Ukiwa mwongo sharti uwe na kumbukumbu

SI unit

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
1,953
766
Madogo wa primary wakiwa mapumziko wakawa wanapiga stori.
Dogo 1: Kijijini kwa babu yangu kuna ng'ombe mkubwa ana"cover" eneo lote la kijiji, duniani hajawah kutokea ng'ombe mkubwa hivyo.
Dogo 2: Hiyo chamtoto, kijijini kwa babu yangu kuna ngoma kubwa wakikaa wanakijiji wote wanaenea juu yake.
Dogo 1: Aaaaaah! Hakuna kitu kama hicho, haiwezekani kabisa. "Rungu" hilo nakwepa, vuuuu..um..
Dogo 2: Dah! Kwani umesahau yule ng'ombe wa kijijini kwa babu yako alichinjwa na ile ngozi ikanunuliwa kijijini kwa babu yangu ndo wakatengenezea ngoma?
 
Back
Top Bottom