Ukiwa na tabia ya kujifananisha na watu, jua mtoto wako hatofanana nawewe

Kulupango

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
288
534
Ukiwa na tabia ya kuiga muonekano wa mtu fulani, au muondoko wa mtu fulani, au kuiga kuzungumza kama mtu fulani, au kuiga mapozi yake ikiwemo kuiga kucheka kwake, kukasirika kwake, kufoka kwake nakadhalika. Haswa ikiwa ni mtu ambae hauna nae nasaba moja (yaani sio ndugu yako kwa vyovyote vile) lakini wewe unapenda kuiga mambo yake, elewa ukija kuzaa mtoto huenda usifanane na mtoto wako.. haswa tabia hii ukiwa unaifanya kwa watu tofauti tofauti (yaani unaiga watu tofauti tofauti). Wengine husema kwamba vinasaba (genetic) huchanganyikiwa kwasababu kuiga kunaweza kupelekea ufanane na mtu unae muiga. wengine husema ni mambo ya imani na mila. Hivyo basi unatakiwa kuishi wewe kama wewe nasio kuiga masauti au matendo ya miili ya watu. Ukizaa mtoto hafanani nawewe usije kusema sio mtoto wako.
 

Attachments

  • IMG-20200425-WA0001.jpg
    IMG-20200425-WA0001.jpg
    16.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom