Uko wapi Udikteta wa Rais Magufuli?

Uko wapi Udikteta wa Rais Magufuli?

Joined
Aug 21, 2016
Posts
33
Reaction score
504
Vyama vinavyounda UKAWA vimetangaza kufanya maandamano yenye lengo la kupinga udikteta, UKUTA. Maana yake ni Kwamba serikali ya Rais Magufuli in ya kidikteta.

Niwakumbushe UKAWA yafuatayo:

1. Serikali ya Rais Magufuli imechaguliwa na watanzania kikatiba katika Uchaguzi mkuu 2015.

2. Kulingana na katiba, Rais hushauliwa na Baraza la mawaziri. Na pia Rais hushauriwa na Chama chake. Hivyo, Rais Magufuli anafanya maamuzi Kwa kushauriwa na taasisi hizi. Hivyo madai Kwamba anaamua bila kushauriwa hayana mashiko.

3. Madai Kwamba anawagandamiza baadhi ya watanzania, ni jambo la kushangaza. Tukumbuke wakati WA sakata la EPA, Chadema walipiga kelele sana wakati JK alipowaomba wezi WA fedha za EPA wazirudishe. Wakasema anaongea na wezi. Rais Magufuli amechukua msimamo tofauti, amekuwa dhabiti. Sasa Chadema wanadai dikteta. Hapana.

4. Rais Magufuli amekuwa na msimamo Mkali dhidi ya Ufisadi, wakwepa kodi, ubadhirifu kwenye serikali na halmadhauri na mashirika ya umma. Anapigania utajiri WA Nchi Yetu uwanufaishe watanzania wote. Ukweli Rais Magufuli ni Jibu Kwa maombi ya watanzania wengi kutokana na hali ilivyokuwa imefika.

4. Upinzani wanachokifanya ni kutaka kuwapotodha watanzania ili waichukie serikali yao. Upotodhaji lengo ni uchochezi.

Ukowapi udikteta wa Rais Magufuli? Lakini uchochezi wa UKAWA in dhahiri. UKAWA wanadai demokrasia inaminywa. Tukumbuke, mgombea UKAWA alivyopatikana. Ilikuwa ndani ya chopa na watu wachache siyo kwenye vikao. Hapakuwa na mchakato ulio wazi. Iko wapi demokrasia kwenye UKAWA?

Pia tukumbuke, walimtuhumu Lowassa Kwa muda mrefu kuwa ni fisadi na wakawaeleza watanzania kuwa wanao ushahidi. Ghafla wakaamua awe mgombea urais. Uko wapi Uzalendo WA kweli ndani ya UKAWA?

Watanzania tumuunge Mkono Rais Magufuli.
 
Jpm ni mwami lakini mimi siuoni ubaya wowote, bona rwanda wanaye mwami kagame, uganda nao wanae kabaka museveni.
 
Unajitekenya huku unacheka..katiba inatoa Uhuru wa kutoa mawazo(freedom of expression) na association pia,yeye anakataza mikutano na maandamano huku akiwa wakwanza kuifanya tena kwa kuwaponda wapinzan..wajinga kama weww ndio wanaoamin hamna udikteta.
 
Fred Mpendazoe, kwa umri nilionao na ulionao wewe nina haki kabisa kukuita mpotoshaji.

Maandishi yako hapo juu yanathibitisha kujipendekeza kulikopitiliza.

Kwa akili yako hujui kwanini hasa Magufuli wanamuita dikteta? Basi kama hujui ni kuwa wale wote waliokuwa wanakuchukulia kama mtu mwenye upeo wa juu wa kuelewa walikuwa wanakosea.

Binadamu anayeamua kuishi maisha ya aina yako ya kubadili badili misimamo bila ya hoja makini ambazo yeye mwenyewe zinamridhisha ni sawa na uhayawani, heshima yake, familia na hata walio karibu naye nao inashuka kwa kiwango cha juu sana.

Ndio maana hata mwenyekiti wa chama kikongwe mlichorudi kwa vile diplomasia haijui akaamua kuwatukana hadharani kuwa ni ng'ombe mliokatwa mikia hadharani na mbele yenu lakini kwa kukosa aibu usoni mmekomaa kujidhalilisha.

Fred, hata ukiamua kufuga kuku tuu wa mayai unaweza kuishi na bado ukaheshimika.

Ni ushauri tuu mzee mwenzangu.
 
Simamia unachokiamini Vizazi vyako vitakukumbuka hivi mnashindwa hata kumuiga Aboud Jumbe Mwinyi juzi tu kaondoka zake? Hii tabia ya kumsifu mtu hata Kama anachofanya anakosea ni tabia ya wanafiki. Sasa unajipendekeza ili iweje? Kumbuka kuna wenzio umewakuta hapo ccm wewe ni muhamiaji tu unatafuta fursa.
 
Mtoa mada rudi ktk hoja naona unaongelea vitu tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom