Ukizubaa kidogo tu ushakatwa... Si unaona!!

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Habari wana JF............poleni na shughuli zakujenga taifa letu.

Dunia tambala bovu walisema wahenga wetu na leo nimeamini hili........Dada mmoja alikuwa na shoga yake kipenzi anayemuamini kwa kila jambo,lakini alichomtenda haamini mpaka kesho kama peponi au laah.

Alikuwa na mume wake kipenzi waliyefunga ndoa kanisani kabisa tena kwa shangwe na nderemo lakini allikuja kuchukuliwa na huyo shost yake {bonge la nyau}wakati walikuwa wana share vitu vingi sana si unajua tena mambo ya ushost na pia huyo mwizi wa bwana hakuwa vizur kiuchumi kwahiyo hata financial support alikuwa anaipata.

Yule mwizi allikuwa mwanafunzi wa chuo fulani hapa mjini,mwanaume kauvaa mkenge akawa hasikii wala haoni kabisa.Nyumbani harudii mpaka hostel za wanawake analala hapo chuo na huyo demu.

Mke alisikia habari za huyo mumewe na shost yake lakin alipojaribu kumuuliza bwana mkubwa ikawa utata sana..........Haikupita muda sana yule jamaa alilala nje tena na demu hapo hostel...........mke anampigia simu jamaa anakata,baadae akapokea simu yule lakin mkewe akawa analalamika na kumwambia anajiua.Mume akamwambia we jiue tu ukitaka!!!!!

Yule dada alijiua.............mumewe alipokea simu usiku kutoka kwa majirani baada ya binti wa kazi kutoa taarifa hizo,jamaa pombe zilimuisha akaacha papuchi na kkurudi hom na akalia mpaka kuzima msibani.

Navyoongea leo nimemuona yule demu mwizi kachakaa kama mpira wa makaratasi.............nadhani pia watakuwa wameachana.

UKIZUBAAAA KIDOGO TU TAYARI USHAKATWA..................SI UNAONA mambo ya eatel maneeeeeeeeeeeeeee!!!!!
Muwe makini wanandoa..............,tusiamini mtu kupita kiasi moyo wa mtu ni msitu wenye kiza kinene hatujui anakuwazia nini!!!!!!!!!!!!
 
Mjini hakuna ushoga.
Ushoga mwisho mkata.
Ndugu zako tu bwanako akiwa na hela watajitongozesha sembuse rafiki.
Nani anataka kupigwa na jua?
Aaaaa mjini akili bibi eeeeee kama huna akili kila siku utalia rariiiiiiii
 
kujiua is against religious teachings and its the 'easy way out'. ukipata changa moto jikaze kiume na uombe Mungu akusaidie
 
Mjini hakuna ushoga.
Ushoga mwisho mkata.
Ndugu zako tu bwanako akiwa na hela watajitongozesha sembuse rafiki.
Nani anataka kupigwa na jua?
Aaaaa mjini akili bibi eeeeee kama huna akili kila siku utalia rariiiiiiii
we dada wewe.
 
Duuuuuu pole yake huyo Dada Aliyeamua kukatisha maisha yake kwa ajili ya penzi...wengi katika ulimwengu wa leo wanatendwa katika mahusiano...la muhimu ni walimwengu tubadilike na kuwa na hofu ya Mungu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom