhihirisha vigezo walivyokuwa navyo, na sasa wamehama, tuhuma peke yake haziondoi haki kwa anaye tuhumiwa, hasa ukizingatia kwamba tuhuma nyingi za kisiasa ni chuki zinazolenga kuwathoofisha washindani, mfano na wajibu wa kuwashitaki waliohusika kwenye kashfa ya Richmond ilibaki kwa waliomadaraki kwa miaka zaidi ya saba, hii ikimaanisha kwamba tuhuma hazikuwa na mashiko na uhalali wa kuwashitaki mliwachafua.
Mliopo madarakani mtujuze vision ya taifa iko wapi?, ahadi mlizo toa tangu awamu ya kwanza ni kwa kiasi gani zimetekelezwa?, mnahitaji miaka mingine mingapi kukamilisha ahadi mpya na za zamani?, kapu la madeni limejaa kwa kiasi gani?, shillingi ya Tanzania inakwenda wapi?, ongezeko ajira kupitia viwanda limefikia wapi?, na mwisho takwimu za idadi ya watu wasiojua kesho yao?
Itaendelea muda mfupi ujao....................