Habari Mabibi na Mabwana wa Jf;
Haya matukio ya Panya Road kwa sasa yamekua yana tatanisha sana.
Mfano Mimi ni mkazi wa Temeke (Tandika) sikuwai kusikia wala kuona Panya Road.
Lakini cha ajabu nikienda kazini maeneo ya Sinza nawasiki watu wanahadisia kua Panya Road wamevamia Temeke (Tandika ).
Basi nabaki najiuliza, mbona mimi nakaa huko na hiyo siku ambayo wanasema Panya Road wamevamia nilishinda uko na nikawa ktk mizunguko mpaka saa 4 Usiku sikusikia wala kuona Panya Road?.
Hii inanifanya nikumbuke story ya Babu yangu, kuhusu Mwizi Maaru hapa jijini Dar alieitwa MAHMOUDU.
Ipo hivi;
Miaka ya nyuma kulitokea Mwizi maarufu kwa jina MAHMOUDU, kipindi hicho Dar yote kituo cha polisi kilikua Msimbazi Police tu ukiondoa makao Mkuu Centre, hii zamani kidogo.
Kesi za wizi zilizokua zikilipotiwa zote mtuhumiwa wao ni MAHMOUDU.
Haijalishi mleta mashtaka katokea wapi iwe Magomeni au Temeke, tena hata kama matukio yalitokea kwa wakati Mmoja.
Police walimtafuta MAHMOUDU na kumuweka ndani, chakushangaza kesi zikawa zinakuja na mtuhumiwa wao ni yuleyule bwana MAHMOUDU.
Sasa hawa Panya Road kweli wapo kama tunavyo Peana taarifa au tunatishana tu na kulikuza hili jambo.