Uko tayari Ku-'dance'?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,447
39,857
Najua watu walionjeshwa muziki kidogo mapema leo na CD ikatolewa kwa haraka. Hata hivyo kwa wale wapenda miziki ya JF wasikose kesho kwani kuna burudani ambayo inatarajiwa kupakuliwa straight from "studios". Hivyo kwa wapenda muziki you better put your dancing shoes, na vaa gauni lako la mapambo na kina baba suti yako ya tuxedo huku mmeshikana wawili wawili.. for tomorrow (barring matatizo ya kiufundi) we will have another dance; like end of the year dance.. !


Waambie na wengine wasikose mapema kesho a new music (not the one posted here earlier today)..
 
Sasa Mzee Mwanakijiji, sisi wengine tunaomba usituumbue kwa 'kuzima' muziki mapema, in case tukiwa latecomers. Tunaomba angalau iwe ni 24 hours music au hata 12 hours. Alafu iwe time ya kawaida (normal hours) isije ikawa tena usiku wa manane Bongo time!
Mi shajikwatua na niko tayari ku-dance weka CD tuburudike!
 
He he he...Where are my dancing shoes?...:)
 
As a hakuna kiingilio, wahudhuriaji tutakuwa wengi, hata kama kucheza hatuwezi basi tutashangilia watakao toa staili za funga mwaka!

wacha nikasafishe miwani yangu kabisa tayali kwa ushuhudiaji!
 
Huu ni muziki ambao ulitakiwa usikike miaka michache uliyopita lakini tatizo mwenye bendi hakutaka usikike, lakini sasa kutokana na kutokana na bendi mpya kuanzishwa kabla hawajarekodi kibao chao kipya tunataka tuone bendi ya zamani mziki wake ulikuwaje. Msiwe na wasiwasi mwenye CD hiyo atawawekea hapa kesho usiku wa manane kwenye ambao mko mabundi kama mimi mnaweza kujikuta mnaiona usiku usiku na wale wengine ambao hulala wasiwe na shaka wakiamka watakuta mziki unastream live!

I'm tapping my toeas to the beat!
 
Huu ni muziki ambao ulitakiwa usikike miaka michache uliyopita lakini tatizo mwenye bendi hakutaka usikike, lakini sasa kutokana na kutokana na bendi mpya kuanzishwa kabla hawajarekodi kibao chao kipya tunataka tuone bendi ya zamani mziki wake ulikuwaje. Msiwe na wasiwasi mwenye CD hiyo atawawekea hapa kesho usiku wa manane kwenye ambao mko mabundi kama mimi mnaweza kujikuta mnaiona usiku usiku na wale wengine ambao hulala wasiwe na shaka wakiamka watakuta mziki unastream live!

I'm tapping my toeas to the beat!

Naweza kubashiri kibao hicho kitatoka albamu ya Ripo....na jina la kibao kitakuwa Madi....si unajua tena huu uundaji wa bendi zingine unaoendelea bila kwanza kuziba nafasi bendi za zamani?

Nasubiria kwa hamu Asha miye niji mwaye mwaye, nshajifunga kibwebwe
 
Asha, hata mimi siwezi kutabiri licha ya kwamba rhythm yake ni kama naifahamu hivi si unajua tena "bolingo" zote zinafanana fanana?
 
Asha, hata mimi siwezi kutabiri licha ya kwamba rhythm yake ni kama naifahamu hivi si unajua tena "bolingo" zote zinafanana fanana?

Swadakta babu weeh, nitawakaribisha Masha, Mboma, Kipokola au Mang'enya mmoja wao tuje kujivinjari naye. Mwanzo wa ngoma ni lele..

Asha
 
Counterfeiters wa santuri wakijitokeza nitawapa vidonge vyao!!
 
it is coming, kuna tatizo la kuweka hapa bado ma DJ wanatafuta player nzuri.. !


Huu muziki ukitoka, shurti ukae muda takribani usiopungua masaa 24. Maana watu tumekesha ndani ya huu ukumbi kusubiria muziki na sasa wengine tunakaribia kwenda kulala. Tusijeamka kesho tukaambiwa kuwa tulikosa sebene kwani lilipigwa wakati siye tunakula mbonji. Tulolala nasi tupate nafasi ya kuamka na kulicheza sebene. Kazi na dawa, ati.....
 
Hivi nyi mnamwamini Mwanaki-jei-jei? Kweli wabongo ni wepesi kusahau!! Yaani mnamwamini mtu aliyewagandisha hapa kwa masaa kibao akiwaambia atabandika picha za Kikwete na totoz halafu hewa.....kweli nyi mnacheza
 
Tunakesha kusubiri, maana isije ikawa "matatizo ya kiufundi" kama yaliyowakuta ndugu zetu wa Raia Mwema na Tanzania Daima leo, hadi usiku huu tena baada ya KELELE za Mwana Kjj... Haya twasubiri huku tunasinzia......... Maana wengine mabundi, sujui wanga...
 
Kuna post Mwanakijiji alisema muziki tunaosubiri kwa hamu unaendana na makala/habari zilizo kwenye magazeti ya jana ya Tanzania Daima na Raia Mwema. Magazeti hayo tayari yako mtandaoni tunaomba basi huo muziki .... sisi wengine tayari ni alfajiri na sioni dalili ya kuwepo kwa huo muziki!
 
poleni kwa kusubiri, DJ kaniambia atajitahidi leo kwa sababu tatizo ni mrefu kidogo na sehemu fulani fulani hazisikiki vizuri..
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom