mr.kifather
Member
- Feb 10, 2012
- 83
- 16
Ukisoma hii article 151 (1) "Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwamajina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge".
unaweza ukazani mahakama imewekwa huru kutoka kwenye msukumo na nguvu ya raisi lakini si kweli bali ni kiini macho kwasababu hii ifuatayo;
172.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo itaundwa na wajumbe tisa watakaoteuliwa na Rais kama ifutavyo:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;
(d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;
(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara;
(f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar;
(g) Wakuu Wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja
kutoka Tanzania Bara na moja kutoka Zanzibar watakaopendekezwa na Jaji Mkuu; na
(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu wa
Tume ya Utumishi wa Mahakama.
(2) Tume inaweza kumualika mtu mwingine yoyote mwenye
utaalamu mahususi kushiriki kikao chochote cha Tume, isipokuwa mtu
huyo hatakuwa nahaki ya kupiga kura.
Hii article kimsingi imemrejeshea raisi mamlaka yote ya uteuzi wa majaji kwasababu wanaopendekeza majina ya watu watatu kama article 151 (1) inavyoelekeza wote ni wateule wa raisi, sina imani watu hawa wanaweza mkatalia raisi endapo atapendekeza mtu wake.
kwa msingi huu basi, ni vipi mahakama zetu zina uhuru kwenye rasimu hii ya katiba mpya??
naomba msaada wenu kwenye swala hili...