Ukiwa una ratiba kuna haja ya kuwa na to do list

x - mas

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
915
598
Habarini mageat thinkers. Wataalamu wanashauri ni vema kabla ya kulala kuhakikisha unaandaa mpango wa kazi au kuaandaa mambo ambayo utafanya siku inayofuata, Napata ukakasi kwa mtu ambaye anaratiba yake binafsi ambayo ndio mwongozo wake wenye majukumu yake yote ambayo anatakiwa kufanya kwa wiki ikionyesha mpangilio wa mambo yote anayotakiwa kufanya kila siku kwa vipande maalumu vya muda, naweza fananisha na ile ratiba ya wiki ya masomo darasani.

Je,kwa mtu kama huyu kuna haja ya kukaa na kupanga to do list ya siku inayofuata? Nimepata utata baada ya kusoma kitabu ch EAT THAT FROG cha Brian Tracy ambacho kimesisitiza kuwa na list ya majukumu ya kufanya kwa siku inayofuata katika list hiyo mtu anashauriwa kupanga mpangilio uanze na mambo muhimu kwanza yaani mambo ambayo nilazima yafanywe kwasababu kufanywa au kutokufanywa kwa mambo hayo athari za matokeo yake ni makubwa katika maisha ya muhusika.

Maisha yetu yanaongozwa na ratiba kati ya hizo ratiba zingine hatuzipangi sisi mfano ratiba za kwenda kazini kwa maana hiyo utaona kuna mambo mengine ni muhimu sana lakini kwa mujibu wa ratiba jambo ilo linatakiwa lianze kufanywa mwishoni mwasiku mfano kuanzia saa kumu alahasiri tayari hapo kuna kuwa na kupingana kati ya ratiba na ’to do list.’’ To do list’ inakutaka kumaliza mambo muhimu kwanza kasha uanze na mambo muhimu kiasi na mengineyo lakini ratiba ina kusubirisha hadi saa kumi wakati asubuhi inakuacha na muda wa kutosha,hapa ni kwa zile ratiba ambazo tunapangiwa na mamlaka.

Karibuni tupeane mawazo hapa inawezekana kuna mahali nimemisunderstood.Napenda sana kufuata ushauri wa kitabu lakini nashindwa kubainisha kati ya ratiba na to do list naona kama kunamkanganyiko kidogo.
 
To do list, naratiba yako ya siku?
Hem nitofautishie hii misemo mm sjaelewa vizuri maana hasa na kusudio.
 
To do list, naratiba yako ya siku?
Hem nitofautishie hii misemo mm sjaelewa vizuri maana hasa na kusudio.


nikwamba ratiba ni orodha ya shughuli ambayo hutengenezwa na mtu binafi au mamlaka fulani kwa lengo la kuonesha shughuli ambazo zinatakiwa kufanywa kwa kila siku za wiki ikionesha na muda wa kufanywa kwa kila shughuli kwa kawaida ratiba inakuwa imeandikwa na kuifadhiwa au kubandikwa ukutani sehemu ambayo ni rahisi kuonwa lakini to do list ninayozungumzia ni ile orodha ya mambo yakufanya siku inayofuatwa tunyoshauriwa kuiandaa usiku kabla ya kulala.
utaona tayari mambo ya kufanya hapo tayari yapo kwenye ratiba sasa kuna haja ya kuandaa to do list? hapo hata mimi nikahitaji mawazo kutoka kwenu uwenda naelewa vibaya hizi term.
 
Tutumie soft copy ya kitabu hicho, Brian Tracy yupo vizuri sana



softcopy ninayo ilanashindwa namna yakuituma humu nifundishe au jaribu kugoogle eat that frog kisha fungua link ya kwanza kutokea.
 
Back
Top Bottom