Ukiwa hivi wanawake lazima wakupende

Ukiwa hivi wanawake lazima wakupende

Nina ushahidi binafsi ...

Wakati nikiwa kijana ....
Kulikuwa na mrembo hivi alikuwa akiwatolea watu wengi nje. Nilipoonana naye nikawa naongea naye kwa mara ya kwanza, wenyeji wa pale walinambia najisumbua wala siwezi pata kitu. Niliwambia kuwa nimezaliwa kuweza na ni lazima nitaweza.

Nilichokifanya nilibadili mfumo wa maongezi na badala yake nilianza kuwa naye sehemu ambazo haziruhusu kutenda mambo hayo (sex).

Baada ya miezi kama sita hivi, yeye ndo alianza kunionea wivu kwani alitamani muda mwingi niwe naye. Alijenga mazingira ya kila Jumapili kuja nyumbani. Tulizoeana na ndugu na marafiki zetu walitufahamu kama marafiki (sio wachumba wala wapenzi).

Siku ya siku nilipojaribu tu ... ilikuwa kama kumsukuma aloinama.
Mkuu miezi yote hiyo sita![emoji23] [emoji23] unahujumu muda wa Taifa
 
Habari wakuu!

Moja ya mambo ambayo wanaume wanapenda katika dunia hii ni kupendwa na wanawake.
Bila kujali mwanaume ameoa, kupendwa na kukubalika na wanawake ni moja ya hatua muhimu katika maisha ya Mwanaume yeyote mwenye utambuzi.

Si rahisi kufanikiwa katika maisha ikiwa unamigogoro na hawa viumbe. Watu makini hulijua hili. Wanawake ndio viumbe pekee ambao unaweza kuwatumia kama ngazi ya mafanikio yako. Kwa kulitambua hili basi utaungana na mimi kuwa Kupendwa na kukubalika na wanawake ni moja ya ndoto yako katika kutimiza maendeleo yako.

Wachungaji na wanasiasa wanalijua hili, Wasanii na wafanyabiashara pia wanafahamu jambo hili. Ukipendwa na kukubalika na wanawake basi Dunia ipo mikononi mwako.

Mambo yatakayokufanya upendwe na ukubalike na wanawake popote pale ulipo;
1. Kujipenda mwenyewe
Wanawake wanapenda vijana au wanaume wanaojipenda. Vijana wasafi na watanashati. Kujipenda hapa inahusu mavazi, usafi wa mwili, afya kwa minajili ya mazoezi au hata kazi itakayoufanya mwili wako uonekane shupavu. Ukijipenda lazima wanawake wajigonge kila uchao.
Hii itakufanya uwe na good outlook yenye mvuto wa kimapenzi. Wanawake wanavutiwa na watu wenye mvuto mzuri kama vile wanaume tunavovutiwa na wanawake wazuri.

2. King of Drama
Wanawake wanapenda vijana wachangamfu, wacheshi na waigizaji. Wanawake hupenda wanaume wenye maneno matamu, Swagz za kimataifa, wanawake wanapenda kuishi katika ndoto hivyo ukimwambia nitakujengea jumba kubwa na gari nzuri hata kama si kweli basi wao hufurahi. Ni jambo baya na kosa la kiufundi kumwambia ukweli mwanamke. Kwa mfano unamwambia sitaweza kukununulia gari kwa hali niliyonayo. Hivi unategemea huyo binti atakukubalia. Wanawake wanapenda matumaini na faraja.

Pia wanapenda kucheka na kufurahi, hivyo ukiwa mtu wa kuwafanya wanawake wacheke kila mara ni rahisi kuwapata bila kujali umri, maumbile na elimu zao.

3. Kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Mwanaume anayejituma ni rahisi kupendwa na kukubalika kwa wanawake. Wanawake hujua kuwa mwanaume anayejituma ni mwanaume rijali ambaye huweza kuihudumia familia yake. Pia kama umeanzisha biashara yako ukawa na sifa hii basi wanawake watamiminika kukuunga ili biashara yako ikue. Watakachohitaji kutoka kwako ni heshima, kauli nzuri na nidhamu. Ukianza dharau basi utaula wachuya.

4. Kujiamini na sauti yenye bashasha
Ukiwa na kauli na maneno matamu yenye itifaki za kiume lazima wanawake wakupende. Wanawake hupenda wanaume wenye kauli zenye msimamo hasa kwenye ishu muhimu. Hupenda kauli za mzaha na utani. Hupenda kauli za kujali kama vile pole, Ahsante, Umependeza, Karibu mrembo, n.k.
wanawake hupenda kuwaambia wanaume maneno haya; utaweza wewe, huniwezi, huwezi kunipiga, huwezi kunitunza, n.k Wakishasema hivyo hukuangalia usoni na ndipo watatambua jinsi gani usivyojiamini. Na pia watasikiliza jibu lako. Hapo lazima uongee kwa ujasiri ukijiamini ili mtoto aone ukweli japokuwa unamuongopea.
Wanawake wanapendwa kudekezwa kuanzia kwenye kauli mpaka matendo.

5. Kushinda mitihani ya maisha
Unapokutwa na changamoto fulani lazima ujue kuwa wapo watu wanakutizama. Wanawake ndilo kundi kubwa kutokana nan hulka yao ya umbea. Ukishindwa jambo lolote lile liwe kubwa au dogo basi unapoteza mvuto kwa wanawake waliowengi. Wanawake hutumia falsafa ya kuwa Mwanaume hashindwi. Ndio sababu mwanaume anapoishiwa kisera(kauli na mitongozo), kimuonekano(kimavazi) na kiuchumi ni rahisi kukimbiwa na hawa viumbe.
Lazima ushinde katika mitihani ya maisha.

Waliooa watanikubalia kuwa, wake zao huwapa mitihani mingi kupima uanaume na akili ya mwanaume.

Kati ya Hivyo hakuna sehemu PESA nimeitaja, Ila mambo hayo ndiyo yatakufanya upendwe na kukubalika kwa wanawake

Nawasilisha
kama huna hela ata ufanye hayo hauwezi ukapendwa
 
Mimba ya sungura ina muda mfupi sana ukilinganisha mimba ya tembo. Miezi 6 ilinipatia kilicho bora.
[emoji23] [emoji23] kilicho bora kipi mkuu!hiyo uliyosema ilikuwa ni kama kumsukuma aliyeinama?[emoji23]
 
Kweli kabisaaaa.
Maana yote uliyoyataja ndiyo yenyewe.
Pesa hujaitaja lakini kujituma na kufanyakazi kwa bidii kunafanya upate pesa.
Big up
 
Acha kujidanganya mkuu.
Watu hujiamini kwa vitu natural na si Artificial. Pesa ni Man-made thing haifakufanyi upendwe bali ile tabia yako iliyokufanya upate pesa ndio huweza kukufanya ujiamini na ukubalike kwa hao viumbe. Hata hivyo, wanawake hawapo kama unavyowafikiria mkuu.
Wasemacho si wanachokimaanisha. TAKE FROM ME
We unawajua wanawake vizuri
 
Back
Top Bottom