Katikomile
JF-Expert Member
- Jul 12, 2007
- 471
- 74
Tatizo sugu katika hii mitoko ni baadhi ya wanawake kwenda na kampani yao/zao. Utakuta mtu kapewa mwaliko, anaamua kubebana na mashoga zake watatu au wanne, eti wanamsindikiza! Hata kama ni mmoja, kwani uliambiwa uende na mtu? Sasa soma mtiririko ufuatao, ujifunze kitu kama una tabia hiyo au ulikuwa na mpango wa kufanya hivyo.
INAKUPUNGUZIA SIFA
Kama ulikuwa ni mpenzi wa jamaa huyo, hapa utakuwa umeshapunguza credit za kuwa mke. Kwa vyovyote vile, hata kama hatakuambia, atabaki na donge moyoni. Atakuwa na maswali mengi sana, lakini hatakuwa na majibu na muda wote atakuwa amejenga tabasamu la kutengeneza.
Amka. Kama una tabia hii na una mpango na mshkaji acha, other ways uwe na nia ya kumchuna na kuanza zako, lakini kama unataka kuingia kwenye ndoa, utampoteza!
ATAJUA UNAMCHUNA!
Maswali kichwani mwake yatakuwa mlima, lakini kubwa litakalotawala ni ile hali ya kuhisi kabisa kwamba unafanya buzi. Yes...unamfanya buzi, kwasababu kama ni kinyume chake, kwanini uongozane na kampani? Kama alikuwa na nia wewe, haraka atageuka, ana haja gani ya kuwa na mwanamke mfujaji wa fedha?
UTAMWOGOPESHA...
Kama ndiyo anakutaka na wewe kwa mara ya kwanza, utamwogopesha kuongea chochote. Kwanza atajua umekuja na watu ili asiweze kuongea, lakini pia ataogopa kukualika katika mtoko mwingine, maana utakuwa umejipotezea sifa ya ustaarabu.
BAJETI YAKE VIPI?
Vyovyote itavyokuwa, utakuwa hujui ana bajeti kiasi kwa ajili ya siku hiyo, lakini kubwa zaidi hufahamu ana kiasi gani kwenye pochi yake siku hiyo. Hata kama ungekuwa wewe, kwa hakika usingeona bajeti yako ikiharibiwa bila mpangilio.
Halafu utafiti usio rasmi unaonyesha kwamba, marafiki wanaobebwa katika mitoko isiyo yao, huwa wanakula na kunywa vinywaji vya bei ghali zaidi hata mualikwa. Hili ni tatizo, kama hana pesa za kutosha na network ya ATM haisomi itakuwaje?
UNAWEZA KUUMBUKA
Iwe unamkomoa, hujui au ni bahati mbaya, lakini vipi kama utakutana na mwanaume fyatu kidogo, ambaye hajali. Unajua kitakachotokea, anaweza akalipa bili yako na yake, halafu akasema hao wengine hawakuwa kwenye bajeti yake, kwa maana hiyo ulipe wewe au wajilipie wenyewe! Aibu kiasi gani?
Mkatili zaidi, anaweza akawaacha mkaagiza sana, bili ikishakuwa kubwa anaenda kaunta na kulipa vyake tu, halafu anamwagiza aje awadai. Akija kwenu anajifanya anakwenda msalani, kumbe kawaachia msala, itakuwaje? Ukute na wewe kwenye pochi yako una elfu kumi tu, halafu bili 45,700, utaumbuka!
UMENIPATA?
Umeona eeh! Nadhani ni vizuri kama una haka katabia ukabadilika, kwani si njema hasa kwa mwanaume ambaye unatarajia awe wako. Ukipewa ofa ya mtoko, nenda peke yako.
Ukweli ni kwamba, ukibebana na wenzako unaibua hisia tofauti ambayo inaweza kukupotezea pointi za kuwa mwenzi mwema hapo baadaye.
Source: Globalpublisherstz.com