Uknown Alergy

August_Shao

Senior Member
Nov 23, 2007
164
47
Jamani naombeni msaada wenu.....Nina miaka yapata 12 sasa nina allergy ya ajabu sana. nimejaribu kutumia dawa lakini sipati majibu mazuri, dawa zote unazozifahamu za allergy hapa dunia nimetumia but still I got nothing.
Tatizo langu ni kwamba kila ninapogusa Maji huwa ninawashwa sana kwa muda wa dakika kama 15 hadi 20. na hii ni kila siku ya Mungu. Sasa naombeni mtu mwenye msaada wowote anisaidie hapa kwani nimemaliza kila aina za medication.
 
pole sana, Tatizo lako kidogo lifanane na langu, lakini mimi siyo mpaka niguse maji, mimi hali ya hewa ikibadilika tu kidogo nawashwa sana kwenye mikono, miguu hadi nitumie dawa ya alergy ndo inapoa. anayejua dawa jamani
 
Mke wangu anatatizo kama lako tofauti yake yeye akienda kuoga baada ya kumaliza kuoga anawashwa kama nipo nachukua kitana au shanuo namsaidia kumkuna mwili mzima lakini sio kila siku ndio maana atujatumia dawa yoyote. yeye akiosha vyombo, akifua nguo shwari tatizo kuoga lakini alergy zipo za aina nyingi, mwezi huu wote shwari.kama wewe ushatumia dawa zote za kizungu mimi nifanyeje? perhaps mitishamba.
 
Jaribu kwenda kwa wataalamu wanaweza kukusaidia vizuri badala ya kubahatisha bila mafanikio!
 
Kupata tiba ya kudumu kwenye matatizo ya allergy sio rahisi. Kinachofanyika huwa ni kupunguza athari kama muwasho, mafua, n.k. So don't try too hard.

Shao, umewahi kujaribu "alternative medicine" yoyote? (I'm just asking)
Have you found anything through googling that gives you even a tiny bit of relief?
 
Pole sana ndugunyangu hata mume wangu anapatwa na tatizo kama lako ila si kila siku. na kwa sasa anajaribu kuobseve kama inatokana na chakula fulani au ni hali ya hewa
 
pole sana ndugu yangu,hii hali imenipata na mimi ila huwa ni wakati wa kipupwe,nyakati za asubuhi huwa na washwa sana usoni kwenye mikona na kwenye mapaja na situmii dawa yoyote,
 
jamani najaribu now ALOE VERA......package nzima yani....Sabuni, Gel and Juice....halafu kitu ambacho nimeweza kukiona baada ya research yangu ya muda ni kwamba kabla ya kuenda kuoga unatakiwa kupakaa hii Gel just before shower sehemu ambazo huwa zina washa......I tried it today nimeona kama kweli inafaa but let me continue with this then nitatoa muafaka kama dawa imepatikana au bado.....please keep researching GUYS
 
Pole sana ndugu! mimi nahisi pengine ni maji ya eneo unaloishi ndo yana some chemicals ambazo hazipatani na mwili wako, je umeshawahi kutumia maji ya aina nyingine unaweza kujaribu kutumia mineral water (japo ni ghali) ili kuweza ku estabish kama nia aina ya maji au ni kitu tofauti. Some times mabomba tunayotumia pia yanatoa ainafulani za madini ambayo haipatani na miili yetu,au hatakujenga some fungus ambazo pia ni hatari.
Lakini pia wakati mwingine unaweza kuwa una react na chlorine ambayo inatumika ku purify maji yetu ya bomba.
Kwa mtu mwenye allergy ni vizuri akijua kinachomsababishia reaction (allegen) ili akiepuke na hiyo ndo tiba ya kudumu.
 
Jamani naombeni msaada wenu.....Nina miaka yapata 12 sasa nina allergy ya ajabu sana. nimejaribu kutumia dawa lakini sipati majibu mazuri, dawa zote unazozifahamu za allergy hapa dunia nimetumia but still I got nothing.
Tatizo langu ni kwamba kila ninapogusa Maji huwa ninawashwa sana kwa muda wa dakika kama 15 hadi 20. na hii ni kila siku ya Mungu. Sasa naombeni mtu mwenye msaada wowote anisaidie hapa kwani nimemaliza kila aina za medication.

JAMANI DAWA NIMEPATA ATLAST KWA MIAKA 12 YA MATESO.
medication:

1. Nilifanya maombi kwa Mungu kwa kufunga
2. niienda kwa daktari akanipa dawa na kunikataza baadhi ya vyakula, na ukienda kupima allergy utakuta huna allergy yeyote ile.
food restricted
.PORK
.WHEAT
.EGGS
.MILK
.SEAFOOD
DAWA ZA KUTUMIA
1. CLARITINE - LORATIDINE 10MG
2. TENOMET 400- CIMETIDINE BP 400MG, REMEDICA - CYPRUS

PLEASE USINYWE DAWA BILA KUPIMA AFYA YAKO KWANZA.......MIMI NIMECHECK DAMU YANGU KWANZA...FULL CHECK-UP
 
Back
Top Bottom