Ukizima moja zinazima zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukizima moja zinazima zote

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 17, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Ukizima Moja, Zote zinazima!  [​IMG]
  Mwanaume na mwanamke wapo tofauti zaidi kuliko kufanana na hivyo ndivyo walivyo, kukataa haiwezi kubadilisha ukweli.
  Mwanamke na mwanaume husikia na kuona vitu kwa utofauti mkubwa acha suala la chumbani.
  Sasa fikiria mume na mke ni electric circuit, na circuit ya kwanza ina taa (bulb) 3,000 na mfumo wake ni kwamba ukizima bulb moja unasababisha bulb zote 2,900 kuzima.
  Na circuit ya pili ina bulb 3,000 pia na ipo designed kwa namna ambayo ukizima bulb moja, zingine zinaendelea kuwaka, ukizima bulb 2,000 bado zilizobaki 1,000 zitaendelea kuwaka.
  Mwanamke ni sawa na electric circuit ya kwanza kwa maana kwamba kukiwa na conflict eneo moja la ndoa au maisha mwanamke hufunga system nzima ya mwili wake (bulb moja ikizima zote zinazima) kwani feelings za mwanamke zimeunganishwa (integrated system) na kuingiliana mwili, roho na nafsi, hii ina maana akiumia roho na mwili unaumia na nafsi inakuwa imeumia.
  Hii ina maana mume akifanya jambo moja linalomkera mke; mke atajisikia hapendwi na mume hamjali (bulb zote zitazima) hadi matengenezo ya mwanaume kuwa wazi na karibu ndipo anaweza kurudi kwenye hali ya kawaida na si kuwambia let’s forget it eti ndo umemalizana naye.
  Kumbuka somo la spaghetti
  “If she is in a battle with him in one area, she is at war with him in all areas”
  Kila mwanaume na afahamu kwamba:
  Kama mke anajisikia kuna tatizo katika eneo moja la maisha (kuumizwa, upweke, kukataliwa, kuchoka, mawazo, kukosa upendo, kutoheshimiwa, hasira nk) hukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
  “When her spirit is crushed, her body is not available”
  Wanaume huweza operate kama vile hawana feelings au tatizo, hata wanawake hulalamika kuhusu hili.
  Kwani yeye ikizima bulb moja bado zinazobaki hupendelea kuwaka, hata ukizima zingine nyingi bado bulb zilizosalia hupendelea kuwaka.
  Hii ina maana mwanaume ni mfano wa box kiasi kwamba hawezi kuhusanisha tatizo moja na lingine kwake mwili ni kitu kingine, roho ni kitu kingine na nafasi ni kitu kingine.
  Ndiyo maana mwanaume anaweza kuwa katika mgogoro katika eneo moja la maisha na asiathirike chochote.
  Ndiyo maana kukiwa na mgogoro kati ya mke na mume bado mume anaweza kuhitaji tendo la ndoa bila tatizo na akajisikia vizuri tu kushiriki.
  MBILINYI.BSPOT.COM
   
 2. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,149
  Likes Received: 23,848
  Trophy Points: 280
  Mambo ya series na parallel circuits sasa!.
   
Loading...