PostGE2025 Ukiwa na mikono yenye damu, meza ya maridhiano inakukataa automatically

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam!

Asomaye na afahamu,

1. Mfalme Daudi alipenda sana kumjengea hekalu Mungu Ili Sanduku la AGANO lipate pa kukaa, akasahau kuangalia mikono yake ilivyojaa damu, ombi lake likakataliwa, mwanae Mfalme Suleimanmwenye mikono safi ndiye akaja kupata ridhaa kujenga hekalu.

2. Hitler, Idd Amin na madikteta wengineo, wangependa sana kuridhiana na wananchi wao Ili kurejesha amani ila damu mikononi mwao ilikataa. Damu huwa ina tabia ya kudai kisasi.

WAY FORWARD.

Viongozi kagueni mikono yenu, pakiwapo damu, Sheria ya asili inakataa watu wenye damu mikononi kuja meza ya amani ya maridhiano. Kukimbilia washroom kuosha mikono kamwe hakujawahi kuondoa damu maana damu ni uhai, ni nafasi, haifutiki.

Wenye haki ya kuwaleta watanzania Katika meza ya maridhiano ni watu na viongozi wasio na Damu mikononi wapo na wanajulikana. Mauaji ya kimbari hayakumalizwa na viongozi waliokuwepo, watu wapya ndio walikuja kuleta maridhiano na kuleta TOBA ya haki ndipo kukatulia.



Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha.
 
Tundu Antipas Lissu,ninakuombea usikubali dhambi hii kukubali kukaa na wenye mikono yenye damu mbichi.

Mungu akulinde.
 
Naunga mkono hoja, kuna umuhimu wa kupata viongozi waadilifu na walioelimika, ukifuatilia umwagaji damu wakati usiokuwa wa vita, zaidi unafanywa na watu wenye ufinyu wa elimu mfano Idd Amin Dada, Saddam Hussein, Joseph Stalin na Adolf Hitler.
 
Jitu limechinja Watanganyika 23,000 halafu leo linarembua macho kutaka maridhiano.
Akiweza kurudisha uhai wa aliohusika kuwauwa ndipo maridhiano yatafana.

Tufauti na hapo, akubali nao wamuue Ili waipate haki.

Akishindwa Hilo, atokomee gizani,

Waje wengine kuleta maridhiano ya haki.
 
Kwa hiyo unamtaka Tundu na Kitima na Heche ndiyo waandae maridhiano?? You are joking!!

Nyinyimetaka luchoma nchi tarehe 29/10 na tunajuwa mlikuwa na ushirikiano kati ya CHADEMA, Gwajima, Maria Sarungi na MangeKimambi katika kupnga na ku-finance Qakenya wa kuanzisha fujo za uharibifu ili Watanzania wadandie kwenye huo uhayawani.

Kama hamtaki maridhiano KWENDRAAAAA
 
Kabla ya October 29 muda ulikuwepo wa kutosha kufanya maridhiano.

Muda huu kwa waliopo umewatupa mkono.
Bado nafasi wanayo, ila Kiburi ni kikubwa sana.

Mtu isipomfaa akili yake, basi utamdhuru Ujinga wake.

Tuwape Muda, may be watajifunza kwa vitendo.
 
Wa Tanzania tupo tayari kuchangishana kufidia hasara iliyosababishwa na maandamano,

Ila shart ni moja tu, Samia arudishe hai roho za waliouwawa.

Swali: Roho ya mwanadamu waeza ilinganisha na pesa na Mali?
 
Wa Tanzania tupo tayari kuchangishana kufidia hasara iliyosababishwa na maandamano,

Ila shart ni moja tu, Samia arudishe hai roho za waliouwawa.

Swali: Roho ya mwanadamu waeza ilinganisha na pesa na Mali?
Waliouawa ni haki yao kwa ule UHAYAWANI walioufanya. Hizo roho hatuzihitaji kabisa kuishi nazo.

Unaanzaje kuchoma miundombinu ya serikali kama vituo vya polisi, mahakama, vituo vya mafuta? Hustahili kuishi na sisi
 
Waliouawa ni haki yao kwa ule UHAYAWANI walioufanya. Hizo roho hatuzihitaji kabisa kuishi nazo.

Unaanzaje kuchoma miundombinu ya serikali kama vituo vya polisi, mahakama, vituo vya mafuta? Hustahili kuishi na sisi
Kwa hiyo Master Tindwa, Sheikh Sharif Majini, yule mama wa Arusha aliyepigwa risasi ya mgongoni, binti wa miaka kumi na mbili aliyeuawa akalala na bango lake la "no reform no election"(limeandikwa maandishi mekundu) au kile kichanga cha miezi sijui sita, kilichopigwa risasi kilipokuwa chumbani kimelala kitandani? Na wengineo wengi waliofuatwa majumbani mwao walichoma miundombinu?

(Hata kama walichoma adhabu ni kifo kwa kuchoma makorokoro tunayoweza kujenga upya, vipi kuhusu uhai wao mtaurudishaje?) Na je, hawastahili kuishi na wewe chawa? Ni haki yao kuuawa bila kufikishwa mahakamani watu waliokuwa wanajiokoa kwa kukimbia? au visasi? Vipi kuhusu wategemezi wao kwenye familia wamewaachaje? Vipi, kuhusu ubakaji au ufiraji uliofanyika yakitendeka yote hayo? Kuna mambo yanashangaza sana?
 
“Kidole Cha Kati”

Unaandika kama vile umekalia kipande cha nyama ngumu,em hapo ulipokaa simama jitizame kwa nyuma kama hujalowa.
 


Itatangulizwa hela hapo....wewe acha tu badala ya hiyo hela kutumia kutoa fidia kwa wahanga wa mauaji wanaenda kupewa kina Jaji Chande na wenzake waendelee kula Mema ya nchi na kuendelea kustaafu vizuri
 
Waliouawa ni haki yao kwa ule UHAYAWANI walioufanya. Hizo roho hatuzihitaji kabisa kuishi nazo.

Unaanzaje kuchoma miundombinu ya serikali kama vituo vya polisi, mahakama, vituo vya mafuta? Hustahili kuishi na sisi

Hahaha, Na yule alie uza bandari, Mbuga na Migodi kwa bei ya kutupa tumfanyaje sasa.

Au yeye Anyongwe Hadharani 😌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…