Ukiukwaji wa maadili kwenye taasisi za fedha

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Ndugu zanguni wa JF leo nimeona nilitoe hili bomu, kwani kuna mambo ambayo baadhi ya wadau kwenye hizi taasisi wamekuwa wakifanya au kufanyiwa na wao kuona ni kawaida kabisa. Angalia mambo yafuatayo ambayo ni kinyume cha maadili:
  • Bank Tellers: kwa baadhi ya bank kubwa hapa nchini imekuwa ni jambo la kawaida kwa Tellers kupewa kitu kidogo na wao kupokea ili watoe huduma fasta. Mfano dhahiri ni pale baadhi ya watu wanapokwenda ku-withdraw/ ku-deposit fedha zao na kukutana na foleni kubwa, hapo ndipo wanapotumia mwanya huo kupatiwa huduma chapchap kwa kutoa kitu kidogo e.g. 5000; 100,000 kulingana na kifungu kinachotakiwa kuwekwa au kutolewa. Na ndo maana leo hii kazi ya ubenki teller inaonekana ina marupurupu yasiyo rasmi, lakini hii ni kinyume cha taratibu za kibenki sababu baadhi ya watumishi wamefikia viwango vya kulazimisha na kuona ni haki yao kupewa kitu chochote. Baadhi ya benki zimeunda sera ya ku-report zawadi zozote zinazotolewa kwa watumishi wao ( Gift reporting policy)

  • Loan Officers ( Maafisa Mikopo): hawapo nyuma kwani kuna tabia ambayo inafanya na baadhi yao ambayo ni kinyume na taratibu za waajiri wao, kwanza nianze kwa kusema mikopo sio dhambi na ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu na cha muhimu ni kuwa na malengo kabla ya kukopa. Ila wapo baadhi ya maofisa ambao wamefaidika au wanaendele kufaidika kupitia migongo ya watu wengine. leo hii imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya maofisa mikopo na wakopaji kufikia makubaliano ya kugawana sehemu ya kiasi kitakachokopeshwa kwa mkopaji.
Mfano: mtu anapokopa Tsh milioni 15 na ili mambo yako yaende fasta anatoa ahadi ya kumpatia afisa mikopo let say 2 Millions akifanikisha. Na mara ingine maafisa mikopo wamekuwa wakiwazungusha wakopaji kwa makusudi ili tu mkopaji aahidi kitu chochote. sisemi kwamba kila mkopaji anayecheleweshewa mkopo wake kunakuwa ya rushwa, hapana. Mara nyingine mkopaji anakuwa hajafikisha vigezo ambavyo ni lazima atimize ndo apewe fungu lake.

Madhara yake: endapo kuna mazingira ya rushwa ( ambayo nimeyaeleza hapo juu) mara nyingi maafisa mikopo huishia kutengeneza mikopo mibovu( Non-performing Loans). Na hii ni kwa sababu loan officer atakuwa anafanya kila liwezekanalo ili akifanikisha apate mgao wake. Ni mchezo wa kawaida sana siku za leo kuona maafisa mikopo wanawasaidia wateja hadi manipulation ya financial statements.
  • Benki Kuu (BOT) na Kushindwa kudhibiti riba: Sote tunashuhudia ni jinsi gani taasisi za fedha zinavyojipangia riba ya kuwatoza wateja wake. Huku wahanga wakubwa wakiwa ni waalimu pamoja na wajasiriamali wadogowadogo ( low income earners). Taasisi hizi hasa Microfinance ( e.g. Bayport, Platinumcredit, Blue finance, Finca, Easy finance, Daladala Saccos just to mention few of them) zinatumia ujanja wa kihesabu kuwatapeli wakopaji ( Re-payment Schedule). Wakopaji wengi huwa hawtizami kwa umakini hii re-payment schedule na kuona mzigo mzito uliokuwepo mbele yake.
Licha ya hayo yote lawana nyingi ninapeleka kwa Benki kuu ya taifa, na ninadiriki kusema ya kwamba inachelewa sana kulishughulikia suala hili za tozo kubwa ya riba kwa wajasiriamali. Hata kama kuna madai ya kwamba watanzania hawakopesheki, ati kuna risky kubwa sana na ndo maana riba iko juu(25% - 30%). Lakini mi naamini ya kwamba hata nchi ambazo tunazisikia ya kwamba wananchi wake wanakopesheka ni kutokana na jitihada za serikali kutengeneza mazingira mazuri ili watu wake waweze kukopesheka ( Ku-reduce ile risky) na hivyo riba itapungua tu.
Leo hii watanzania hatuna National IDs, hatuna Credit Monitoring agency ( Kuna moja nasikia imeanzishwa na TIB ambayo sijui ni kisiasa au la) hatuna National Credit Act ili tuondakane na recklessy lending.

  • Wakopaji mapapa wanaozichafua benki zetu: Hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa na Makampuni feki pamoja na watu binafsi ambao kazi yao ni kukopa huku kisha kukimbilia kule tena mamilioni ya fedha. Jamani hali hii inaonekana ni halali kabisa, Mfano kuna baadhi ya watu wenye nyadhifa zao serikalini, kwenye vyama vya siasa masilani CCM, Wafanyabiashara Maarufu ambao ni mafundi wa kuandika michanganuo ya biashara ( Business plans) na kulamba mamilioni ya fedha kisha kutokomea. Watu hawa ni mafundi sana kwa sababu wana-collude na wafanyakazi wa ndani na kisha wanatengeneza mikopo ambayo sio binding kisheria. Mtu huyo anatokomea, alikopa CRDB aka-default, Kesho anakwenda Kukopa-NBC aki-default na Huko anawakimbia anakenda Kwenye Benki Nyingine yeyote anayoitaka yeye. Wana-enjoy hali bubu iliyopo ( BOT Kama Nyoka Asiye na Meno)
Mambo haya yana-Impact Kiuchumi jamani, hivi ni mojawapo ya vitu vinavosababisha middle and lower class waendelee kuumizwa na riba kubwa zinazotozwa. Kwa upande mwingine ninawapongeza BOT kwa uamuzi wao wa kuanzisha programu ya kuzi-discourage local banks kuwekeza kwenye hati fungani (Treasury Bills/Bonds), hii nadhani itachochea ushindani kwenye soko la mikopo na hivo kuwafanya wakopeshaji washushe riba zao.

Mwisho kabisa napenda kuishia hapa kwa kuwaomba Waalimu wawe makini sana hizi microfinance zinazotoa mikopo kwa kuwaacha na quote ifuatayo " Nyuki hakumbatiwi, Ncha ya Mkuki Haipigwi Konzi"

Kwa maoni tuwasiliane kupitia developtz@gmail.com
 
BOT mbona unawapa pongezi kwa kazi ndogo sana hiyo ya mnada wa hati fungani kufanyika kila baada ya 3months badala ya kila mwezi!!!!!

bado hawajatekelzaa majukumuu yaoo at least ipasavyoooo!! shame on them..
 
Yeah Mkuu nakubaliana na wewe lakini tatizo ni kwamba politicians nao wana-interfere sana shughuli za BOT, Nadhani Prof. Beno Ndulu

inabidi apigwe orientation course kwenye reserve banks kubwa kubwa ambazo ni independent ili ajue namna atakavyofanya restructuring benki yatu iweze ku-perform
 
Ni kweli yote yanatokea.watumishi wabadilike,ni kujidhalilisha kupokea kitu kidogo kama 5000,ni sawa na ba medi anayeomba bia/kinywaji
 
Back
Top Bottom