Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Rich people buy income generating assets,middle class buy Liabilities thinking they are Assets(eg.cars,exp television set,bling bling etc),poor people live in debts.Je uko wapi kijana mwenzangu?
 
Maisha ni kujipanga na kujipanga ni kuamua! Hakuna formula ya maisha, ndio maana wakati mwingine maisha ni bahati ya mtu. Unaweza kuanza kwa kujenga halafu vingine vikafata au ukaanza na gari halafu nyumba ikafata, whichever is excellence!

Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi

Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu

BAADA YA KUONA SIELEWEKI, NIMEONA NIWAPE MFANO HUU.

Hapa Tanzania, Wahindi wamekuwa waoga kujenga Tanzania kwa hofu kuwa labda hapa si kwao. Wahindi wanaishi National Housing kwa kupanga, ni mabillionaire, wameshika uchumi wa nchi hii, hawatishwi na kodi za nyumba, mfano kwa Arusha wanalipa kodi hadi 1.5m kwa mwezi kwa nyumba ambazo si national housing huko Arusha.
Sasa vipi wewe Mtanzania ungeanza na biashara then Nyumba?[/QUOTE]
 
Pia Inategemeana na ulivyo jipanga co kila mtu huwa huwa na maisha ya middle class mungu ndiye muweza wa yote
 
Ndio maana watanzania ni wezi maofisini, kwasababu mshahara wote wamekopea na kuinvest kwenye vitu visivyozalisha!
 
Hata usemeje,lazima nitanunua kiwanja na nitajenga nyumba yangu mimi mwenyewe,
Usipende kuwakatisha watu tamaa,Maisha ni jinsi unavyoyachagua

hapo kwenye bold umesema ukweli kabisa,maisha ni jinsi unavyochagua coz unaweza hata kuchagua kuwa maskini aidha kwa kujua au kwa bila kujua.tatizo letu wabongo mtu akishapata kazi,atawaza kujenga,baada ya kujenga atanunua gari,baada ya gari anabakia kuwaza ni jinsi gani atastaafu.atakuwa anakimbizana na muda wa kustaafu ili awe ameshasomesha watoto.yaani utadhani maisha mwisho wake ni kustaafu.anaanza hivi,mkopo wa kwanza ananunua kiwanja,atakatwa miaka minne,ukiisha anachukua tena anaanza kujenga,anajibana bana hadi akimaliza nyumba(iwe ya standard kuishi)ni bbada ya miaka nane hadi kumi baada ya kuanza kazi.anakopa tena ili anunue gari,unakuta baada ya miaka kumi na nne ndo kamaliza nyumba na gari.imagine,kama hiyo mil 5 alizokopa kwa mara ya kwanza akaanza uwekezaji ambao ungekuwa ukimuingizia hata mili moja na nusu kwa mwezi,ok,walau hata mil moja tu.ina maana baada ya mwaka anakuwa na mil 10 faida.yaani inakuwa ni mara mbili ya ile aliyokopa.ina maana kwa spid hii akiamua kujenga na kununu gari ni ndani ya miaka mitatu tu.

haya ni makosa ambayo huwa tunayafanya kwa kukosa ushauri,unachukua hela unaizika halafu tunabaki tunalia umaskini.yaani mawazo yetu yanaamini hatuwezi kuwa kama mengi au bhakressa,yaani utadhani utajiri huwa ni wa watu flani tu na sio sisi,sisi tunapaswa kusulubika hadi kustaafu then tunaanza kuwabana watoto ndio wawe wanatutimizia mahitaji yetu.tofauti na wenzetu wao wanataka ndio wawe wanawapa watoto wao support mpaka watakapokuwa stable,lakini sisi ni kinyume
 
:A S embarassed::A S embarassed:mhhh...lets not justify thngs easily...eti biashara kwanza...mara ooh eti nchi zingine hawaruhusiwi kujenga kwanza.Ukweli ni kwamba ukijenga mapema u can do the rest peacefully...gari na biashara.Biashara zenyewe za bongo grocery,T/pesa,MPESA na nguo feki na lazima uwe na frame stand za magar(mwenge/kkoo/ubungo etc) otherwise utakua unapiga marktym tu na kulipa kodi isiyo na mrejesho,turn over ya vijana wengi hata mil 20 haifiki ndo ujishaue kuanzisha kabiashara-mara kanakufa na bank wanaendelea kulamba mkopo wao.vijana wenyewe wakiona kipindi cha ujasiriamali wanabadili channel.Jengaa...kaa kwako jibane kula mchicha kusanya mtaji...anzaa biashara iki-takeover weka nyumba rehani ongeza capital -the rest wll serve for themselves.
 
Mada nzuri sana hii nadhani itawasaidia watanzania japo wengi wamesoma na bahati mbaya hawajaelimika na mbaya zaidi ni wabishi na hawataki kutembea nchi zingine wakaona.....Kimsingi kama umeajiriwa na mtu/kampuni ujue hapo upo haupo. Kitu cha kwanza hakikisha unaanza kujiajiri kwanza ili upate uhakika wa kipato chako na baada ya hapo ufanye mambo mengine ambayo hayazalishi bali yanatoa. Jaribu hata kununua HISA potelea mbali hata kama utapata loss. Loss katika biashara ni changamoto so usikate tamaa bali tafuta namna ya kupambana nayo......ni rahisi kuvumilia loss ukiwa na kazi lakini mradi wako ukisimama basi ondoka katika kazi hiyo ili wadogo zako pia wapate nafasi lakini kwa kuanzisha mradi utakuwa pia umetengeneza ajira kwa wengine na wewe pia...hii tabia ya kila mtu kufikiria kuishi kwa kuajiriwa tuuu ni kikwazo kwa uchumi wa taifa pia.
 
Mimi nawajua rafiki zangu wengi tu ambao wamejenga lakini hata hawaishi kwenye nyumba zao maana wanahamishwa hamishwa kikazi Baba na mama..hii eti umeajiriwa unajenga ili ukae kwako!!!?? ukihamishwa?
 
Ni ukweli usiopingika kwamba investment can make someone's economy to grow kuliko kujenga Nyumba Na kununua Gari la kutembelea kabla ya kuwa Na uchumi ulioimarika maana vyote hivyo havizalishi, lakini bado inategema kidogo Na nature ya kazi ya Mtu anayefanya, Mtu mwingine angependa awe Na Gari ili limsaidie aweze kufanya kazi Yake vizuri. Swala la kuwekeza ni zuri lakini lina changamoto kwambwa wapi pa kuwekeza, fursa za kuwekeza mbali na kufanya biashara haziko wazi sana kwa kila kijana/mtu kuziona.
 
maisha ni hesabu zako mwenyewe,maisha hayana kanuni kila mtu na stepu yake kamwe ucjaribu kuiga staili ya mwenzio...
 
Tuombe uzima ndugu zangu baada ya miaka 20 tutajua upande gani ulikuwa sahihi.....mi naamini kwa wale ambao wanaamimni kwny kununua au kujenga vitu ambavyo havizalishi watakuwa kwny waist mgumu sana
 
hapana maisha ya mjini ni ghali hasa upande wa kodi.kama una sehem ya kuishi vitu vingine ni.ziada.kwa mtazamo wangu mm naona nyumba kwanza vingine baadea sana
 
Kakak unajaribu kuelezea maisha in one simple way or two. Lakini kwani hatujaishi long enough kujua kwamba hamna kanuni au njia ya kuelezea maisha kwa maelezo machache au hata mengi... hivi kwani kila anaefungua biashara inafanikiwa? na ikifanikiwa asijenge ainvest zaidi?. Hakuna mali hapa duniani kama ardhi kaka, na pia kuwa na sehemu unayoweza kukaa kwa amani kunakusaidia kufocus katika mapambano yako... japo hata nayosema hapa sio haitoshi kuelezea maisha.... But kwa ushauri wangu mtu ambaye ni kijana akaweza kujenga na akawa na nyuma akiwa kijana anachances zaidi ya wewe unatakiwa kulipa kodi kila mwezi. As akimaliza nyumba yake wewe na yeye mnakuwa mpo katika race hiyo hiyo ya mafanikio....
 
Wadau, hasa vijana wenzangu, Ushauri kwa vijana wenzangu. Ukiona wewe kwanza ndiyo umepata kazi, ukaanza kwa kununua gari la kutembelea, baada ya hapo ukanunua kiwanja na ukaanza kujenga ujue wewe utaishia kuwa middle class na kuteseka ki uchumi katika maisha yako yote. Ninaposema kuteseka ki uchumi namaanisha kila ikihitajika laki moja wewe kuitoa mpaka ukope au ukitoa unaishiwa. Vijana wengi wanapenda kuishi maisha ya luxury wakati hawana sifa ya kuwa na luxury, unakuta ndani kwake kajaza vifaa expensive wakati hana rasilimali ya kumpa kipato, wengi wanafanya hivyo ili waonekane wako na maisha safi kwa jamii, kumbe wanajichimbia kaburi Asilimia kubwa ya middle class walieanza kwa ku invest kwenye mambo yasiyozalisha, mfano nyumba ya kuishi mwenyewe au gari, ukianza, ukianza kwa kujenga nyumba ya kuishi wewe ndio mbaya kabisa. Watu tunaowaita matajiri, walianza kwa ku invest kwenye kitu kinachozalisha pesa then gari la kutembelea, nyumba vikaja baadae. Huo ni ushauri wangu kwa vijana wenzangu BAADA YA KUONA SIELEWEKI, NIMEONA NIWAPE MFANO HUU. Hapa Tanzania, Wahindi wamekuwa waoga kujenga Tanzania kwa hofu kuwa labda hapa si kwao. Wahindi wanaishi National Housing kwa kupanga, ni mabillionaire, wameshika uchumi wa nchi hii, hawatishwi na kodi za nyumba, mfano kwa Arusha wanalipa kodi hadi 1.5m kwa mwezi kwa nyumba ambazo si national housing huko Arusha. Sasa vipi wewe Mtanzania ungeanza na biashara then Nyumba?
ya kweli hayo
 
Na unajua uhalisia wa hapa tz kwetu? Sio kila mtu anapanga national housing!. Na kama unaenda kupanga kwa middle class mwenye nyumba then unasema umemzidi akili haileti maana kidogo.... Na narudia mimi namsupport kijana anayeweza kujange angali kijana hakosei kama jinsi atayeamua kila senti anayoipata kuinvest.... :A S 465:
 
Kijana mwenye uwezo wa kurudi nyumbani kwake kachoka na mihangaiko ya maisha na kurudi kwake kupumzika ni bora mara 1000 ya kijana mwenye kurudi nyumba alopanga.... Japo biashara au kuinvest sio wazo baya... hakuna formula....
 
Sio lazima walojenga kwanza wawe na wakati mgumu, japo najua hata kama watabaki middle class watakuwa na afadhali kuliko waliinvest na kufilisika... Ukiwa na uwezo jenga, kuwa na ardhi na nyumba sio a negative development ni one step ahead. Kama ulivosema wahindi hawajengi hapa wanaogopa si kwao wasingehofu wangejenga pia.
 
sidhani kama kuna ukweli, maisha ni kujipanga na kupanga ni kuchagua. nyumba na gari nayo ni mahitaji ya msingi sana tu ya kuanza nayo kama hukuwa navyo na haijalishi ununue vya kwanza au vya mwisho, jitihada binafsi ndio muhimu zaidi
Husninyo my dear... Mleta madam is dead right

Jitihada bila strategies ni sawa na kuongea sana ili upunguze kitambi

You should know tactics in life to make to higher level

Cash is the biggest assets any Tanzanian can ever have
 
Kijana mwenye uwezo wa kurudi nyumbani kwake kachoka na mihangaiko ya maisha na kurudi kwake kupumzika ni bora mara 1000 ya kijana mwenye kurudi nyumba alopanga.... Japo biashara au kuinvest sio wazo baya... hakuna formula....
Teh Teh Teh Teh.. Jidanganye na unyerereist

Capitalism is way different
 
Hamna njia utaelezea na ikawa ndo njia ya mafanikio.... success1.jpg
 
Back
Top Bottom