Uko wapi weledi wa mama Prof. Ndalichako?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Maamuzi yake na watendaji wake wote katika wizara inayosimamia huduma za elimu nchini ndiyo majibu ya kidato cha NNE ya sasa.Hali si nzuri kabisa tofauti na miaka ya nyuma, walimu hawana ari na kazi, wanaingia darasani ili kuonekana wako makazini tu.

Wengine tulisema kuongoza Wizara ya elimu ni tofauti na kuongoza kitaasisi kidogo kama NECTA ambacho kipo chini ya wizara hiyo.

Hili suala la elimu linahitaji mijadala wa kitaifa kwa maneno ya Mh James Mbatia na sio kuamua haraka haraka tu bila kushirikisha wadau husika kwa kuhisi kua mtangulizi wako aliharibu hapo awali. Tukiendelea hivi baada ya miaka kadhaa tutakua na wasomi wachache nchi ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya awamu ya NNE ambayo ilionekana kubadili hali ya elimu nchini, ni kwamba tunarudi hatua nyingi nyuma kwa maneno ya mzee Jenerali Ulimwengu.
 
Watawala wanajua tatizo linalosumbua elimu yetu lakini kamwe hawawezi kijikita kutatua tatizo ili kutengeneza taifa la wajinga kwa kuwa wajinga ndio mtaji wao mkubwa wa kura.
 
Kama serikali itaendelea kutomjali mwalimu shule za umma zitaendelea kutia aibu tu,hata hao walimu wa sanaa mashuleni hawatoshi,rais aachie ajira za walimu watoto wafundishwe bila wasomi bombadier watapanda akina nani?
 
Serikali inaisi kuendesha wizara zote ni Sawa ebu tufikirie nini mana ya serikali kusema elimu bure ili kupunguza idadi ya wasomi na hata ao wachache ni bora wasomi km mitaala inabadilishwa kila siku ili wajinga ndo wawe wengi.lkn mengne tunaweza ilaumu mtu kumbe anaongozwa na mwingne kufanya atakavyo yule mtu yaani viongozi vivuli aya yote udhirisha kuwa bado tunatawaliwa tu Uhuru akuna lbda wa kujiita mtanzania ila c kujumuishwa ktk maendeleo ya aina yeyote
 
Maamuzi yake na watendaji wake wote katika wizara inayosimamia huduma za elimu nchini ndiyo majibu ya kidato cha NNE ya sasa.Hali si nzuri kabisa tofauti na miaka ya nyuma, walimu hawana ari na kazi, wanaingia darasani ili kuonekana wako makazini tu.

Wengine tulisema kuongoza Wizara ya elimu ni tofauti na kuongoza kitaasisi kidogo kama NECTA ambacho kipo chini ya wizara hiyo.

Hili suala la elimu linahitaji mijadala wa kitaifa kwa maneno ya Mh James Mbatia na sio kuamua haraka haraka tu bila kushirikisha wadau husika kwa kuhisi kua mtangulizi wako aliharibu hapo awali. Tukiendelea hivi baada ya miaka kadhaa tutakua na wasomi wachache nchi ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya awamu ya NNE ambayo ilionekana kubadili hali ya elimu nchini, ni kwamba tunarudi hatua nyingi nyuma kwa maneno ya mzee Jenerali Ulimwengu.
Nilitegemea useme hapa na uoneshe kosa alilolifanya Mama Ndalichako.
Amefanya kosa gani?
 
Ufaulu wa Div I mpaka Div III ni 27% percent! Hiyo div 2.75 iliyoongezeka inaweza ikawa umepunguzaDiv I 50 na kuongeza Div III au Div IV100!! Hapo ufaulu umeongezeka kweli? Uchanganuzi sahihi ni ule unaotupa hali ya ufaulu kwa kila daraja!!
 
Tutawalaumu mawaziri wote, wakati mwingine vijana na wenyewe wako bize sana na mitandao na vitu vingi vya ujanjaujanja huku wazaki wakiwachekea. Hili suala ni la kila mtu katika jamii kushirikiana.
 
Tutawalaumu mawaziri wote, wakati mwingine vijana na wenyewe wako bize sana na mitandao na vitu vingi vya ujanjaujanja huku wazaki wakiwachekea. Hili suala ni la kila mtu katika jamii kushirikiana.
Utakua mzazi wa ajabu na hivyo kama utabaki kumlaumu mwanao uliyemzaa wewe, unatakiwa ubadili mbinu kudeal na mwanao anapokushinda. Ithibiti wa tabia ya mwanao ni wewe mzazi
 
Utakua mzazi wa ajabu na hivyo kama utabaki kumlaumu mwanao uliyemzaa wewe, unatakiwa ubadili mbinu kudeal na mwanao anapokushinda. Ithibiti wa tabia ya mwanao ni wewe mzazi
Uko sawa kusema wako bize na mitandao ya jamii ndani yake yupo mzazi ambaye hatizimi wajibu wake ipasavyo.
mtoto analelewa ha housegirl huku mzazi anamuona mara mojamoja.
Jamii inaaza kuharibikia nyumbani sio shuleni wala barabarani.
Lazima tuwawekee vijana kanuni na kuzisimamia kwa faida yao.
 
Tatizo ni kuingiza siasa katika maslahi ya wafanya kazi wa kada husika bila kutatua maslahi yao hakuna cha maana
 
Back
Top Bottom