Uko wapi weledi wa mama Prof. Ndalichako?

Uko wapi weledi wa mama Prof. Ndalichako?

Ww mleta mada ni wa kupuuzwa pamoja na mada yako. Huyu waziri ulitaka awe amefanya kitu gani ktk elimu kwa kipindi hiki kifupi?

kama una viroba kichwani kaoge ama kanywe maji ya baridi. elimu siyo kigodoro ama mnanda ama ndoa ya mkeka uliyofungishwa, ni mchakato. huyu waziri matunda yake mengi ya kimfumo yataanza kuonekana baada ya miaka 2.

kwa sasa waziri kadhibiti udanganyifu ktk mitihani wa baadhi ya shule, ndiyo maana kuna nyingi huzioni tena kwenye kumi bora.

apongezwe waziri kwa kudhibiti udanganyifu
 
Suala ZIMA la ELIMU ni MTAMBUKA! Hatuwezi kumlaumuWaziri. Haya,tuanze hivi: Hawa vijana walomaliza Kidato cha Nne mwaka 2016 walianza Kidato cha Kwanza Mwaka 2013, wakati huo Mh. Ndalichako alikuwa Waziri? Jibu ni HAPANA, kwa hapo tu, kwanini tumlaumu yeye leo? Matokeo ya Kidato cha nne siyo mchakato wa wiki 2 ama 3 za Mitihani..
 
Tatizo na elimu ya Tanzania kila waziri anaekuja anakuja na jipya hakuna mitaala inayoeleweka, pia ushirikishwaji kwa wadau wa elimu hususani walimu wenyewe wanaojua matatizo ya elimu hamna...

Hapa ndio tulipofikifikia zero kwenye kata utadhani zimemwagwa
 
Ni nani aliyeturoga? Kila kukicha afadhali ya jana duh! Ila hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho..yangu mie macho tu..wamevurunda katika afya, elimu, utawala bora na mengine mengi tu! Mungu naomba unipe uvumilivu tu!
 
Tatizo kubwa nikutokujishughulisha na mitaala na badala yake kuweka nguvu nyingi kwenye ufaulu. Haijulikani mtoto aliyemaliza darasa la tano anatakiwa aweje tofauti na yule wa darasa la pili na ndiyo maana mtoto anafika sekondari hajui kusoma vizuri. Elimu isipomwezesha mwanafunzi kujitambua na kuwa na uwezo wakuyaelewa na kuyalinda mazingira na kuyadhibiti mazingira yake basi elimu hiyo haimsaidii mwanafunzi. Ufaulu wa mwanafunzi upimwe kwa kuonyesha umaahiri wake katika hili na elimu inayotolewa ifanane nchi nzima.
 
Maamuzi yake na watendaji wake wote katika wizara inayosimamia huduma za elimu nchini ndiyo majibu ya kidato cha NNE ya sasa.Hali si nzuri kabisa tofauti na miaka ya nyuma, walimu hawana ari na kazi, wanaingia darasani ili kuonekana wako makazini tu.

Wengine tulisema kuongoza Wizara ya elimu ni tofauti na kuongoza kitaasisi kidogo kama NECTA ambacho kipo chini ya wizara hiyo.

Hili suala la elimu linahitaji mijadala wa kitaifa kwa maneno ya Mh James Mbatia na sio kuamua haraka haraka tu bila kushirikisha wadau husika kwa kuhisi kua mtangulizi wako aliharibu hapo awali. Tukiendelea hivi baada ya miaka kadhaa tutakua na wasomi wachache nchi ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya awamu ya NNE ambayo ilionekana kubadili hali ya elimu nchini, ni kwamba tunarudi hatua nyingi nyuma kwa maneno ya mzee Jenerali Ulimwengu.
Bavicha at work!!
 
Ww mleta mada ni wa kupuuzwa pamoja na mada yako. Huyu waziri ulitaka awe amefanya kitu gani ktk elimu kwa kipindi hiki kifupi?

kama una viroba kichwani kaoge ama kanywe maji ya baridi. elimu siyo kigodoro ama mnanda ama ndoa ya mkeka uliyofungishwa, ni mchakato. huyu waziri matunda yake mengi ya kimfumo yataanza kuonekana baada ya miaka 2.

kwa sasa waziri kadhibiti udanganyifu ktk mitihani wa baadhi ya shule, ndiyo maana kuna nyingi huzioni tena kwenye kumi bora.

apongezwe waziri kwa kudhibiti udanganyifu
Wewe siwezi kukujibu maana unatsnguliza mhemko kwenye mambo ya msingi, Kama hujui ni vipi waziri Ndalichako ana effect gani kwenye hili la matokeo basi una kiwango cha hali ya chini kabisa cha kufikiria. Fuatilia athari za mabadiliko ya sekta ya elimu tokea mwaka jana.Walimu hawako motivated kabisa, wazazi kwa sasa ndio wenye sauti kuliko walimu, kuna upungufu Mkubwa wa walimu lakini tunaambiwa kua uhakiki unaendelea.
 
Ni nani aliyeturoga? Kila kukicha afadhali ya jana duh! Ila hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho..yangu mie macho tu..wamevurunda katika afya, elimu, utawala bora na mengine mengi tu! Mungu naomba unipe uvumilivu tu!
Usitegemee maendeleo kwenye taifa lako kama unatengeneza wasomi wachache
 
Umesema kweli Mkuu.

Ni aibu kwa Wizara ya Elimu yote na hasa Waziri ambae pale mwanzoni alikuwa anaongea sana kwa namna ya kubeza yaliyofanywa na watangulizi wake.

Sioni mikakati yoyote ya kututoa hapa elimu yetu hasa ya sekondari ilipofikia.

Mnaweza kubakia kusema Elimu Bure tu lakini haina ubora wowote.
Mkuu nakubaliana na wewe 100 percent.Sioni mkakati wowote wa kututoa out of this mess we are in. Ninacho-ona ni kudokoa tu matatizo hapa na pale na kuyapatia ufumbuzi.Elimu yetu inahitaji "Marshall Plan," sio udokozi wa hapa na pale,hali sio shwari kabisa.
 
Siasa !!! Siasa !!! Siasa !!!
Inatakiwa Siasa itenganishwe na kila kitu,
Itenganishwe na Biashara, Afya, Elimu, Huduma za Jamii, hapo ndipo tutakapoendelea.

Maamuzi yake na watendaji wake wote katika wizara inayosimamia huduma za elimu nchini ndiyo majibu ya kidato cha NNE ya sasa.Hali si nzuri kabisa tofauti na miaka ya nyuma, walimu hawana ari na kazi, wanaingia darasani ili kuonekana wako makazini tu.

Wengine tulisema kuongoza Wizara ya elimu ni tofauti na kuongoza kitaasisi kidogo kama NECTA ambacho kipo chini ya wizara hiyo.

Hili suala la elimu linahitaji mijadala wa kitaifa kwa maneno ya Mh James Mbatia na sio kuamua haraka haraka tu bila kushirikisha wadau husika kwa kuhisi kua mtangulizi wako aliharibu hapo awali. Tukiendelea hivi baada ya miaka kadhaa tutakua na wasomi wachache nchi ambao kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya awamu ya NNE ambayo ilionekana kubadili hali ya elimu nchini, ni kwamba tunarudi hatua nyingi nyuma kwa maneno ya mzee Jenerali Ulimwengu.
 
Mijadala ya elimu ya Tanzania imefanywa sannna!!!! Lakini mambo ni yaleyale!!!! Sijui nani mchawi wetu
 
Mkuu nakubaliana na wewe 100 percent.Sioni mkakati wowote wa kututoa out of this mess we are in. Ninacho-ona ni kudokoa tu matatizo hapa na pale na kuyapatia ufumbuzi.Elimu inahitaji "Marshall Plan,"hali sio shwari kabisa.
Mkuu Asante sana kwa kutumia maneno muafaka haswa... MARSHAL PLAN.. That's what is needed.
Shida sijui kama wanafahamu hilo.
 
Mama Ndalichako yuko poa sana. Tatizo ni kwamba sio wanafunzi wote lazima wafaulu. Hawa wanaofeli ndio wanatakiwa wawe wasafisha vyoo na wafagia barabara. Kwa kifupi wote hatuwezi kuwa madaktari, waalimu, wahandisi au wahasibu. Lazima pawe na masekretari, office attendants n.k. kazi zote ni bomba tu ila cha maana mshahara. Kwa hiyo matokeo ya kidato cha nne pekee hayatoshi kumuhukumu Mheshimiwa Ndalichako au kohoji weledi wake. Kikubwa ambacho nakiona huko mbele ni kwamba aliyesoma atarudi kuwa boss wa asiyesoma. Hapa katikati elimu ilimezwa na mambo mengi kama meshen town na forgery ya vyeti. Sasa wote lazima tuisome namba
 
Back
Top Bottom