Uko wapi siku hizi?; Swali linalotukera vijana ambao hatujafanikiwa na tusio na kazi!

Saveya

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
2,309
2,246
Habari wana bodi,

Moja kwa moja niende kwenye hoja, siku hizi kumekuwa na tabia ya vijana waliosoma pamoja au kukua pamoja zamani, wakikutana mmoja ataanza kumuuliza mwenzie (Mara nyingi ni Yule aliyefanikiwa) kwamba Uko wapi siku hizi?

Hili swali huwa Mara nyingi linaudhi sana endapo anaeulizwa 'yuko wapi siku hizi ' (ikimaanisha unafanya kazi wapi) , ukute ni Jobless hana kazi a.k.a kula kulala huwa linakera sana asikwambie mtu wakuu!, tena Kama ni 'demu ' ukimwambia kwamba wewe ni 'Jobless ' ukichukua number zake ukimtumia meseji hajibu kabisa!,

Wengi wanaouliza swali hilo hutaka Kufanya ulinganisho tu!

---- Michango ya Wadau----

Ni jambo la kawaida kwa watu mliojuana kutaka kujua maendeleo yako, na inawezekana ikawa kwa nia mbaya, lakini si lazima iwe kwa nia mbaya.

1. Kuna watu wanataka kujenga professional network na watu waliojuana nao kitambo, kwao hao ni muhimu kujua nani yuko wapi.Tanzania mambo mengi yanaenda kwa kujuana, ukiibiwa, ukiwa unajuana na Polisi, inakusaidia kuondoa mlolongo wa ukiritimba, utaenda Polisi na kumtafuta mtu unayemjua kwanza akusaidie ku navigate system. Vivyo hivyo kwa daktari etc. Hizi networks zinahusika mpaka kwenye mambo ya biashara pia.Nani ana access na nini, nani anauza nini, nani anahitaji nini etc.

2. Pengine unavyoona kwako kunawaka moto, kwa mwenzio kunateketea.Kuna wengine wanakuuliza uko wapi wenyewe hawana kazi wanataka uwape mchongo, au wana kazi lakini kuna tetesi watapunguzwa, wanatafuta pa kukimbilia.

3. wengine ni watu wa kuwa na data tu ma Al-Watan wanataka wajue habari za kila mtu, nani yuko wapi, ili ikitokea haja ya kutafutana isiwe tabu.

4. Wengine wanataka kuwa na sehemu nyingi za kutembelea na kugonga vizinga wakiishiwa na nauli, wakitaka kutembeza kadi za harusi, wakitafuta ma sponsor etc.

5. Wengine ni kweli wanapenda kujilinganisha. Na hili lisichukuliwe vibaya. Maisha yana changamoto nyingi zinazozaa ushindani. Na ili ukue inahitaji ukubali ushindani. Lakini, ushindani mzuri kabisa ni ushindani dhidi yako wewe mwenyewe, ulikuwa wapi, uko wapi na unataka kwenda wapi. Maana unaweza kushindana na mtu kumbe mwenzako katoka katika ukoo tajiri, au kapata nafasi kwa wizi, au kajiuza mwili. Hivyo si busara kujishindanisha na watu bila data kamili.
 
Maisha watu yamewapiga, tumekuwa na hasira sana mtu ukinihoji naona kama unanikebehi..😃
Na hivi wengine tulivyozoea salamu za Kinyamwezi za peace and love with positivity, hatukawii kuonekana tunajishaua.

Kuna profesa wangu mmoja wa uchumi alikuwa anafundisha uchumi, akiona watu vichwa vinapata moto anatuliza darasa kwa stories.

Siku moja tulikuwa tunaongelea mambo ya unemployment, katika stories zake akasema si uungwana kumuuliza mtu swali "Unafanya kazi wapi?", kwa sababu kama hana kazi unaweza kumtia unyonge au hata kusababisha adanganye.

Sasa hilo swali la "Uko wapi siku hizi?" inabidi kama lina ulazima kuuliza liulizwe kisanii sanii kwa werevu wa kutomuumiza mtu asiye na jibu zuri.

Unaweza kumuuliza mtu swali open ended kupata muelekeo kwanza, kabla ya kufika huko.
 
Wengi ni wale waliofanikiwa kabla yako, huamini labda utabaki hivyo hivyo miaka yote!! Sasa mkikutana au akikuona mtandaoni; anataka ajue ulivyo sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Back
Top Bottom