habari ni kweli ila baba h kuwa na utu ss sio mahakimu cha msingi ni kumtakia mema mwenzetu sisi tiko kwenye safari na hatujajua mwisho wetu utakuwaje.
tumuombe mola atupe mwisho mwema hilo ndio la kuomba na sio kufurahia na kukejeli msiba wa mwenzetu
Kuna waliokufa na wana vitu vya kuigwa, sio huyu jamani!Kifo cha Ditto hakiwezi kumrejesha yule dereva duniani au kufuta hasira za wanyonge dhidi ya upindishwaji wa makusudi wa sheria ili kumlinda.
Vivyo hivyo kumshambulia Marehemu Ditto (Kama kweli kafa) hakuwezi kubadili hayo yaliyojitokeza sana sana itaonyesha wale walioshiriki kudhulumu haki ya Dereva wa daladala ambao bado wapo hai kuwa kitendo walichofanya hakikuwa cha kiungwana na kiliwakera wengi
Kufa kwa Ditto si kitu cha ajabu wala si topiki ya kujadiliwa hata sasa hivi tunapojadili hapa watu wengi tu wameshakufa ila kinachofanya watu wajadili hapa wanamjadili kama kiongozi aliyestahili kuwa kioo cha uadilifu na si kama mtu binafsi
Huyu si mtu wa kwanza kujadiliwa hata viongozi wakuu waliojijengea heshima kama Julius na Abeidi Karume wanajadiliwa hadi hivi sasa
Kujadiliwa kwa kiongozi katika jamii kwa mwelekeo hasi au chanya inategemea na mchango wake katika jamii husika.
...moja ya sababu kuu za kummaliza mtu mwenye kisukari n presha ni ongezeko la mapigo ya moyo[msukumo wa damu] ..inaweza kutokana.. TENSION[MAWAZO,KAZI NYINGI],MATUMIZI YA DAWA AU KITU CHOCHOTE KINACHOWEZA KU STIMULATE MAPIGO YA MOYO KUWA JUU[STIMULANTS]..Ie CAFEINE,VIAGRA ets
Ya Dito inasikitisha sana. Amefariki kwa shinikizo la damu leo saa mbili asubuhi akiwa hotelini, Morogoro, tena akiwa anaangalia TV.... mwili wake unasafirishwa leo mchana huu kuelekea Dar es Salaam ambako utapitishiwa hospitali ya jeshi ya Lugalo, kabla ya shughuli ya mazishi kuendelea nyumbani kwake Upanga, Dar es Salaam. Ina Lilalh Waina Ilaihu Rajiun
Kuna waliokufa na wana vitu vya kuigwa, sio huyu jamani!
Alikuwa mkorofi twamjua weka mahala pema peponi, alikuwa muuaji twamjua weka mahala pema peponi, alikuwa mhuni twamjua weka mahala pema peponi.
Hiyo mbingu ni ya wanadamu ama ya Mungu? Mbona mnataka kuleta vichekesho. hapo mahala pema peponi ni pa wanadamu ama patakatifu pa Mungu?
Ndio maana maradhi ya namna hii, pamoja na 'stroke' yanaitwa Silent Killers'kwa maana huwezi kujua dalili wala wakati. Kifo kinaweza kuja ghafla tu, wakati ulikuwa na dalili njema tu kabla ya hapo.
Ndio maana, inasisitizwa sana watu muwe mnapima afya zenu mara kwa mara, angalau mara moja kwa mwaka, hata kama hujisikii kuumwa.
Hili ndilo tatizo letu hapa nyumbani, kuweza kuwafikishia wananchi huduma za afya ili na wao wapate kujilinda na magonjwa ya namna hii.
vifo vingine vinastahili kufanyiwa sherehe. Is he really dead? Maana yule mtoto wa mjini.